Kesi muhimu katika ulinzi wa taarifa zetu binafsi

Jan 28, 2024
96
133
Kati ya moja ya jiwe (case) muhimu kwako wewe kama mwanasheria ni hili, kesi hii iliyoamuliwa na Mahakama Kuu (MK) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sehemu sahihi ya kuwasilisha madai yanayohusiana na ulinzi wa wa taarifa binafsi nchini Tanzania.

Kweny kesi hii, mlalamikaji alifungua shauri MK na kuishitaki TIGO kwa kuingilia faragha yake na kumchafua. Walakini, mdaiwa (TIGO) aliweka pingamizi kwamba MK haina mamlaka yakusikiliza shauri linalohusu taarifa binafsi na faragha, na kudai kuwa kesi ililetwa kimakosa mbele ya MK, kinyume na sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi No. 11 ya 2022 na Kanuni zake zinavyoelekeza.

MK, baada ya kujadili, ilihitimisha kuwa kulingana na sheria husika, madai ya ulinzi wa taarifa binafsi yanapaswa kufunguliwa katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Tume). Kufuatia hayo, MK iliamua kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
UMUHIMU WA UAMUZI HUU (Kwa Wanasheria)
Uelewa wa Sheria za Ulinzi wa Taarifa Binafsi: Uamuzi huu unaelekeza jinsi kesi za faragha na taarifa binafsi zinavyopaswa kusimamiwa kulingana na sheria na kanuni za ulinzi wa taarifa binafsi. Wanasheria wanahitaji kuwa na ufahamu kamili wa taratibu za kisheria zinazohusiana na faragha na taarifa binafsi ili kuzuia kesi kutupiliwa mbali kwa sababu ya kutokuzingatia sheria husika.

Uelewa Ulioimarishwa wa Mamlaka za Kisheria: Uamuzi huu unatoa mwanga juu ya mamlaka na majukumu ya Tume. Wanasheria wanahitajika kuelewa jinsi mamlaka za kisheria zinafanya kazi na jinsi wanavyohusika katika kutatua mizozo ya ulinzi wa taarifa binafsi.

Mabadiliko katika Mikakati ya Kisheria: Wanasheria wanaweza kuwa na haja ya kurekebisha mikakati yao ya kisheria kwa kufungua kesi za faragha na taarifa binafsi katika Tume badala ya kwenda mahakamani. Hii inahitaji ufahamu wa jinsi ya kuwasiliana na kuzingatia taratibu zilizowekwa na sheria hii mpya.

N:B. Tukumbuke sheria hii ni mpya kabisa Tanzania, hivyo ni muhimu kwa aliye mwanasheria na hata asiye kuifatilia, kuisoma na kuielewa ili iwe ngao katika kulinda faragha na taarifa zetu binafsi.

#UlinziWaTaarifaBinafsi#UchambuziWaKesi#KuzingatiaSheria#HakiZaFaragha​
 

Attachments

  • Fatna Faradji Kayuga vs Mic Tanzania (PLC)Ltd (Civil Case No 125 of 2023) 2024 TZHC 815 (15 Ma...pdf
    2.8 MB · Views: 5
"An order for payment of T.shs 450,000,000/= (say four hundred million and fifty shillings only"

Hapa kingereza changu cha Ugoko au ni Typing error?
 
Back
Top Bottom