Rais Samia: Hadi Desemba 2024, Taasisi za Umma na Binafsi ziwe zimetekeleza Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,884
12,134

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atazindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, leo, Aprili 3, 2024, Ukumbi wa JNICC.

Tume hii ina majukumu muhimu kama kusimamia sheria na kushughulikia malalamiko. Muundo na taratibu za Tume zimekamilika na zinazingatia haki za faragha na usalama wa taarifa za watu.

Tume hii ni muhimu katika kukuza uchumi wa kidigitali na kuhakikisha usalama wa taarifa za ndani na nje ya nchi.

Usikose kushiriki katika tukio hili muhimu.

View: https://www.youtube.com/watch?v=3yM6DTt2Mzc

MKILIA: WANAOKUSANYA NA KUCHAKATA TAARIFA BINAFSI WAJISAJILI NA WAPATE KIBALI
Akizungumza katika Uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Emmanuel Mkilia amesisitiza Watu Binafsi na Taasisi zinazokusanya na kuchakata Taarifa Binafsi wanatakiwa kujisajili na kupata vibali vya kuendelea kufanya wanachokifanya.

Aidha, amesema “Tume ilianzishwa rasmi Mei Mosi, 2023 na itatekeleza majukumu yake Tanzania Bara na Zanzibar kwenye masuala ya Muungano.”

NAPE: UWEKEZAJI WA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI UTAIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni chombo muhimu katika kuimarisha Misingi ya Demokrasia, Utawala Bora na Utawala wa Sheria na hivyo kuzidi kuvutia wawekezaji kutoka Nje.

RAIS SAMIA: KUTOA TAARIFA YA MTU KUNAWEZA KUSABABISHA UNYANYAPAA AU MAUAJI
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam amesema baadhi ya taarifa zinaweza kutumika kuhujumu Jamii.

Amesema “Wakati mwingine taarifa ya Mtu inaweza kusababisha unyanyapaa, vurugu, vita na hata mauaji.”

RAIS SAMIA: TAASISI ZOTE ZITEKELEZE SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KABLA YA DESEMBA 2024
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuhakikisha Taasisi zote za Umma na Binafsi zinasajiliwa na zinatekeleza Sheria ya Taarifa ya Ulinzi Binafsi kabla au ifikapo Desemba 2024.

Amesema hayo wakati akiizindua tume hiyo, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

WhatsApp Image 2024-04-03 at 13.15.18_78311bb6.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

WhatsApp Image 2024-04-03 at 13.18.00_c6e91fda.jpg

WhatsApp Image 2024-04-03 at 13.17.59_07d39547.jpg

Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

WhatsApp Image 2024-04-03 at 13.19.16_007cd95a.jpg

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.
Snapinsta.app_434748722_17860714629121312_5568957596732925735_n_1080.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mohammed Khamis Abdulla akitoa hotuba ya ukaribisho na utambulisho kwenye hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Snapinsta.app_434743721_17860715574121312_7848270213932034722_n_1080.jpg

Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

WhatsApp Image 2024-04-03 at 13.23.20_ff7b4ebe.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akigusa screen ya iPad kuashiria uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

WhatsApp Image 2024-04-03 at 13.25.03_94d2b3db.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha iliyotengenezwa na kufumwa kwa nyuzi kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kuzindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

PDPC.jpg

Rais Samia amesema laiti faragha zingekuwa Wazi basi tusingetazamana

Dr Samia amesema hayo wakati akizindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na mifumo ya Usajili na Malalamiko

Source: Ayo TV
 
Binafsi namshukuru mama kwa kuliona Hilo.
Ukifika lodge hakikisha hakuna kamera chumbani especially Kama una Mambo yako.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atazindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, leo, Aprili 3, 2024, Ukumbi wa JNICC.

Tume hii ina majukumu muhimu kama kusimamia sheria na kushughulikia malalamiko. Muundo na taratibu za Tume zimekamilika na zinazingatia haki za faragha na usalama wa taarifa za watu.

Tume hii ni muhimu katika kukuza uchumi wa kidigitali na kuhakikisha usalama wa taarifa za ndani na nje ya nchi.

Usikose kushiriki katika tukio hili muhimu.

MKILIA: WANAOKUSANYA NA KUCHAKATA TAARIFA BINAFSI WAJISAJILI NA WAPATE KIBALI
Akizungumza katika Uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Emmanuel Mkilia amesisitiza Watu Binafsi na Taasisi zinazokusanya na kuchakata Taarifa Binafsi wanatakiwa kujisajili na kupata vibali vya kuendelea kufanya wanachokifanya.

Aidha, amesema “Tume ilianzishwa rasmi Mei Mosi, 2023 na itatekeleza majukumu yake Tanzania Bara na Zanzibar kwenye masuala ya Muungano.”

NAPE: UWEKEZAJI WA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI UTAIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni chombo muhimu katika kuimarisha Misingi ya Demokrasia, Utawala Bora na Utawala wa Sheria na hivyo kuzidi kuvutia wawekezaji kutoka Nje.

RAIS SAMIA: KUTOA TAARIFA YA MTU KUNAWEZA KUSABABISHA UNYANYAPAA AU MAUAJI
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam amesema baadhi ya taarifa zinaweza kutumika kuhujumu Jamii.

Amesema “Wakati mwingine taarifa ya Mtu inaweza kusababisha unyanyapaa, vurugu, vita na hata mauaji.”

RAIS SAMIA: TAASISI ZOTE ZITEKELEZE SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KABLA YA DESEMBA 2024
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuhakikisha Taasisi zote za Umma na Binafsi zinasajiliwa na zinatekeleza Sheria ya Taarifa ya Ulinzi Binafsi kabla au ifikapo Desemba 2024.

Amesema hayo wakati akiizindua tume hiyo, leo Aprili 3, 2024 katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

View attachment 2952727

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

View attachment 2952729
View attachment 2952733

Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

View attachment 2952736

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.
View attachment 2952860
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mohammed Khamis Abdulla akitoa hotuba ya ukaribisho na utambulisho kwenye hafla ya uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
View attachment 2952862
Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

View attachment 2952739

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akigusa screen ya iPad kuashiria uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

View attachment 2952741

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha iliyotengenezwa na kufumwa kwa nyuzi kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye mara baada ya kuzindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Aprili, 2024.

View attachment 2952808

Kuna mitandao ya wakopeshaji huko online wamekuwa wakiwachafua waliokopa pesa,Sasa wajiandae kulipa mabilioni ya fidia.
 
Haiwezekani unawasilisha taarifa mfumo huu na huu hauna taarifa ni uhuni.

Kama NIDA wana taarifa zangu, NHIF wana taarifa zangu, Benki kuu wana taarifa zangu kama mtumishi iweje nidaiwe taarifa tena?

IT mnakwama wapi.
 
Hao wameambiwa tu lakini kazi ipo. Kwani mifumo kusomana hata tangia jana mpaka sasa ingesha somana
Sasa mpaka Disemba ndio nini maana yake?
 
Back
Top Bottom