Kwanini Israel inapewa msaada wa kijeshi/ silaha na Marekani?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
38,098
47,090
Katika mambo ambayo yamekuwa yakieleweka vibaya, kukanganya na pia kuzua dhihaka kutoka kwa watu wasioipenda Israel ni pamoja na hili la kupewa misaada wa jeshi/ silaha na Marekani pamoja na kuwa ni nchi tajiri iliyoendelea.

Ni vizuri tujifunze na kuelewa mambo bila ushabiki, kuna sababu kadhaa muhimu Israel kupewa msaada na Marekani.

1. Kwanza karibia nchi zote duniani ikiwemo US huwa kwa kiasi fulani zinajiendesha kwa mikopo, kwa hiyo ikitokea unaweza kupata pesa za bure sehemu nyingine ni jambo la kufurahia na huwezi kuzikataa kwa sababu inakuwa umeepushwa kukopa na kuingia madeni. Israel wataendelea kuzipokea na kuzifurahia pesa za bure za US na Ulaya.

2. Taasisi za ushawashi za kutetea maslahi ya Israel "Jewish/ Israel lobby" huko Marekani ni mahiri sana, zenye ushawashi mkubwa kwa jamii kubwa ya Wamarekani na zinajua kusuka mipango na mikakati kupitia wanasiasa wa Marekani kuipatia Israel pesa. Wanaweza kushawishi matajiri kutofadhili kampeni za uchaguzi za baadhi ya wanasiasa wasiowakubali au kufadhili kampeni za wapinzani.

3. Marekani ni kama Inawalipa Israel zaidi badala ya msaada. Pesa inazowapa Israel ni zaidi ya msaada kwa sababu ina usemi na maamuzi makubwa katika biashara ya silaha ya Israel. Waisrael ni watu wenye akili sana kiteknolojia na wanaweza kushindana vikali na Marekani vikali katika utengenezaji wa Silaha za hali ya juu za kila aina. Wamarekani wasingependa kuona ushindani wa aina hiyo utakaopunguza faida kwa kampuni zao na pia hata kupelekea baadhi ya silaha kuangukia mikononi mwa adui zake kama Israel itaachwa huru kuuza vyovyote katika hiyo biashara na pia ikiwemo wanasayansi wake kununuliwa au kufadhiliwa na mahasimu kama Urusi, hiyo inayoitwa msaada ni sehemu ya gharama hiyo kuepusha hayo yasitokee.

4. Marekani inadumisha mshirika wa uhakika wa Mashariki ya kati. Katika Mataifa mengine yote ya Mashariki ya kati ambayo ni washirika wa Marekani Israel peke yake ndio haitegemewi kubadilika kuwa kinyume au adui wa Marekani wakati wowote.

5. Udini, Ukristo ulianzia Israel. Hii japo sio sababu ya msingi sana ila kuna Wamarekani wengi ambo wengine wako kwenye vyombo vya maamuzi wanaiona Israel ni sehemu muhimu katika dini yao.

6. Tamaduni na tunu(values) zinazoshabihiana kati ya Israel na West. Israel ni demokrasia imara yenye kuzingatia uhuru wa raia wake na uchumi unaoeendeshwa na soko. Hakuna nchi nyingine ya Mashariki ya kati inayokaribiana na West kama Israel.

7. Kujisikia vibaya "Guilty feeling" ya US/West kutokana na mauaji ya kiyahudi "holocaust" yaliyofanywa na Ujerumani pamoja na washirika wake kuelekea vita vya pili vya dunia. US na mataifa mengine kama Uingereza yanajiona hayakuwajibika vya kutosha wakati huo kupunguza au kuepusha kabisa.
 
Uturuki kaongezwa NATO kimkakati,Ila NATO Ina wenyewe,UK, France, German..na ndiyo walioanzisha Jewish state of Palestine
Ujerumani kakaribishwa NATO na Uturuki pamoja na mataifa mengine 12 zikiwemo Canada, Norway, Ureno n.k
 
Nimelielewa swali lako,
Naona Urusi inapokea pia silaha kutoka Iran, China na Korea Kaskazini!
Na ndo maana yangu! Urusi inapokea shehena za silaha kutoka kwa washirika wake umesahau kuitaja south Africa, Nchi nyingi duniani zinasaidiana silaha iwe mauziano, misaada au namna yeyote Ile, ila misaada kwa Israel inakua nongwa kwa sababu kawashika pabaya mashariki ya kati
 
Hapokei ana nunua kama ambavyo nchi yako inanunua pia.
Tofautisha kupewa na kununua.
 
Na ndo maana yangu! Urusi inapokea shehena za silaha kutoka kwa washirika wake umesahau kuitaja south Africa, Nchi nyingi duniani zinasaidiana silaha iwe mauziano, misaada au namna yeyote Ile, ila misaada kwa Israel inakua nongwa kwa sababu kawashika pabaya mashariki ya kati
Urusi hapokei msaada wa silaha bali ana nunua silaha, Urusi si nchi ya kupokea misaada maana anajiweza kifedha.
Punguza uzuzu.
 
Katika mambo ambayo yamekuwa yakieleweka vibaya, kukanganya na pia kuzua dhihaka kutoka kwa watu wasioipenda Israel ni pamoja na hili la kupewa misaada wa jeshi/ silaha na Marekani pamoja na kuwa ni nchi tajiri iliyoendelea.

Ni vizuri tujifunze na kuelewa mambo bila ushabiki, kuna sababu kadhaa muhimu Israel kupewa msaada na Marekani.

1. Kwanza karibia nchi zote duniani ikiwemo US huwa kwa kiasi fulani zinajiendesha kwa mikopo, kwa hiyo ikitokea unaweza kupata pesa za bure sehemu nyingine ni jambo la kufurahia na huwezi kuzikataa kwa sababu inakuwa umeepushwa kukopa na kuingia madeni. Israel wataendelea kuzipokea na kuzifurahia pesa za bure za US na Ulaya.

2. Taasisi za ushawashi za kutetea maslahi ya Israel "Jewish/ Israel lobby" huko Marekani ni mahiri sana, zenye ushawashi mkubwa kwa jamii kubwa ya Wamarekani na zinajua kusuka mipango na mikakati kupitia wanasiasa wa Marekani kuipatia Israel pesa. Wanaweza kushawishi matajiri kutofadhili kampeni za uchaguzi za baadhi ya wanasiasa wasiowakubali au kufadhili kampeni za wapinzani.

3. Marekani ni kama Inawalipa Israel zaidi badala ya msaada. Pesa inazowapa Israel ni zaidi ya msaada kwa sababu ina usemi na maamuzi makubwa katika biashara ya silaha ya Israel. Waisrael ni watu wenye akili sana kiteknolojia na wanaweza kushindana vikali na Marekani vikali katika utengenezaji wa Silaha za hali ya juu za kila aina. Wamarekani wasingependa kuona ushindani wa aina hiyo utakaopunguza faida kwa kampuni zao na pia hata kupelekea baadhi ya silaha kuangukia mikononi mwa adui zake kama Israel itaachwa huru kuuza vyovyote katika hiyo biashara na pia ikiwemo wanasayansi wake kununuliwa au kufadhiliwa na mahasimu kama Urusi, hiyo inayoitwa msaada ni sehemu ya gharama hiyo kuepusha hayo yasitokee.

4. Marekani inadumisha mshirika wa uhakika wa Mashariki ya kati. Katika Mataifa mengine yote ya Mashariki ya kati ambayo ni washirika wa Marekani Israel peke yake ndio haitegemewi kubadilika kuwa kinyume au adui wa Marekani wakati wowote.

5. Udini, Ukristo ulianzia Israel. Hii japo sio sababu ya msingi sana ila kuna Wamarekani wengi ambo wengine wako kwenye vyombo vya maamuzi wanaiona Israel ni sehemu muhimu katika dini yao.

6. Tamaduni na tunu(values) zinazoshabihiana kati ya Israel na West. Israel ni demokrasia imara yenye kuzingatia uhuru wa raia wake na uchumi unaoeendeshwa na soko. Hakuna nchi nyingine ya Mashariki ya kati inayokaribiana na West kama Israel.

7. Kujisikia vibaya "Guilty feeling" ya US/West kutokana na mauaji ya kiyahudi "holocaust" yaliyofanywa na Ujerumani pamoja na washirika wake kuelekea vita vya pili vya dunia. US na mataifa mengine kama Uingereza yanajiona hayakuwajibika vya kutosha wakati huo kupunguza au kuepusha kabisa.
Hamas wasingeichokoza Israel kusingekuwepo ugomvi
 
Israel ni kijitaasisi cha Marekani na Uingereza ambacho kilipachikwa mashariki ya kati kwa ajili ya kulinda masilahi ya Mataifa yao, hayo mengine ni ngonjera na tumba tu.
Kinalindaje maslahi ya marekani embu fafanua?
 
Kwani israel ikipewa misaada na marekani nyie wafia dini inawauma nini ? Kwani ni pesa zenu mmechangishwa huko misikitini ? Mbona mnauchungu na pesa za marekani ila hamna uchungu na pesa za iran kusaidia magaidi wa hezbollah na hamas kufanya ugaidi
 
Mbona hata Ukraine wanapata msaada wa pesa nyingi tu na silaha kutoka marekani?

Mengine porojo tu kubwa ni mwendelezo wa marekani kupitia huyo kibaraka wake hapo Middle East kuendelea kutaka kuitawala dunia ila mambo yanakwenda kubadilika haraka sana. Mataifa Kama urusi, China na Iran yanaongoza mapambano ya kuvunja huo mwiko.
 
Back
Top Bottom