Kwanini Hans Poppe na wenzake walitaka kumpindua Mwl. Nyerere? (SEHEMU YA 1️⃣)

Jan 28, 2024
48
48
HATIBU GADHI & OTHERS versus REPUBLIC, 1996.
Screenshot_20240414-152007.jpg
Karibu katika sehemu ya kwanza ya uchambuzi wa kina wa kesi hii ya kihistoria yenye mengi yaliyojificha ama yasiofahamiwa na watanzania wengi wa kizazi cha sasa. Katika makala hii ya kusisimua tutachambua kwakina kwanzia historia ya wahusika (hasa Hans Poppo), Kabla ya tukio, sababu zilizopelekea watu hao kutaka kuipindua serikali, kesi zilizofunguliwa dhidi ya wahusika na yote yamuhimu unayotakiwa kuyafahamu kuhusiana na kesi hii.
Tahadhari: Makala hii imeandaliwa kwa madhumuni ya kutoa ufafanuzi na elimu kwa umma. Hakuna lengo lolote baya lililokusudiwa katika uandaaji wa makala hii. Pia ni muhimu kufahamu kuwa fafanuzi uliotolewa unazingatia sheria na kanuni zilizokuwa zinatumika wakati huo. Na mwisho kabisa, makala hii haipaswi kutumiwa kama ushauri wa kisheria wala kuchukuliwa kama msingi wa kufanya maamuzi yoyote ya kisheria.

JARIBIO LA MAPINDUZI TANZANIA (1983)
Mwaka 1996 iliamuliwa moja ya kesi mashughuli na muhimu sana Tanzania, baina ya Hatibu Gandhi na Wenzake dhidi ya Jamuhuri iliyokuwa ni rufaa iliyofanywa na Bwa. Gandi na wenzake (akiwemo Zachariah Hans Poppe),waliokua wameshitakiwa vifungo vya maisha katika mahakama kuu kutokana na makosa ya uhaini waliyoyatenda mnamo mwaka 1983 kinyume na kifungu namba 39(2)(a) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu, sura ya 16. But wait, Ilikuaje mpaka Hans Poppe akahusika katika kesi hii ya uhaini na kujaribu kuipindua serikali ya Nyerere🤔?, Ulisukwa vipi mpango huu wa mapinduzi🤔?, Serikali iliwezaje kuustukia na kuukabili mpango huu🤔?Makala hii inakwenda kujibu maswali yote hayo kwa kuelezea kwa kina chanzo na namna mzee wetu Hans Poppe alivyohusika. Lakini kabla ya yote ni muhimu kufahamu historia ya Hans Poppe mwenyewe kwanza.
HISTORIA FUPI YA HANS POPPE
Screenshot_20240414-053436.jpg
Inawezekana wengi wetu tumemfahamu mzee wetu Poppe kutokana na umahiri wake wa kusimamia usajili katika team ya mpira wa miguu ya Simba S.C, lakini nyuma yake kuna historia yenye kusisimua mnoo. Labda tuanze, huyu Zacharia Hans Poppe ni nani? Poppe ni mtoto wa aliyekua kamanda mwandamizi msaidizi wa jeshi la polisi mkoa wa kagera (SACP Hans Poppe) ambaye ni moja ya wajerumani wachache waliobaki kuitumikia Tanzania. Kwenye makuzi yake Poppe ameweka historia Tanzania kwa kuwa mtu wa kwanza kushika cheo cha Luten Usu akiwa na umri wa miaka 19 tangu kuanzishwa kwa JWTZ.
4.1.UncleZaka.jpg

Mzee SACP Hans Poppe aliuwawa na askari wa Idi Amin mnamo August 24, 1971 katika mpaka wa Uganda na kisha wanajeshi hao wakauchukua mwili wake na kwend nao Uganda. Lakini pia Zacharia Poppe ni miongoni mwa mashujaa waliopigana katika vita ya kagera, na baada tu ya vita ya kagera Zack Poppe alienda uganda kwaajili ya kufanya upelelezi na kutka kujua ni wapi baba yake amezikwa lakini kwa bahati nzuri aliupata mwili wa baba yake katika hospitali ya taifa ya Uganda na kufanikiwa kuurudisha nnchini Tanzania kwaajili ya mazishi mnamo mwaka 1979.
WhatsApp Image 2019-01-15 at 22.22.51.jpeg

Historia hii fupi imeeleza machache kati ya mengi yaliyupo nyuma ya historia ya Hans Poppe, hata hivyo kama ukihitaji kusoma history hii kwa urefu zaidi ingia hapa. Lakini swali linabaki pale pale, ni kwanini Zacharia Hans Poppe (Poppe) aliingia katika njama za kutaka kuipindua serikali ya Nyerere?
CHANZO CHA NJAMA ZA UHAINI
Kuna moja ya story maarufu sana inayozungumzia vita ya kagera kama chanzo cha jaribio hili la uhaini, lakini hapa nitazungumzia chanzo halisi kutoka katika vyombo na vitabu vinavyo aminika.

Kujua chanza cha njama hizi zilizopelekea jaribio la mapinduzi, tutasafiri hadi nyuma kabisa kati ya mwaka 1964 hadi 1985, wakati Tanzania inapitia katika kipindi cha 'Ujamaa' chini ya Raisi wa awamu ya kwanza Mwl. Nyerere.
feb-29-2012-president-nyerere-breaks-ground-at-an-iyamaa-village-E13BGA.jpg

Itakumbukwa katika miaka hiyo ya ujamaa, dunia ilikua inapitia katika anguko kibwa la kiuchumi, ambapo nnchini Tanzania mwaka 1982 ndo ulikua mwaka mgumu zaidi kiuchumi katika historia ya nnchi. Janga hili lilipelekea Tanzania kuanzisha sheria kali inayojulikana kama Sheria ya Kupambana na Uharibifu wa Kiuchumi (Sheria Maalum) ya Mwaka 1983 ama The Economic Sabotage (special provisions) Act, 1983, ili kukabiliana na wimbi la uhalifu wa kiuchumi.

Anguko hili la kiuchumi na hali ngumu ya kimaisha ilipelekea watanzania wengi kuanza kupinga sera za Mwl Nyerere za Ujamaa na utawala bora, na wengine wakiamini yeye na serikali yake ndio chanzo cha mateso hayo yote ya kiuchumi, na wengine wakiona kama Mwl, ameshindwa kuwakomboa katika janga hili. Moja ya watu waliochoshwa na anguko hili na ukosekanaji wa mahitaji muhimu nnchini alikua mzee wetu Hans Poppe na wenzake waliokuwa maafisa wa JWTZ kipindi hiko. Katika moja ya vitabu mashughuli kijulikanacho kama 'Nyerere & Africa: End of an Era' kilichoandikwa na Godfrey Mwaikikagile kilichoeleza juu ya Tukio hili, Mzee Poppe alinakiliwa akisema. Nanukuu​
"Baadhi yetu tulichoshwa na ugumu wa hali ya maisha na tukaamua kutafuta mabadiliko. Chaguo pekee la kufanikisha mabadiliko wakati huo ilikuwa kupitia matumizi ya nguvu. Hatukuwa na kitu cha kibinafsi dhidi ya Nyerere. Kitu pekee kilikuwa ni kwamba alizungukwa na wanafiki ambao kuendelea kwao kunategemea kudumisha hali ya sasa."
Hivyo basi ni wazi kwamba kilichopelekea mzee wetu Hans Poppe na wenzake kutaka kuipindua serikali ya Nyerere ilikua ni anguko la kiuchumi lililowaathiri zaidi watanzania mwaka 1982 na si kwamba walikua na chuki yeyote dhidi ya Mwl Nyerere bali Uchumi. Nadhani kwa leo itakua busara kama tukiishia hapa, japo ndo kwanzaa picha linaanza. Anyway, Je, ni kena nani waliopanga njama hizi pamoja na Luten Hans Poppe? Nini kiliwakuta? Na nani aliwasaliti mpka kupelekea wao kukamatwa?

Majibu yote ya maswali haya yatapatikana katika sehemu ya pili ya mkasa huu. Tukutane katika muendelezo wa makala hii tamu yenye kuelimisha, kukumbusha, kufafanua na kusisimua.
 
Back
Top Bottom