Jihadhari na makampuni ya Kitanzania yanayoagiza magari

Okay nimekuelewa kuwa mna act kama middle man kufanikisha biashara.

Sina tatizo na bidhaa nyingine na pia na jukwaa lenu nimeingia kwny link sijaielewa.

Ishu yangu ni hawa wauzaji magari walioibuka kama uyoga wanaliza sana watu hasa hasa kina dada na watu wa maofisini....

Wanakuambia lipia nusu then unamalizia gari ikifika na wanakusajilia na kukukatia bima bure ili hali washakuchapa hela na gari unaletewa magumashi kabsa.....
Asente kwakunielewa, naomba unisaidie baada y akuingia kwenye website yetu umekwama wapi ili tupafanyie kazi inawezekana kuna watu wengi wanakwama kama wewe wanashinwa kutoa mrejesho kama wewe ulivyo nisaidia kuniamba tatizo , jambo la pili kwenye biashara za kutanguliza pesa office peke yake sio security mzuri.
 
Alaf Wanavimba Sanaa Kujiona Wako Makini Kumbe Janja Janja Tu Na Hela Za Watu.

Wadau Tumieni Makampunzi yanayo jielewa...like SBT na BeFoward. High Quality & Transparent Service With Significant Records On Customer Satisfaction.

Achaneni na Car Dealers Uchwara.

Thank Me Later
Sure boss.....
 
Asente kwakunielewa,naomba unisaidie baada y akuingia kwenye website yetu umekwama wapi ili tupafanyie kazi inawezekana kuna watu wengi wanakwama kama wewe wanashinwa kutoa mrejesho kama wewe ulivyo nisaidia kuniamba tatizo , jambo la pili kwenye biashara za kutanguliza pesa office peke yake sio security mzuri.
Kukikucha nitakupa feedback now ngoja nipumzishe fuvu....
 
Habari wa JF,

Katika pita pita zangu mitandaoni hasa JF na instagram nimeona kuna kampuni/watu wanaofanya huduma za kuagiza magari nje kwa masharti ya kulipia nusu na kumalizia kiasi kilichobaki baada ya gari kufika. Mengi ya makampuni hayo (Sisemi wote) ni "MATAPELI WAKUBWA SANA" na huu ni mchezo ambao huwafanyia wateja wao.

1. Huwa wanapost gari kwenye mitandao either wameliona kwenye site za magari au wana picha zake.

2. Baada ya kupost wateja wataliulizia na wanakuambia lipo.

3. Then watakufikisha kwenye ofisi zao nyingi zipo posta na maeneo ya mwenge- sinza- mlimani city.

4. Mtaingia mkataba na wewe kufanyia malipo gari hilo nusu. Hapa mnaweza kuwa hata wateja wanne mnafanyia malipo gari moja.

Baada ya malipo ndio mchezo unaanza.

Kwanza hawatakuonyesha chasis number ya gari na pia watakutajia km chache mno lets say between 40,000-70,000 ila kamwe hawatakupa picha ya odometer.

Baada ya hapo jamaa huwa wanaingia mzigoni kuanza kutafuta gari inayofanana na ile uliyoagiza may be kwa rangi.

Wakiipata huko japan kwa bei rahisi watakuuagizia ila zile zilizopata ajali na kufanyiwa modification. Au wakiukosa wanakutafutia hapa bongo gari kama ile na kule japan/nje wanakuagizia chasis number tu na vile vibati vya chasis number kwenye mlango then vikifika bongo wanakubandikia kwenye gari then wanakuambia gari imefika. Kumbe badala ya kuagiziwa gari umeagiziwa chasis number then gari inabandikwa na kufanyiwa usajili upya.

Kampuni hizi mara nyingi zinakua na blaah blaah ukiwauliza maswali na magari yao mara nyingi yanachelewa sana. Ili ku buy time ya kufanya manuva yao.

Unaponunuua gari mtandaoni hakikisha kabla ya kulipia unafanya yafuatayo.

1. Pata picha ya gari lote mpaka odometer.
2. Pata chasis number ya gari (Hii itakusaida kujua hilo gari lipo au laah).
3. Omba auction report/sheet. Check picha hapo chini... Wauzaji wajanja wajanja hawakupi hii hata iwaje....

USIFANYE MALIPO KAMA HUJAPEWA HIVYO VITU LA SIVYO UTAUZIWA PICHA YA GARI BADALA YA GARI.....

Kesi za namna hii zipo sana central police na washawachoka hawa watu ila bado watu wanaendelea kupigwa sana.....

Chukua tahadhari.

Siku njema.

Hongera kwa kuwasaidia watanzania wengi, hawa makanjanja wapo wengi mno.
 
Hongera kwa kuwasaidia watanzania wengi, hawa makanjanja wapo wengi mno.

Na hizi habari sambazeni na kwenye ma group ya whatsapp kwa wingi.

Sipendi dhuluma na uonevu. Kama ni Hela Mtu Atafute Ya Halali Sio Kuonea na Kudhulumu Wengine Plus ni mambo kama haya yanafanya hata wengine wanaofanya biashara hizi ki halali na wao waonekane sio wa kweli.

It Has To End.
 
Na hizi habari sambazeni na kwenye ma group ya whatsapp kwa wingi.

Sipendi dhuluma na uonevu. Kama ni Hela Mtu Atafute Ya Halali Sio Kuonea na Kudhulumu Wengine Plus ni mambo kama haya yanafanya hata wengine wanaofanya biashara hizi ki halali na wao waonekane sio wa kweli.

It Has To End.
Hapo kwenye whatsapp umenikumbusha njia nyingine wanayotumia. Huwa wanaunda na magroup ya whatsapp ukishalipia wana kuadd mule, sasa mule utakuta member kama 50 au zaidi hapo ujue kuna watu wao kama 15 hivi.... wanaanza kusifia kampuni kuwa jamaa ni wa uhakika mara tuliletewa gari and blaah blaah ili ku-win trust yako.... Ukijifanya una doubt huduma yao wataibuka watu kuwatetea kumbe ni wenzao.....

Jamaa wana mipango lukuki kupiga watu...
 
Asente kwakunielewa,naomba unisaidie baada y akuingia kwenye website yetu umekwama wapi ili tupafanyie kazi inawezekana kuna watu wengi wanakwama kama wewe wanashinwa kutoa mrejesho kama wewe ulivyo nisaidia kuniamba tatizo , jambo la pili kwenye biashara za kutanguliza pesa office peke yake sio security mzuri.
Nimepitia leo web yenu. Jana nilichanganywa na zile ads zinakuja kabla ya contents.

Pia naona forums nyingi hazijawa updated for more than a month.

Also majukwaa yamejificha sana mpaka uscroll kwenda chini ndio utaona forums mbalimbali.

Pia sijaelewa kwenye auction kuna kuweka 30,000 na ile 50,000 ina maana bid ikichukuliwa na mwingine hela inakuwa refunded?

Pia jitahidi iwe user friend kuaccess majukwaa like hapa JF ni easy majukwaa yapo juu tu ukitaka kuingia....

Screenshot_20220324-081814_Chrome.jpg
 
Sio kweli kabla ya makampuni twajwa hapo juu watu walikuwa wanunua wapi magari?
Tupe jina la kampuni inayoaminika na iliyoshika soko kuzidi kampuni tajwa hapo Juu,Hizo kampuni ni nadra kusikia malalamiko toka kwa wateja wao,hawana uhuni unaolalamikiwa na mtoa Mada,wana kasoro baadhi lakini ni zakuongeleka na za kurekebishika, Sio za kitapeli na Wizi (hawana)

Labda tutajie kampuni unayoifahamu yenye hadhi na heshima ambayo watanzania hatuijui,tusaidie.
 
Siri ya utapeli ipo hapo kwenye kuweka gharama/bei ya chini kuliko gharama halisi za huko Japan.

Note: Biashara nyingi zinazoendeshwa na Watanzania zimejaa janja janha na utapeli.
Ikiwa catering services mtakubaliana sahani ya 20,000/- ukumbini analeta sahani ya 9,000/- tena bila aibu
Kama ni gari basi ndio mambo ya kubadilishiana chasis au anakuletea lolote ilimradi brand name na rangi vinafanana.
Kaman ni ujenzi basi watajenga chini ya kiwango
Wewe umesema kiini cha tatizo hasa. Watanzania tuna akilifupi mno mno. Biashara karibu zote zimejaa ''ujanja ujanja'' na maneno mengi. Yaani mfanyabiashara haoni madhara ya kutokuwa mwaminifu hata kidogo. Ni tamaa mbele kwa mbele. Nadhani ni culture tuliyojenga kwa sababu ya uadimu wa bidhaa kipindi cha ujamaa. Muuzaji anakuwa ndiye mfalme na mnunuzi anakuwa kama mtumwa. Huwa nasema ombeni sana wachina wasije kuruhusiwa kufanya hizi biashara ndogo ndogo maana wabongo wote wenye biashara watakufa njaa.
 
Unachokizungumza kina ukweli kwa asilimia fula iko hivi kampuni za kuagiza magari kutokea nchi yoyote bila kuwa na branch Japan au Uk ningumu kushindana na Makapuni yaliyo sajiliwa Japana kwasabu zifutazo.

Iliweze kupata magari kwa gharama nafuu nilazima uwe member wa Auctions unatakiwa usajili kampuni yako Japan au Uk ili uweze kupata magari moja kwamoja kutoka minadani au kwa watu binafsi na kuuza kwa gharama za ushindani kwenye soko,ukiwa hapa Tanzania ningumu sana kupata fursa ya kupata magari kutoka kwa wamiliki moja kwamoja au kutoka kwenye minada bila kupitia kwa mtu wa kati ambaye ni member wa Auction au anaishi Japan au uk.

Unaponunua gari mtandaoni ningumu kulikagua kwa macho kabla ya kulipia zaidi ya kutumiwa picha, ubara anajua mnunuzi wa ambaye ni member wa Auction,akishanunua Auction anaweka cha juu mtu wapili ukinunua tayari gharama zinaongezeka kwasabu ya mtu wakati hadi kunfikia mtu wamishi gharama zinakua kubwa ukijumlisha na ushuru na gharama zingine za bandarini usajili wa plat number nk.


Watu wananunua magari mtandaoni moja kwamoja bila kupitia kwenye makampuni ya Kitanzania baadhi yao pia wanapata changamoto kwanfano unaagiza gari mtu anakutumia picha mnakubaliana likifika dar unakuta gari Engine inagonga, gari nililelile alokutimia picha kila kitu kiko vilevile utamshitaki waki na gari ni used sio mpya au unatumapesa watu wanalala nazo mbele unabaki unalia mwenye utawatafutia wapi.

Jambo lingine muhimu kwenye maswala ya magari ya used watu wengi wanauelewa ndogo sana kuhusu magari ya mtumba watu wanakariri bei magari ya mtumba yanauzwa kwa grade kulingana na ubora nfano unaweza kuta magari mawili IST yanafanana rangi mwaka cc km kilakitu lakini moja likauzwa dolla 1,000 nalingine likauzwa dolla 2,500 kwenye mnada wa siku moja kutokana na grade ya gari na history yake , ukimuwekea mnunuzi waki Tanzania magari mawili moja linauzwa milion 12 moja linauzwa milion 15 atachagua la milini 12 bila kujua kwamba used zinatofautina ubora matokeo yake wauzaji wanaendana na soko linavyotaka wanatafuta magari ya zero grade ya bei rahisi minadani nakutumia uelewa ndogo wa wanunuzi bila kujali ubora na future ya gari ndio maana wanaficha hizo Auction inspection sheets japokua kuna baadhi ya magari uuzwa mtaani sio kila gari la used ilinauzwa na inspection sheet japokua pia lugha wanayotumia kundika hizo sheets ni kijapan unaweza usielewe kilichoandikwa .

Baada ya kufanya utafiti nakugunduka kuna changamoto nyingi kwenye uagiza wa magari na vitu mbalimbali tukanzisha huduma ya kuunganisha wa uzaji na wanunuzi na sisi kazi yetu kuhakikisha tunalinda masilahi ya pende zote mbili bila kuegemea upande wote kupitia kwenye website yetu www.digxam.com unaweza kuagiza kitu chochote ukaletewa bila changamo kama mleta mada alivyo eleza.
Nia yako ni moja. Kutetea uozo unaosemwa hapa na pia kuwa-discourage watu wanaotaka kuagiza magari wenyewe kutoka Japan. Ni hivi: Mara nyingi ni salama zaidi mtu kuagiza gari mwenyewe kutoka Japan kuliko kutumia hizi kampuni za kibongo. Kama mtu yuko makini siyo rahisi kupigwa fedha kwani website za magari zinazoaminika zinafahamika na wengi ni waaminifu tofauti na wabongo wenye tamaa kama fisi.
 
Sawali lako ni zuri sana naomba nitoe maelezo kidogo kuna njia mbili za uuzaji Magari Japana njia ya kwanza, sellers wananunua magari sehemu mbalimbali na kuweka kwenye stock kisaha wanapiga picha na kupost kwenye website zao hii njia ni mzuri ila gharama zake nikubwa kidogo.

Njia ya pili kuna sellers wanangoja order kutoka kwa wateja wao kisha wanaenda kwenye minada kuwatafutia wateja wao magari kulingana na bajet za wateja wao.

Njia ya kwanza kununua gari la kuweka kwenye store au yard seller anapaswa kuwa na mtaji kubwa wakununua gari na kulisafirisha kutoka alikolinunua hadi kwenye yard yake pia kuna gharama za kukodi yard ulinzi na usafiri wakutoka kwenye Auction kulipeleka yard kisha likipata mteja likanunuliwa litasafirishwa mala ya pili kulipeleka port kwajili ya kulisafiri kuja Dar au Mombasa.Gharama zote zinakuwa include kwenye prices za manunuzi kwaiyo mnunuzi anagharamikia gharama zote hizo sio muuzaji.

Njia ya pili nizuri kwapandezote mbili mnunuzi na muuzaji kivipi ,muuzaji aingii kwenye gharama kubwa kama muuzaji anayetumia njia ya kwanza ,baada ya kununua gari anatumia gharama kidogo sana au anakwepa garama zisizo za lazima, anachokifanya anapanda trani anaenda kwenye minada ya karibu na bandari akimaliza manunuzi analichukua gari anilipeleka bandari bila kutumia magari la kusafirsha magari au car carrier,kwakutimia njia hii seller anapaswa kuwa muwazi kwamteja wake nakumulezea mazingira ya biashara yatakuwaje mapema ili mnunuzi akubalia au akatae,baada ya mnunuzi kukubali muuzaji anatakiwakungalia aina za gari ambayo kapewa orda na mteja wake kwenye minada kisha anamtumia picha za gari zaidi ya moja kutoka kwenye website ya mnada lengo mnunuzi achague angalau magari mawili au tatu katika magari matatu mnunuzi akuwa na nafasi mzuri ya kupata gari moja kwajili ya mteja wake kwa gahara nafuu sana na grade mzuri ukilinganisha njia ya kwanza ambayo muuzaji ananunua gari bilakujua atamuuzia nani nalini ataliza hilo gari.

Kuhusu tofauti ya yetu Digxam Trades na hawa baadhi ya sellers wa hapa Tanzania, sisi tunadili na bidhaa nyingi sana zaidi ya magari pia tuna office Japan na Tanzania kwajili ya kupakia mizigo mablimbali ambayo tayari imenunuliwa hivyo basi majukumu yetu ni matatu

1.kuungamisha mnunuzi na muuzaji
2.Kulinda masirahi ya muuzaji na mnunuzi
3.Kuasafirisha mizigo midogo kwanjia ya container

Ukiingia kwenye website yetu unapaswa kupost kitu unachikita unatoa maelezo kiwe na sifa gani kisha utajibiwa na wauzaji kutoka sehemu mbalimbalia kulinga na jukwaa kama ni jukwaa la Japana utajibiwa na wauzaji wa Japana kama ni Kariakoo utajibiwa na wauzaji wa kariakoo...,mazungumzo yenu au makubaliano yetu kati ya muuzaji na mnunuzi yanatakiwa kuwa wazi, ili ikitokea tatizo Admin ajue pakuanzia ushahidi wote utakuwa wazi,mkisha kubaliana unalipia pesa kwenye account yetu ya Kampuni ya Digxam Trades kupitia kwenye menu ya simu yako ya kiganjani au bank,baada ya mzigo kununuliwa mnunuzi ata confirm kwamba kila kitu kikosawa kisha sisi Digxam Trades tunamlipa muuzaji,kama ni mzigo ndogo wauzaji wanalipwa baada ya mzigo kufika officen kwetu Japana au kwingine kama ni gari muzaji analipwa baada ya kutuma BL officen kwetu,kila jukwaa linakanunuzi zake kulingana mazigira ya sehemu .
Maelezo meeengi yasiyo na maana yoyote kwa mnunuzi. What a f#ck mnunuzi atake kujua milolongo yote hiyo wakati yeye anataka gari. Mimi nachojua kama mnunuzi ni kunagalia specifications za gari husika na bei yake, kama naridhika basi na-place order yangu.
 
Nimepitia leo web yenu. Jana nilichanganywa na zile ads zinakuja kabla ya contents.

Pia naona forums nyingi hazijawa updated for more than a month.

Also majukwaa yamejificha sana mpaka uscroll kwenda chini ndio utaona forums mbalimbali.

Pia sijaelewa kwenye auction kuna kuweka 30,000 na ile 50,000 ina maana bid ikichukuliwa na mwingine hela inakuwa refunded?

Pia jitahidi iwe user friend kuaccess majukwaa like hapa JF ni easy majukwaa yapo juu tu ukitaka kuingia....

View attachment 2162445
Hivi huyu jamaa ameweza kuku-twist mpaka ukalainika? Unaona kweli hiyo link aliyoweka ni forum yenye hadhi ya kuaminika? Angalia usije kulizwa hapa. Tumieni website zinazoaminika ambazo umepewa link, hizo za Befoward na hiyo nyingine.
 
Hapo nyuma, nilishawishika kununua gari kupitia kwa wakala wa hapa Nyumbani.

Niliona Picha ya gari kupitia ukurasa wa Instagram, baada ya kuhoji gari la mwaka gani na limetembea Km ngapi, nilichojibiwa hakikuwa na uhalisia wowote.

Kwabahati nilipata website moja ya wauza magari kutoka Japan, Nikabahatika kukuta gari nililolihitaji kupitia kwa wakala yule wa hapa nchini, nakukuta taarifa alizonipa hazikuwa sahihi bali kuna mchezo alitaka kuucheza ili aje anihadae hapo baadae. Nilifanya maamuzi wa kutafuta gari lingine lenye vigezo ninalolihitaji na kulipia haraka.

Niliweza kupata gari zuri kwa gharama nafuu na kuepuka gharama kama ya T-sh 3m kama ningeamua kununua kupitia yule wakala.
 
Maelezo meeengi yasiyo na maana yoyote kwa mnunuzi. What a f#ck mnunuzi atake kujua milolongo yote hiyo wakati yeye anataka gari. Mimi nachojua kama mnunuzi ni kunagalia specifications za gari husika na bei yake, kama naridhika basi na-place order yangu.

Ukisikia mtu anajieleza kwa nguvu tuna ofisi japan na bongo au china na Tanzania kaa kijanja
 
Hivi huyu jamaa ameweza kuku-twist mpaka ukalainika? Unaona kweli hiyo link aliyoweka ni forum yenye hadhi ya kuaminika? Angalia usije kulizwa hapa. Tumieni website zinazoaminika ambazo umepewa link, hizo za Befoward na hiyo nyingine.
Kaka,
Jamaa hajanitwist niliona ameweka web yake nami nikapitia ni kama middle man. Uzi wangu haujasema wote ni matapeli ila nimetoa tahadhari maana watu wengi wanalizwa mno.
Mimi nishakutana nao sana na siwezi kuagizia gari kupitia middle man kabsa na sishauri mtu aagize gari kupitia hawa watu....

Though kuna wengine ni waaminifu ila ni nadra sana....
 
Back
Top Bottom