Huyu aliyeelekeza magari ya serikali kupaki saa kumi na mbili ana maana gani?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
914
4,262
Leo imetolewa hoja kwamba magari ya serikali yapaki saa kumi na mbili. Unajiuliza hawa watu wanapotoa haya matamko wanashindwaga nini kufanya tathimini?

Nchi hii inawaza kuendesha shughuli zake masaa ishirini na nne; Mama anawaza kuona soko la Kariakoo linafanya kazi masaa ishirini na nne kuendana na ratiba ya vyombo vya usafiri.

Tunaelewa kwamba kadri muda wakutoa huduma unavyoongezeka ndivyo serikali inapanua muda wa usimamizi. Leo walevi kipaki magari bar imekuwa ni agenda inayopelekea mteule wa Rais kusema magari yapaki saa kumi na mbili?

Huyu Mbunge aliyetoa hoja alishindwa kupiga picha gari husika akamtumia waziri Dreva au bosi akawajibishwa tukasonga mbele?

Mimi naamini kila gari linasimamiwa na Kiongoz aliyepewa dhamana na serikali. Likitumika vibaya kiongozi anapaswa kushughulikiwa lakini siyo waovu wachache warudishe juhudi za serikali kutoa huduma saa ishirini na nne.

Mnapotoa matamko na makatazo someni sera ya nchi kwanza. Mimi ningesema tumelipokea na tutalifanyia kazi then you go back to the office and communicate.

Ulaya nidhamu imejengwa kwenye uwajibishaji wa watovu wa nidhamu. Tuangaike na tatizo na siyo kufanya vitu jumla.

Mwisho, najiuliza hao watakaotembea usiku na gari za serikali watakamatwa na polisi na kuzuiwa?
 
Kuna mdau alishauri magari yote ya Serikali yawekwe alama kuonyesha taasisi husika. Nakubaliana na wazo la mdau maana kuna baadhi ya taasisi za Serikali inaonyesha zina usimamizi mbovu sana wa magari yake. Unakuta gari imepaki bar usiku dereva na wapambe wake wanapiga vilevi tu.
 
Atakuwa na matatizo ya akili huyo, yeye mwenyewe la kwake hapaki saa 12. Au magari yanayobeba hao wanaitwa viongozi sio ya serikali??
 
Badala apambane na walevi anajibu hoja bungeni kama vile anashauri familia

Leo hii mahoteli mengi makubwa yanauza chakula na vinywaji. Kwamba Dreva akipaki apate chakula mfano pale kabla ya chalinze anakuwa analewa?

Hawa mawaziri wanatakiwa wakae pembeni tu. Kibali kinaombwa kwa nani? Hakuna mtu mdogo anayetembelea hayo magari na kipaki bar, hao ndiyo wenye mifumo wenyewe acheni kutilaghai.

Gari ulipaki hapa city Mall beyond saa kumi na mbili iwe kosa ? Kwa sheria gani?

Na vyombo vya habari vinaandika tu bila kuibua maswali; angekuwa nchi zinazokimbia kiuchumi alipomaliza bunge akatoka nje angekuta vyombo vya habari utitiri vinamsubiri ajibu hoja.

Tanzania vyombo vya habari vimebaki kuripoti, bunge nalo linashindwa kuuliza swali la nyongeza .......twafaaaa acha tupewe tu
 
Leo imetolewa hoja kwamba magari ya serikali yapaki saa kumi na mbili. Unajiuliza hawa watu wanapotoa haya matamko wanashindwaga nini kufanya tathimini?
gari za serikali watakamatwa na polisi na kuzuiwa?
Nyie watoto mliomaliza kunywa maziwa ya mama majuzi tu, hamjui kuwa kupaki magari saa 12, ni kanuni ya matumizi wa hayo magari toka enzi ya mkoloni.
 
Hivi kama jiji la dar ,mpaka gari limpeleke boss tegeta jioni na dereva kuja kulipaki Gongo la mboto anapoishi si saa tano usiku, na bado aamke saa kumi usiku.tuache uroboti wa sheria za zamani wakati Mama kafungua nchi masaa 24, hizo ni sheria enzi za nyerere.

Au boss asitoe huduma baada ya kazi akiwaza gari lake linatakiwa likapaki.😂😂huku tunasema wananchi wahudumiwe usiku na mchana huku gari zote za serikali zipaki saa 12 jioni. Futuhi.kila wizara na idara ina ma transport officers wawajibike kufuatiia matumizi ya magari ya umma yatumike kwa shughuli kusudiwa, kama kuna dereva mtovu awajibishwe siyo kutoa tamko la jumla
 
Huku wilayani kuna vijiji umbali KM 110 kutoka Wilayani njia za vumbi, tukienda tunahakikisha tumepitia vijiji kadhaa ili kuokoa mafuta na kurudirudi, vijiji vingine tunaondoka mpaka saa mbili usiku na tunafika wilayani saa nne usiku kuendelea....sasa hapo vijana wasio nawake itakuwaje wasipopita kula???
Hii itakuwa usumbufu sana na huku WILAYANI haitekelezeki
 
Nadhani Serikali ipige marufuku kupaki/kuegesha magari ya UMMA kwenye bar badala ya kuegesha . magari yote 12.30 jioni.Kupaki/kuegesha magari ya UMMA kwenye bar inaleta taswira mbaya kwa jamii na hawa madereva wanaotumia kilevi huwa wanasabisha ajali na kufanya rasilimali za UMMA kuhaaribika kwa uzembe badala ya bahati mbaya
 
Paki gari la serikali nenda na lako au bajaj au boda ukamwagilie moyo na kuchepuka,
Sio kuzurula na magari ya serikali mda ukiisha.
Vilaza sijui wapi huwa hamuelewi.
Sibebi kifaa chochote baada ya kazi.
 
Nawaona polisi na jeshi la ulinzi la wananchi wanazurura sahivi huku Morogoro

Kwani haya ni magari ya shirika la alizeti?
Yale Ya Bungeni Hayatekelezeki
Tazama Dar Es Salaam Bado Gari Za Serikali Zinapita Tu Njia Ya Mwendokasi
 
Back
Top Bottom