Jihadhari na makampuni ya Kitanzania yanayoagiza magari

Tupe jina la kampuni inayoaminika na iliyoshika soko kuzidi kampuni tajwa hapo Juu,Hizo kampuni ni nadra kusikia malalamiko toka kwa wateja wao,hawana uhuni unaolalamikiwa na mtoa Mada,wana kasoro baadhi lakini ni zakuongeleka na za kurekebishika, Sio za kitapeli na Wizi (hawana)

Labda tutajie kampuni unayoifahamu yenye hadhi na heshima ambayo watanzania hatuijui,tusaidie.
  1. Real Motor Japan
  2. Global Partner
  3. Car junction
  4. Makampuni yako mengi sana wameuza magari kitambo sana hata kabla baadhi ya watu kuzaliwa hapa JF,fatilia makampuni yote ambayo yako chini ya Trade car view wanauza magari mazuri kwa bei mzuri kwa muda mrefu, hata makampuni tajwa walianzia Trade Car View kukariri kampuni au tekinolojia kwenye karne hii eti kwasabu ya matapeli sidhani kama inweza kumsaidia mtu bali nikuyaondolea ushindani makampuny tajwa .
  5. Kama unashida na gari unatakiwa kulinganishe bei na ubora wa gari kutoka kwenye makampuni mbalimbali mimi siko hapa kupotosha mtu yoyote au kulazimisha mtu kuagiza gari kupitia kwenye kampuny yetu tayari tunawateje wetu kitamba ambao tunafanya nao kazi pia tuna deal na vitu vingi zaidi ya magari nilichangia hii mada baada yakuikuta kama mtu mwingine na siungi mkono utapeli kama baadhi ya watu walivyo nishtumu .
 
Nimepitia leo web yenu. Jana nilichanganywa na zile ads zinakuja kabla ya contents.

Pia naona forums nyingi hazijawa updated for more than a month.

Also majukwaa yamejificha sana mpaka uscroll kwenda chini ndio utaona forums mbalimbali.

Pia sijaelewa kwenye auction kuna kuweka 30,000 na ile 50,000 ina maana bid ikichukuliwa na mwingine hela inakuwa refunded?

Pia jitahidi iwe user friend kuaccess majukwaa like hapa JF ni easy majukwaa yapo juu tu ukitaka kuingia....

View attachment 2162445
1.Ads zinakuja kabla ya contents jibu nikweli uwezi kuzificha kisha ukaziita ADs sema nini uki login ADs zote zinakua invisible iliku kupisha content.

2.Pia naona forums nyingi hazijawa updated for more than a month. jibu Forums kawaida zinakuwa solved au unsolved ningumu kuifanyia update

3.Also majukwaa yamejificha sana mpaka uscroll kwenda chini ndio utaona forums mbalimbali. Ukitaka ulinganishaBusiness forums na JF ni sawa na kukariri tekinoloji kila website au Forums ina features zake kulingana na matumizi.

4.Pia sijaelewa kwenye auction kuna kuweka 30,000 na ile 50,000 ina maana bid ikichukuliwa na mwingine hela inakuwa refunded? Auction ina refund kila mtu aki bid kuna option kulingana na muuzaji kaseti nfumo gani utumike.

5.Pia jitahidi iwe user friend kuaccess majukwaa like hapa JF ni easy majukwaa yapo juu tu ukitaka kuingia Hapa sijakulewa unamaana gani.

kwakifupi ni hivi mtu yeyote anweza kuweka bidhaa zake kwenye website yetu akiwa popote Dunia na kafanya biashara na kupokea pesa nfumo wetu unakutanisha watu watatu ili biashara ikamilike.
1.Sellers
2.Buyers
3.Admins
 
Nia yako ni moja. Kutetea uozo unaosemwa hapa na pia kuwa-discourage watu wanaotaka kuagiza magari wenyewe kutoka Japan. Ni hivi: Mara nyingi ni salama zaidi mtu kuagiza gari mwenyewe kutoka Japan kuliko kutumia hizi kampuni za kibongo. Kama mtu yuko makini siyo rahisi kupigwa fedha kwani website za magari zinazoaminika zinafahamika na wengi ni waaminifu tofauti na wabongo wenye tamaa kama fisi.
Mkuu naomba usome vizuri kisha uniambia wapi nime discourage wanaotaka kuagiza magari?
 
Hivi huyu jamaa ameweza kuku-twist mpaka ukalainika? Unaona kweli hiyo link aliyoweka ni forum yenye hadhi ya kuaminika? Angalia usije kulizwa hapa. Tumieni website zinazoaminika ambazo umepewa link, hizo za Befoward na hiyo nyingine.
Mkuu unaonekana ni member muda hapa jf jifunze kusoma na kuelewa kabla ya ku comment, baadhi ya watu hapa jf wana comment kwanza kisha wanasoma thread huu sio utamaduni mzuri.
 
Tupe jina la kampuni inayoaminika na iliyoshika soko kuzidi kampuni tajwa hapo Juu,Hizo kampuni ni nadra kusikia malalamiko toka kwa wateja wao,hawana uhuni unaolalamikiwa na mtoa Mada,wana kasoro baadhi lakini ni zakuongeleka na za kurekebishika, Sio za kitapeli na Wizi (hawana)

Labda tutajie kampuni unayoifahamu yenye hadhi na heshima ambayo watanzania hatuijui,tusaidie
1.Hizo changamoto na kasoro ulizozisema hapo juu ingekua vizuri ukazitaja ili baadhi ya watu wazijue kabla ya kuagiza magari kupitia kwenye makampun tajwa.
2. Kutapeliwa sio kuibiwa pesa zako tu hata kuuziwa gari ambalo liko chini ya viwango bila kuambiwa ukweli baadhi wanauziwa kwa bei kubwa sana pia ni utapeli.
3.Kuagiza gari sio kutoa pesa za manunuzi ya gari unaweza kuja offisi kwetu ukasema unataka gari aina gani ukaagiziwa gari lako likafika bila kutoa pesa ukalipia baada ya kuliona pia nikuagiza gari.
4.Utapeli upo kila sehemu sio Tanzania tu ukitapeliwa unatakiwa kutaja jina la Kampun ambayo imekufanyia utapeli badala ya kuogea jumla jumla kisha ukatataja makampuni mawili tu ukasema hawa sio matapeli makampuni mengine yote yaliyobaki ni matapeli hii pia nayo sio sawa.
 
unashindwaje jisajili tradecarview , be foward au sbt ukaagiza gari mwenyewe?
hao jamaa.janja janja sana bora uende showroom ukachague mwenyewe kama huwezi agiza
 
unashindwaje jisajili tradecarview , be foward au sbt ukaagiza gari mwenyewe?
hao jamaa.janja janja sana bora uende showroom ukachague mwenyewe kama huwezi agiza
Mkuu ungesoma kwanza mada ukailewa kabla ya kuchangia nani kasema anataka kuagiza gari?

Habari wa JF,

Katika pita pita zangu mitandaoni hasa JF na instagram nimeona kuna kampuni/watu wanaofanya huduma za kuagiza magari nje kwa masharti ya kulipia nusu na kumalizia kiasi kilichobaki baada ya gari kufika. Mengi ya makampuni hayo (Sisemi wote) ni "MATAPELI WAKUBWA SANA" na huu ni mchezo ambao huwafanyia wateja wao.
 
1. Huwa wanapost gari kwenye mitandao either wameliona kwenye site za magari au wana picha zake.

2. Baada ya kupost wateja wataliulizia na wanakuambia lipo.

3. Then watakufikisha kwenye ofisi zao nyingi zipo posta na maeneo ya mwenge- sinza- mlimani city.

4. Mtaingia mkataba na wewe kufanyia malipo gari hilo nusu. Hapa mnaweza kuwa hata wateja wanne mnafanyia malipo gari moja.

Baada ya malipo ndio mchezo unaanza.

Kwanza hawatakuonyesha chasis number ya gari na pia watakutajia km chache mno lets say between 40,000-70,000 ila kamwe hawatakupa picha ya odometer.

Baada ya hapo jamaa huwa wanaingia mzigoni kuanza kutafuta gari inayofanana na ile uliyoagiza may be kwa rangi.

Wakiipata huko japan kwa bei rahisi watakuuagizia ila zile zilizopata ajali na kufanyiwa modification. Au wakiukosa wanakutafutia hapa bongo gari kama ile na kule japan/nje wanakuagizia chasis number tu na vile vibati vya chasis number kwenye mlango then vikifika bongo wanakubandikia kwenye gari then wanakuambia gari imefika. Kumbe badala ya kuagiziwa gari umeagiziwa chasis number then gari inabandikwa na kufanyiwa usajili upya.

Kampuni hizi mara nyingi zinakua na blaah blaah ukiwauliza maswali na magari yao mara nyingi yanachelewa sana. Ili ku buy time ya kufanya manuva yao.

Unaponunuua gari mtandaoni hakikisha kabla ya kulipia unafanya yafuatayo.

1. Pata picha ya gari lote mpaka odometer.
2. Pata chasis number ya gari (Hii itakusaida kujua hilo gari lipo au laah).
3. Omba auction report/sheet. Check picha hapo chini... Wauzaji wajanja wajanja hawakupi hii hata iwaje....

USIFANYE MALIPO KAMA HUJAPEWA HIVYO VITU LA SIVYO UTAUZIWA PICHA YA GARI BADALA YA GARI.....

Kesi za namna hii zipo sana central police na washawachoka hawa watu ila bado watu wanaendelea kupigwa sana.....

Chukua tahadhari.

Siku njema.

Ok
Screenshot_20220409-134824_Google.jpg
 
Unachokizungumza kina ukweli kwa asilimia fula iko hivi kampuni za kuagiza magari kutokea nchi yoyote bila kuwa na branch Japan au Uk ningumu kushindana na Makapuni yaliyo sajiliwa Japana kwasabu zifutazo.

Iliweze kupata magari kwa gharama nafuu nilazima uwe member wa Auctions unatakiwa usajili kampuni yako Japan au Uk ili uweze kupata magari moja kwamoja kutoka minadani au kwa watu binafsi na kuuza kwa gharama za ushindani kwenye soko,ukiwa hapa Tanzania ningumu sana kupata fursa ya kupata magari kutoka kwa wamiliki moja kwamoja au kutoka kwenye minada bila kupitia kwa mtu wa kati ambaye ni member wa Auction au anaishi Japan au uk.

Unaponunua gari mtandaoni ningumu kulikagua kwa macho kabla ya kulipia zaidi ya kutumiwa picha, ubara anajua mnunuzi wa ambaye ni member wa Auction,akishanunua Auction anaweka cha juu mtu wapili ukinunua tayari gharama zinaongezeka kwasabu ya mtu wakati hadi kunfikia mtu wamishi gharama zinakua kubwa ukijumlisha na ushuru na gharama zingine za bandarini usajili wa plat number nk.

Watu wananunua magari mtandaoni moja kwamoja bila kupitia kwenye makampuni ya Kitanzania baadhi yao pia wanapata changamoto kwanfano unaagiza gari mtu anakutumia picha mnakubaliana likifika dar unakuta gari Engine inagonga, gari nililelile alokutimia picha kila kitu kiko vilevile utamshitaki waki na gari ni used sio mpya au unatumapesa watu wanalala nazo mbele unabaki unalia mwenye utawatafutia wapi.

Jambo lingine muhimu kwenye maswala ya magari ya used watu wengi wanauelewa ndogo sana kuhusu magari ya mtumba watu wanakariri bei magari ya mtumba yanauzwa kwa grade kulingana na ubora nfano unaweza kuta magari mawili IST yanafanana rangi mwaka cc km kilakitu lakini moja likauzwa dolla 1,000 nalingine likauzwa dolla 2,500 kwenye mnada wa siku moja kutokana na grade ya gari na history yake , ukimuwekea mnunuzi waki Tanzania magari mawili moja linauzwa milion 12 moja linauzwa milion 15 atachagua la milini 12 bila kujua kwamba used zinatofautina ubora matokeo yake wauzaji wanaendana na soko linavyotaka wanatafuta magari ya zero grade ya bei rahisi minadani nakutumia uelewa ndogo wa wanunuzi bila kujali ubora na future ya gari ndio maana wanaficha hizo Auction inspection sheets japokua kuna baadhi ya magari uuzwa mtaani sio kila gari la used ilinauzwa na inspection sheet japokua pia lugha wanayotumia kundika hizo sheets ni kijapan unaweza usielewe kilichoandikwa .

Baada ya kufanya utafiti nakugunduka kuna changamoto nyingi kwenye uagiza wa magari na vitu mbalimbali tukanzisha huduma ya kuunganisha wa uzaji na wanunuzi na sisi kazi yetu kuhakikisha tunalinda masilahi ya pende zote mbili bila kuegemea upande wote kupitia kwenye website yetu www.digxam.com unaweza kuagiza kitu chochote ukaletewa bila changamo kama mleta mada alivyo eleza.
Mkuu umechambua vizuri sana tatizo uelewa wa mswahili zero umepoteza muda wako mswahili hataki kujifunza kitu kipya ndio maana wanatapeliwa SBT na Beforward ni makampuni ya Wahindi na wapakistani sio Wajapan ndio maana wanauza magari mabovu miezi mitatu gari chalii alafu mswahili anajiona mjanja sana mjuaji wa kila kitu Mjapan ni mkweli gari kama ni zero Grade anakueleza ukikubali utalipia pesa kidogo.
 
Kwani hizi kampuni za wabongo wao ndio hawauzi magari mabovu?. Ndio ambazo zinazungumziwa hapa

Je hawa watanzania sio waswahili wajanja na wajuaji wa kila kitu, wanaocheza hadi na kilometres za magari?
 
Hapa sijaona kampuni yoyote ya wabongo zaidi ya porojo makampuni yote Dunia yana majina sijaona jina hata moja la kampuni inayoshutimiwa kufanya utapeli, mleta mada ametumwa na Be forward na SBT kuchafua makampun ya wazawa kwaujila kidogo nanyie mnaingia kwenye mtego na kukandamiza nduguzenu kwatuhumu za uongo nakushangili wahindi wakichukua fursa zenu mswahili acha ujinga amka kwenye usingizi wa pono mleta mada kama kweli anachokiongea ataje jina la kampuni na watu wote waliotepiliwa kwa namna moja au nyingi waweke ushahidi wasije porojo na kuchafuliana hii ni tabia mbaya sana watu wanalipa kodi wanaajiri watu mtu moja naishi kwa shemeji yake anakuja nakufungua uzi wakuchafua makampuni bila ushahidi.
 
Wee nae mshamba tuu ujui lolote odometer unaweza kupunguza ikasoma hta 0
Nani ajui lolote? Mambo ya odometer yote ni yakukoteza tu lengo nikuchafua watu fulani ili watu fulani wafanye kazi ukiombwa ushahidi makampuni ya wazawa wakishu hizo km utweza kuuleta hapa je hawa Be forward na SBT unaukikagani kama awashushi hizo km?
 
Hapa sijaona kampuni yoyote ya wabongo zaidi ya porojo makampuni yote Dunia yana majina sijaona jina hata moja la kampuni inayoshutimiwa kufanya utapeli, mleta mada ametumwa na Be forward na SBT kuchafua makampun ya wazawa kwaujila kidogo nanyie mnaingia kwenye mtego na kukandamiza nduguzenu kwatuhumu za uongo nakushangili wahindi wakichukua fursa zenu mswahili acha ujinga amka kwenye usingizi wa pono mleta mada kama kweli anachokiongea ataje jina la kampuni na watu wote waliotepiliwa kwa namna moja au nyingi waweke ushahidi wasije porojo na kuchafuliana hii ni tabia mbaya sana watu wanalipa kodi wanaajiri watu mtu moja naishi kwa shemeji yake anakuja nakufungua uzi wakuchafua makampuni bila ushahidi.

Kampuni za bongo ni janja janja.
 
Back
Top Bottom