Jihadhari na makampuni ya Kitanzania yanayoagiza magari

Wewe umesema kiini cha tatizo hasa. Watanzania tuna akilifupi mno mno. Biashara karibu zote zimejaa ''ujanja ujanja'' na maneno mengi. Yaani mfanyabiashara haoni madhara ya kutokuwa mwaminifu hata kidogo. Ni tamaa mbele kwa mbele. Nadhani ni culture tuliyojenga kwa sababu ya uadimu wa bidhaa kipindi cha ujamaa. Muuzaji anakuwa ndiye mfalme na mnunuzi anakuwa kama mtumwa. Huwa nasema ombeni sana wachina wasije kuruhusiwa kufanya hizi biashara ndogo ndogo maana wabongo wote wenye biashara watakufa njaa.
Hahahaa, wakenya wanalia kila siku baada ya wachina kuingia mtaa kuuza bidhaa. Kuna chimbo lao moja linaitwa China supermarket.
 
Back
Top Bottom