Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,504
- 9,283
Ni vyema ukawa na kawaida ya kuhifadhi vyakula vya aina mbalimbali nyumbani kwako ili ikusaidie pale unapotaka kupika. Haipendezi kila unapotaka kupika basi unaenda dukani au gengeni kununua kitu hicho. Kama una kipato cha uhakika kila mwezi ni vyema ukawa na hifadhi ya mwezi kwa vile visivyoharibika na ya wiki mbili na wiki wiki kwa vile vinavyoweza kuharibika upesi.
Hifadhi ya mwezi inaweza kuwa na vitu kama:
- Mchele
- Sukari
- Unga wa Sembe
- Unga wa Ngano
- Maharage
- Choroko
- Mafuta ya Kupikia
- Chumvi
- Majani ya chai
- Masala mbalimbali (samaki, pilau, kuku n.k.)
- Nyanya za kopo
- Tambi (Spaghetti)
- Baking Powder
- Hamira
- Blueband, Jam, Mayonnise n.k
- n.k
- Njegere
- Mayai
- Vitunguu saum
- Tangawizi
- Vitunguu maji
- n.k
- Nyanya
- Viazi
- Karoti
- Pilipili hoho
- Maziwa kama una freezer
- Nyama ya ng’ombe, mbuzi, kuku n.k
- Sausages
- Samaki
- n.k
Ha hivi pia ni vyema ukawanavyo ingawa sio vyakula, lakini inategemea na bajeti yako na uwezo wako.
- Sabuni za kuoshea vyombo
- Alluminium foil
- Sponji za kuoshea vyombo
- Toothpicks
- Napkins
- n.k
women of christ