Hifadhi nzuri ya Vyakula kutokana na muda wake ili visiharibike

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281

Ni vyema ukawa na kawaida ya kuhifadhi vyakula vya aina mbalimbali nyumbani kwako ili ikusaidie pale unapotaka kupika. Haipendezi kila unapotaka kupika basi unaenda dukani au gengeni kununua kitu hicho. Kama una kipato cha uhakika kila mwezi ni vyema ukawa na hifadhi ya mwezi kwa vile visivyoharibika na ya wiki mbili na wiki wiki kwa vile vinavyoweza kuharibika upesi.

Hifadhi ya mwezi inaweza kuwa na vitu kama:
  • Mchele
  • Sukari
  • Unga wa Sembe
  • Unga wa Ngano
  • Maharage
  • Choroko
  • Mafuta ya Kupikia
  • Chumvi
  • Majani ya chai
  • Masala mbalimbali (samaki, pilau, kuku n.k.)
  • Nyanya za kopo
  • Tambi (Spaghetti)
  • Baking Powder
  • Hamira
  • Blueband, Jam, Mayonnise n.k
  • n.k
Hifadhi ya wiki mbili ni kama:
  • Njegere
  • Mayai
  • Vitunguu saum
  • Tangawizi
  • Vitunguu maji
  • n.k
Na sababu vingine huharibika mapema, unaweza kuwa unanunua kwa wiki wiki, mfano:
  • Nyanya
  • Viazi
  • Karoti
  • Pilipili hoho
  • Maziwa kama una freezer
  • Nyama ya ng’ombe, mbuzi, kuku n.k
  • Sausages
  • Samaki
  • n.k
Mboga za majani na matunda hivyo unanunua pale unapohitaji au kwa hifadhi ya siku 2-3 maana huharibika au kupoteza ladha upesi hata kama vikiwekwa kwenye friji.

Ha hivi pia ni vyema ukawanavyo ingawa sio vyakula, lakini inategemea na bajeti yako na uwezo wako.
  • Sabuni za kuoshea vyombo
  • Alluminium foil
  • Sponji za kuoshea vyombo
  • Toothpicks
  • Napkins
  • n.k

women of christ
 
Hebu nisaidie jinsi us kuhifadhi njegere na nyanya, nyanya hazimalizi wiki zinaharibika. njegere nikiweka kwenye friji maybe siku mbili nakuta zimeanza kuota
 
Hebu nisaidie jinsi us kuhifadhi njegere na nyanya, nyanya hazimalizi wiki zinaharibika. njegere nikiweka kwenye friji maybe siku mbili nakuta zimeanza kuota
Njegere unatakiwa uzichemshe kwanza hata zisipowiva kbsa zikuwe na kaugum gumu kisha unaziweka kwa friza,zinadumu hadi mwezi mzima,nyanya nayo unaweza inbrend nyingi upendavyo ukaistore kwa friza pia
 
  • Thanks
Reactions: ram
Njegere unatakiwa uzichemshe kwanza hata zisipowiva kbsa zikuwe na kaugum gumu kisha unaziweka kwa friza,zinadumu hadi mwezi mzima,nyanya nayo unaweza inbrend nyingi upendavyo ukaistore kwa friza pia
Nyanya ukiisaga achilia mbali kufreeze lazima mchuzi upate taabu sana. Sishauri!
 
Hebu nisaidie jinsi us kuhifadhi njegere na nyanya, nyanya hazimalizi wiki zinaharibika. njegere nikiweka kwenye friji maybe siku mbili nakuta zimeanza kuota
Njegere zifreeze zikiwa mbichi. Nyanya nunua za wiki tu ili kupata ladha bora, usizifreeze.
 
Back
Top Bottom