SoC02 Njia za asili kuhifadhi vyakula kuokoa pesa na muda

Stories of Change - 2022 Competition

Asantesanasana

New Member
Aug 29, 2022
3
2
Kuna njia mbalimbali za kuhifadhi vyakula ili visiharibike mapema vitufae kwa misimu mingine ambayo vyakula vinakuwa adimu sokoni na bei kuwa ghali au kutopatikana na pia kuokoa matumizi makubwa ya fedha na muda.

Mimi nitazungumzia njia za asili ambayo hazihitaji gharama na hata mtu wa chini kiuchumi anaweza kufanya hili na pia haihitaji elimu mtu kuelewa njia hizi ni njia za kawaida sana na inaweza kufanyika mazingira yoyote .

Unaweza kuhifadhi mboga za aina mbalimbali kwa kuzichemsha kidogo na kuzianika juani ,na kuhifadhi sehemu safi na salama zikakufaa baadaye.

Unaweza kuhifadhi viungo mbalimbali kama nyanya ,vitunguu,Limau, tangawizi, pilipili na Rosemary kwa kutumia jua tu maana kuna muda nyanya na vitunguu huuzwa kuanzia shilingi Mia mbili na kuendelea.

Unaweza kuhifadhi uyoga na viazi vitamu kwa kutumia jua .Unaweza kuchemsha mahindi mabichi toka shambani na ukayaanika, yakatumika baadaye kwa kupika na yakawa na radha na muonekano kama yale mabichi.

Naamini njia hizi zitasaidia watu kujipunguzia gharama za maisha na pia kuokoa muda.

Asanteni.

Namba yangu ya simu ni 0710425986
 
Back
Top Bottom