SoC03 Njia duni za utunzaji wa fedha ndio chanzo cha umaskini kwenye jamii zetu. Tuziepuke!

Stories of Change - 2023 Competition

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
755
1,356
Habari,

Watanzania wengi ni watu wenye vipato vyenye kukidhi mahitaji madogo madogo ya kila siku. Kwa kuzingatia hilo kumekuwa na harakati mbalimbali za kupambana na hali duni za maisha kwaajili ya kutafuta kipato cha uhakika kitakacho wafanya waishi maisha mazuri. Zifuatazo ni njia duni zinazotumika sasa.

1. UPATU, hii ni njia mojawapo ambayo ni duni na imepitwa na wakati. Watu wanachanga hela kwa kupeana kwa zamu. Hii inasababisha hela ya mtu kutokupata faida yoyote pia kumekuwa na hali ya kudhulumia na ugomvi usioisha kila siku.

2.VIKOBA, hii nayo ni njia duni ya utunzaji wa fedha kwa kukusanya fedha kwa mda flani Ili kusaidiana kwenye matatizo mbalimbali kwenye jamii. Hela inakusanywa na kuhifadhiwa bila faida yoyote na kwa mpango usio na uwazi na uwajibikaji pindi kiongozi anapofanya ubadhirifu.

3.KIBUBU, hii nayo ni njia mojawapo ambayo ni duni na imepitwa na wakati. Kuweka pesa kwenye vibobo vya mbao au chuma. Hela haijizalishi pia kuna athari ya kuibiwa.

4. AKAUNTI YA KAWAIDA YA BENKI, hii ni njia inayotumiwa na watu wengi wakiwemo waajiriwa, wajasiriamali na wafanyabiashara. Akaunti hizi za benki zinatoa asilimia 2 tu kwa Mwaka kwa pesa unayoiweka huku zikiambatana na makato mbalimbali kwa mwezi na kwa Mwaka .

5. KUFUKIA CHINI YA ARDHI, hii inafanyika zaidi maeneo ya vijijini, hela inakaa chini ya ardhi haitengenezi faida yoyote.

Zifuatazo ni baadhi ya njia sahihi za utunzaji wa hela kidogo kidogo wenye mrengo wa kutengeza faida nzuri;

1. KUHIFADHI FEDHA KWENYE MIFUKO YA PAMOJA, hii ni moja wapo ya njia sahihi ya kuhifadhi pesa ikiambatana na faida kubwa jumuishi kwani fedha hizo huwekezwa kwenye sehemu zenye kutengeneza zenye kutoa faida kubwa. Mfano UTT AMIS na WATUMISHI FUND n.k

2. AKAUNTI ZA MUDA MAALUMU ZA BENKI, hii ni njia sahihi yenye kutengeza faida ikiambatana uthubutu wa kipindi cha muda maalumu mfano, wavuvi akaunti, wajasiriamali ankaunti, fixed akaunti n.k

3.HISA, ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Unanunua hiza zako kwa kampuni yenye kufanya vizuri. Unapata faida ya kuongezeka kwa mtaji na gawio kama kampuni itafanya vizuri. Kumbuka hisa zinaweza kupanda na kushuka kikubwa ni muda. Kiwango cha chini cha hisa ni hisa 100.

4.KILIMO NA UFUGAJI, hii ni njia moja wapo yenye kutengeza faida, badala ya kufukia pesa unaweza kufanya kilimo na ufugaji wenye tija hivyo kujiongezea kipato.

5. BONDI ZA SERIKALI, njia sahihi ya utunzaji wa pesa wenye kuleta faida. Unaikopesha kwa kipindi flani mfano Mwaka moja, miwili, mitatu na kadhalika. Miaka mingi pia hutengeneza faida kubwa.

USHAURI;
Serikali na mamlaka husika zitoe elimu ya kutosha kwa wanainchi Ili kufanya uwekezaji wenye faida.

NB; USISAHAU KUBONJEZA KITUFE CHA KIJANI KWENYE NENO VOTE.

Asante sana!
 
Punguza kulalamika jukwaa la stories of change halitembelewi na members wengi wa JF
Post mzuri na elimishi lakini haitapata wachangiaji maana haihusu mapenzi wala yanga na simba au umbea wa mjini.
 
Punguza kulalamika jukwaa la stories of change halitembelewi na members wengi wa JF
Hii inchi ina safari ndefu kama kulalamiko ndo huko? Ungesema jukwaa gani linatembelewa kwa wingi na kwa nini? Na kwa nini jingine alitembelewi ungekuwa umeongeza tija. Otherwise zero.
 
rolla punguza povu. Umejiunga 2013 nimejiunga 2016 wewe ni mwenyeji humu zaidi yangu maswali yako majibu unayo ndugu.
Hii inchi ina safari ndefu kama kulalamiko ndo huko? Ungesema jukwaa gani linatembelewa kwa wingi na kwa nini? Na kwa nini jingine alitembelewi ungekuwa umeongeza tija. Otherwise zero.
 
Post mzuri na elimishi lakini haitapata wachangiaji maana haihusu mapenzi wala yanga na simba au umbea wa mjini.
Ndo maana wanasema sisi watanzania hatupendi vitu vya maana ila umbeya usio na maana. Thus mafanikio yanakuwa kwa wachache.
 
Duuh bro umenigusa kwa kwel kwa mwezi mmejitahidi kusave ni laki moja tuu na ukiisha mwez navunja kibubu ila sasa nimepania kwa kila mwezi ninunue kuku wa kienyeji atleast watano nianze ufugaji i think baada ya mwaka mmoja nitaleta mrejesho
 
Duuh bro umenigusa kwa kwel kwa mwezi mmejitahidi kusave ni laki moja tuu na ukiisha mwez navunja kibubu ila sasa nimepania kwa kila mwezi ninunue kuku wa kienyeji atleast watano nianze ufugaji i think baada ya mwaka mmoja nitaleta mmrejesho

Duuh bro umenigusa kwa kwel kwa mwezi mmejitahidi kusave ni laki moja tuu na ukiisha mwez navunja kibubu ila sasa nimepania kwa kila mwezi ninunue kuku wa kienyeji atleast watano nianze ufugaji i think baada ya mwaka mmoja nitaleta mrejesho
Sawa bro, mwanzo mgumu ila mwisho ni mwema sana. Anza sasa
 
Back
Top Bottom