show me the way
Member
- Dec 10, 2020
- 48
- 111
Nipo katika kipindi kigumu cha Maisha kwa sasa ambapo changamoto zimekuwa kubwa sana na zinanibana. Nina degree ya utawala, pamoja na uzoefu na ujuzi katika mauzo, masoko, ukusanyaji wa data, na uandishi wa miradi. Aidha, nina ujuzi kompyuta, na uzoefu wa miaka 7 kwenye kazi na rekodi nzuri.
Kwa miaka 9 iliyopita, nimekuwa nikifanya biashara lakini sijaridhika na matokeo. Mara nyingi, biashara inafilisika sasa najikuta nikiumia hasa kwa kuzingatia majukumu yangu kama baba wa familia na nategemewa hivyo nimeamua kuachana kabisa na biashara kwa sasa.
Ndugu zangu, ninawaomba msaada wenu. Kama mdau wa jamii forum, naomba uniunganishe na fursa za kazi ambazo unadhani zinakidhi sifa na uzoefu wangu. Hata kama sijaelezea kila kitu hapa, nina hakika kwamba nina uwezo wa kufanya kazi katika maeneo yanayofanana na ujuzi niliouelezea.
Nipo Dar es Salaam kwa sasa, lakini nipo tayari kufanya kazi popote nchini. Ninajiamini katika kuzungumza lugha ya Kiingereza na Kiswahili vizuri.