Furaha Dominic, Mpwa wa Hayati Magufuli apandishwa Kizimbani kwa kusambaza Picha za Ngono

Wanaume wawili, Furaha Jacob pamoja na Mustapha Kuhenga (28) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakituhumiwa kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Jacob ambaye ni mkemia na Kuhenga mtaalamu wa TEHAMA, wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi amesema shtaka la kwanza la shambulio la mtandao linamhusu Jacob pekee ambapo Februari 11, 2024 anadaiwa kutuma video WhatsApp yenye maudhui ya ngono kupitia simu yake kwa lengo la kumtishia Mihayo.

Kwa upande wa Kuhenga anadaiwa kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 alituma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu yake kupitia mtandao wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo Mihayo.

Shtaka la mwisho linawahusu watuhumiwa wote wawili ambapo wanadaiwa kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp za Mihayo Desemba Mosi 2023 na Machi 2024.

Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

Swahili Times
Duuh huyo Adamu ni nani? Alifanya nini na hizo picha walizipata wapi?
 
Tajiri kijana kabisa. Kijana mtanashati. Kiongozi mkubwa kabisa pale TCB.
Vijana walistalk ili wapate video wazitumie kupiga hela. Kijana ndio mambo yake huyo. Ishukuriwe tripple 7 imefungwa. Ndio vuna pesa style yake huyo.
Hebu nikumbushe Tripple 7 ni wapi.
 
Furaha amejaa kwenye 18!

Alipokuwa kwenye tume ya makinikia alikuwa mbabe sana Hadi Kwa prof M. Furaha ni bilionea. Ana semi zaidi ya 10, furaha FM, furaha tv, Maza yake kamnunulia vanguard na T.,...D, mjomba ake wa ukweli FS amempa noti nyingi sana.

Dogo anakiburi sana.
Subiri kwanza,unaelewa tafsiri ya neno bilionea? Semi 10 haziwez kumfanya mtu kuwa bilionea Tengua kauli ndo tuendelee na mjqdala!!
 
Furaha Jacob, ambaye ni mkemia na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili ni Mustapha Kuhenga(28) ambaye ni mtaalamu wa Tehama na mkazi wa Mwenge.

Washtakiwa hao wanadaiwa kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Jacob na mwenzake wamefikishwa Mahakamani hapo jana jioni Jumanne, April 23, 2024 na kusomewa mashtaka hayo na wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi.

Mbilingi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya, kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 10709/2024.

Akiwasomea mashtaka yao, Wakili Mbilingi alidai katika shtaka la kwanza ambalo ni shambulio la mtandao linamkabili mshtakiwa Jacob, pekee yake.

Jacob anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 11, 2024 katika sehemu isiyofahamika katika jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, Jacob anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa nia ya kumtisha, Adam Mihayo.

Shtaka la pili ni shambulio la mtandao linalomkabili Kuhenga pekee yake, tukio analodaiwa kulitenda kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 sehemu isiyofahamika, jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, Kuhenga anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Shtaka la tatu ni kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa Kijamii wa WhatsApp Messenger.

Wakili Mbilingi alidai, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kulitenda kosa hilo, Desemba Mosi 2023 na Machi 2024, sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walichapisha picha za video za ngono kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii WhatsApp za Adam Mihayo.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao, wamekana kutenda na kisha kuomba dhamana.

Hakimu Mbuya alitaja masharti ya dhamana ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa wawe na barua mbili na moja wapo kati ya hizo iwe inatoka kwenye taasisi inayotambulika kisheria.

Pia, wadhamini hao wanatakiwa kusaini dhaman ya Sh 3milioni. Washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana na wapo nje kwa dhamana. Hakimu Mbuya aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa.

Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

MWANANCHI
Kabla huja jaribu ku black mail viongozi, make shure una backup plan ya nguvu. When things go south uwe na plan
 
Furaha amejaa kwenye 18!

Alipokuwa kwenye tume ya makinikia alikuwa mbabe sana Hadi Kwa prof M. Furaha ni bilionea. Ana semi zaidi ya 10, furaha FM, furaha tv, Maza yake kamnunulia vanguard na T.,...D, mjomba ake wa ukweli FS amempa noti nyingi sana.

Dogo anakiburi sana.
Huyu dogo kumbe alikuwemo kwenye tume ya makinikia?
 
we umesahau mabilionea wa Arusha? mtu ana V8 mbili na range moja tayari bilionea
billionaire lazima uwe una miliki vitu au hela vyenye thamani ya $1B na kuendelea sio Tsh au ksh

millionaire $1M nakuendelea

kwaiyo wewe kama una Tsh million 1 utaitwa millionaire ?
 
Furaha Jacob, ambaye ni mkemia na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili ni Mustapha Kuhenga(28) ambaye ni mtaalamu wa Tehama na mkazi wa Mwenge.

Washtakiwa hao wanadaiwa kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Jacob na mwenzake wamefikishwa Mahakamani hapo jana jioni Jumanne, April 23, 2024 na kusomewa mashtaka hayo na wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi.

Mbilingi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya, kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 10709/2024.

Akiwasomea mashtaka yao, Wakili Mbilingi alidai katika shtaka la kwanza ambalo ni shambulio la mtandao linamkabili mshtakiwa Jacob, pekee yake.

Jacob anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 11, 2024 katika sehemu isiyofahamika katika jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, Jacob anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa nia ya kumtisha, Adam Mihayo.

Shtaka la pili ni shambulio la mtandao linalomkabili Kuhenga pekee yake, tukio analodaiwa kulitenda kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 sehemu isiyofahamika, jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, Kuhenga anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Shtaka la tatu ni kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa Kijamii wa WhatsApp Messenger.

Wakili Mbilingi alidai, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kulitenda kosa hilo, Desemba Mosi 2023 na Machi 2024, sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walichapisha picha za video za ngono kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii WhatsApp za Adam Mihayo.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao, wamekana kutenda na kisha kuomba dhamana.

Hakimu Mbuya alitaja masharti ya dhamana ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa wawe na barua mbili na moja wapo kati ya hizo iwe inatoka kwenye taasisi inayotambulika kisheria.

Pia, wadhamini hao wanatakiwa kusaini dhaman ya Sh 3milioni. Washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana na wapo nje kwa dhamana. Hakimu Mbuya aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa.

Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

MWANANCHI
MADHARA YA KUMTEGEMEA MWANADAMU (mwendazake)
 
Back
Top Bottom