Jan 20, 2015
15
33
Furaha Dominic anashitakiwa kwa kosa la kurekodi video zisizo na maadili za viongozi mbalimbali kisha kuzitumia kujipatia pesa kwa kuwatisha (blackmailing).

Furaha Dominic ni yule kijana ambaye Magufuli alimkata jina na kusisitiza kuwa hafai kuwa mbunge wa Kawe. Magufuli huenda alikuwa anajua shughuli za huyu kijana na namna anavyojipatia pesa.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi, kanda maalumu ya Dar es Salaam Inspk Murilo amesema ushahidi wa awali umekamilika na mtuhumiwa atafikikishwa mahakamani.

Chanzo Uhondo Tv

Video iko chini


---


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mauaji ya watu wawili, Japhari Mwinyimvua (40) mlinzi na Richard Nonyo (65) baba mzazi wa mtu anayedaiwa ni mganga wa kienyeji wa eneo hilo.

Tukio hilo limetokea Aprili 21, 2024 majira ya saa 3 asubuhi maeneo ya Kigogo fresh, Pugu, Ilala ambapo mlinzi huyo alikutwa ameshambuliwa na baadae kupoteza maisha. Hata hivyo katika mtiririko huo kundi la watu lilimshambulia baba mzazi wa mganga huyo na baadae akapoteza maisha wakimtuhumu mtoto wake kuhusika na kifo cha mlinzi huyo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wanachunguza kwa kasi tukio hilo na wahusika wote wa tukio hili watakamatwa haraka iwezekanavyo na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria .

Katika hatua nyingne, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Furaha Dominick Jacobo (32) mkazi wa Masaki na Mustafa Kihenga (28) mkazi wa Mwenge TRA kwa tuhuma za uhalifu wa kimtandao kwa kusambaza picha chafu za video za watu zisizo na maadili kwa lengo la kujipatia fedha kwa vitisho.

Watuhumiwa hawa wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo kujibu tuhuma zanazowakabili.

Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam


UPDATE
- Furaha Dominic, Mpwa wa Hayati Magufuli apandishwa Kizimbani kwa kusambaza Picha za Ngono
 
Back
Top Bottom