furaha dominic

Furaha Dominic
Furaha Dominic ni mpwa wa Rais wa awamu ya ya Tano ya Tanzania, hayati John Magufuli.

Julai 21, 2020 aliongoza kura za maoni Jimbo la Kawe baada ya kupata kura 101 kati ya 474 zilizopigwa akifuatiwa na Angela Kiziga aliyepata kura 85. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima aliyepata kura 79. Kippi Warioba akipata kura tatu kati ya 475.

Hata hivyo Askofu Josephat Gwajima aliteuliwa na kamati kuu kuwania ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM na kumuangusha mbunge wa upinzani aliyekuwepo kwa tiketi ya Chadema, Halima Mdee.

Mwaka 2024 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilimkamata Furaha Dominick Jacobo (32) na Mustafa Kihenga (28) kwa tuhuma za uhalifu wa kimtandao kwa kusambaza picha chafu za video za watu zisizo na maadili kwa lengo la kujipatia fedha kwa vitisho.
  1. BARD AI

    Furaha Dominic, Mpwa wa Hayati Magufuli apandishwa Kizimbani kwa kusambaza Picha za Ngono

    Furaha Jacob, ambaye ni mkemia na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni. Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili ni Mustapha Kuhenga(28) ambaye ni mtaalamu wa Tehama na...
  2. Yehoyada Yedidia

    Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

    Furaha Dominic anashitakiwa kwa kosa la kurekodi video zisizo na maadili za viongozi mbalimbali kisha kuzitumia kujipatia pesa kwa kuwatisha (blackmailing). Furaha Dominic ni yule kijana ambaye Magufuli alimkata jina na kusisitiza kuwa hafai kuwa mbunge wa Kawe. Magufuli huenda alikuwa anajua...
  3. J

    Furaha Dominic leo ataendelea na Mahojiano. Je, atawataja Kupe waliomnyonya hayati Magufuli?

    Furaha Dominic ni mpwa wa hayati Magufuli. Jumatatu alikuwa na mjadala katika kipindi cha The Big Agenda kinachorushwa na Star tv. Kutokana na mambo mengi aliyokuwa nayo muda wa kipindi haukutosha hivyo mtangazaji nguli Aloyce Nyanda aliahirisha hadi leo saa 3:30 usiku. Furaha awali alielezea...
  4. The Khoisan

    Furaha Dominic: Askofu Gwajima ndiye kiongozi wa kundi linalomkwamisha Rais Samia

    Kwenye interview ya Furaha, amemchanachana Askofu Gwajima kwa kusema kuwa ni MNAFIKI na MUONGO. Kazungumzia vipi alivyowatapeli wananchi wa Kawe kwa kudai kuwa ndani ya siku 100 atawajengea wana Kawe Barabara na kuwapeleka Birmingham. Kwa kweli Gwajima amekuwa Muongo kwa siku nyingi sana...
  5. J

    Furaha Dominic: Rais Samia awe mwangalifu na hao waliomzunguka, wengi wao ni Wafitinishi (KUPE) walimdanganya Magufuli!

    Furaha Dominic ambaye ni mpwa wa hayati Magufuli aliyegombea ubunge jimbo la Kawe na kushika nafasi ya kwanza huku Pascal Mayalla akiwa wa 162 amesema siku atakayokutana na Rais Samia atampa orodha ya Wafitini wote waliomzunguka. Furaha anadai CCM kumejaa siasa chafu za kupakana matope...
  6. J

    Furaha Dominic: Hakuna tofauti ya Uongozi kati ya Hayati Magufuli na Rais Samia

    Furaha Dominic ambaye ni mtoto wa dada wa hayati Magufuli amesema haoni tofauti yoyote kati ya utawala wa mjomba wake na Rais wa sasa mh Samia. Dominic ambaye aligombea ubunge Kawe amesema hajawahi kumuona mtu mwongo hapa duniani kama askofu Gwajima. Kipindi kiko mubashara Star tv, karibu...
Back
Top Bottom