Furaha Dominic, Mpwa wa Hayati Magufuli apandishwa Kizimbani kwa kusambaza Picha za Ngono

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,386
8,134
1713981801618.png
Furaha Jacob, ambaye ni mkemia na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Mbali na Jacob, mshtakiwa wa pili ni Mustapha Kuhenga(28) ambaye ni mtaalamu wa Tehama na mkazi wa Mwenge.

Washtakiwa hao wanadaiwa kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Jacob na mwenzake wamefikishwa Mahakamani hapo jana jioni Jumanne, April 23, 2024 na kusomewa mashtaka hayo na wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi.

Mbilingi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Romuli Mbuya, kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 10709/2024.

Akiwasomea mashtaka yao, Wakili Mbilingi alidai katika shtaka la kwanza ambalo ni shambulio la mtandao linamkabili mshtakiwa Jacob, pekee yake.

Jacob anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 11, 2024 katika sehemu isiyofahamika katika jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, Jacob anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa nia ya kumtisha, Adam Mihayo.

Shtaka la pili ni shambulio la mtandao linalomkabili Kuhenga pekee yake, tukio analodaiwa kulitenda kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 sehemu isiyofahamika, jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo, Kuhenga anadaiwa kutuma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu ya mkononi kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Shtaka la tatu ni kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa Kijamii wa WhatsApp Messenger.

Wakili Mbilingi alidai, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kulitenda kosa hilo, Desemba Mosi 2023 na Machi 2024, sehemu isiyojulikana jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa katika kipindi hicho, washtakiwa walichapisha picha za video za ngono kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii WhatsApp za Adam Mihayo.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao, wamekana kutenda na kisha kuomba dhamana.

Hakimu Mbuya alitaja masharti ya dhamana ambayo ni kila mshtakiwa anatakiwa wawe na barua mbili na moja wapo kati ya hizo iwe inatoka kwenye taasisi inayotambulika kisheria.

Pia, wadhamini hao wanatakiwa kusaini dhaman ya Sh 3milioni. Washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana na wapo nje kwa dhamana. Hakimu Mbuya aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 9, 2024 kwa ajili ya kutajwa.

Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

MWANANCHI
 
Wanaume wawili, Furaha Jacob pamoja na Mustapha Kuhenga (28) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakituhumiwa kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Jacob ambaye ni mkemia na Kuhenga mtaalamu wa TEHAMA, wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi amesema shtaka la kwanza la shambulio la mtandao linamhusu Jacob pekee ambapo Februari 11, 2024 anadaiwa kutuma video WhatsApp yenye maudhui ya ngono kupitia simu yake kwa lengo la kumtishia Mihayo.

Kwa upande wa Kuhenga anadaiwa kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 alituma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu yake kupitia mtandao wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo Mihayo.

Shtaka la mwisho linawahusu watuhumiwa wote wawili ambapo wanadaiwa kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp za Mihayo Desemba Mosi 2023 na Machi 2024.

Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

Swahili Times
Hapa suku gang wanapita kimya kimya 🤣🤣
 
Hawa watu hizo picha za ngono za huyo Adam Mihayo wamezipata wapi? Huyo Adam Mihayo picha hizo alijirekodi yeye mwenyewe kwa hiyari yake au alirekodiwa kwa Siri bila ridhaa yake?
 
Wanaume wawili, Furaha Jacob pamoja na Mustapha Kuhenga (28) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakituhumiwa kuchapisha na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Jacob ambaye ni mkemia na Kuhenga mtaalamu wa TEHAMA, wanakabiliwa na mashtaka matatu ikiwa ni pamoja na kumtisha na kumsababishia msongo wa mawazo, Adam Mihayo.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi amesema shtaka la kwanza la shambulio la mtandao linamhusu Jacob pekee ambapo Februari 11, 2024 anadaiwa kutuma video WhatsApp yenye maudhui ya ngono kupitia simu yake kwa lengo la kumtishia Mihayo.

Kwa upande wa Kuhenga anadaiwa kati ya Desemba Mosi na Desemba 31, 2023 alituma video yenye maudhui ya ngono kwa kutumia simu yake kupitia mtandao wa WhatsApp na kumsababishia msongo wa mawazo Mihayo.

Shtaka la mwisho linawahusu watuhumiwa wote wawili ambapo wanadaiwa kuchapisha picha zenye maudhui ya ngono kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp za Mihayo Desemba Mosi 2023 na Machi 2024.

Pia soma
- Furaha Dominic akamatwa akisambaza picha za Utupu

Swahili Times
The Sherrif, Suley, Joving Journalism, Erythrocyte, Jaji Mfawith tunaomba Live Updates ya kesi hizi huko Mahakamani.

Natanguliza Shukrani
 
Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Cathbert Mbilingi amesema shtaka la kwanza la shambulio la mtandao linamhusu Jacob pekee ambapo Februari 11, 2024 anadaiwa kutuma video WhatsApp yenye maudhui ya ngono kupitia simu yake kwa lengo la kumtishia Mihayo.
Mbinu zile zile zilizotumima kuwa Intimidate waunga mono Juhudi wa mjomba.
 
Back
Top Bottom