Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,037
- 9,926
Jeshi la Polisi limemkamata wakili Yonas Masiaya na kumnyima dhamana. Tukio hilo limetokea jana jioni, Aprili 30, 2024, huku likiwaacha wengi wakijiuliza maswali kuhusu utaratibu wa kisheria.
Wakili Masiaya anatuhumiwa kwa kosa la kusambaza picha ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika makundi ya WhatsApp. Hata hivyo, licha ya tuhuma hizo kuonekana kuwa dhaminika, Jeshi la Polisi limekataa kumpa wakili huyo dhamana, wakisema wanangojea maelekezo kutoka ngazi za juu.
Leo, Mei Mosi, 2024, wakili Ngeeyan Oloibormunyei Laizer pamoja na familia ya wakili Masiaya wamejitokeza katika kituo cha Polisi kufuatilia suala hilo. Hata hivyo, jitihada zao zimegonga mwamba baada ya Polisi kudai bado wanangojea maelekezo kutoka kwa viongozi wao.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeelekeza mawakili wake mkoani Arusha kuchunguza kwa karibu suala hilo na tayari wameanza maandalizi ya kufungua kesi dhidi ya Jeshi la Polisi kwa kushindwa kumpa dhamana wakili Masiaya.
Wito umetolewa kwa Jeshi la Polisi:

- Kumwachia wakili Masiaya kwa dhamana.
- Kufanya upelelezi kwa kuzingatia Sheria na Amri Kuu za Jeshi la Polisi (PGO), bila kusubiri maelekezo kutoka juu ambayo ni nje ya utaratibu wa kisheria.
- Kufanya upelelezi kabla ya kumkamata wakili Masiaya endapo kuna tuhuma dhidi yake.
- Kudai mabadiliko ya sheria ya makosa ya kimtandao ili kulinda uhuru wa watanzania katika matumizi yao ya mitandao kwa kuzingatia Sheria za ulinzi wa taarifa na faragha.