Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,759
- 107,116
Salute
Nakumbuka kipindi nipo secondary kwenye masomo yangu pendwa hasa Biology karibia kila terminology nililiyokua nasoma kwenye definition yake ilikua inaanza na maneno “it’s a Greek word”, swali kubwa nililokua nabaki nalo na mpaka sasa hua najiuliza ni kwamba..Je wagiriki ndio watu wenye akili zaidi hapa duniani maana inaonyesha kila kitu tunachotumia sasa misngi ya kitu hicho imegunduliwa ugiriki. Hata watu maarufu na wenye akili nyingi zaidi kama Euclid, Pythogras, Socrates, Plato, Achimedes, Temistokles, wanatokea huko ugiriki na muundo wa maisha tunayoishi hapa duniani imetengenezwa na hao hao wagiriki.
NB. Majina ya kiume yote ya wagirki yanaishia na herufi S ili kumuenzi mungu wao wa miungu ZEUS (ndio maana jina la Jesus laishia S pia)
Hua najiuliza ni wazungu pekee ndio wamefanya vumbuzi kubwa humu duniani sisi watu weusi hatujafanya chochote wala hakuna watu waliofanya vitu vikubwa hapa duniani? Ukweli ni kua wapo wengi wamefanya makubwa hapa duniani na kuleta Civilizations kubwa katika maeneo mengi hapa duniani.
Ukweli mchungu ambao watu weupe hawataki kuukubali ni kwamba Afrika hasa misri ya kale ndio kitovu cha ustaarabu na Elimu duniani kote.
Kwa kujua hilo ndio maana wazungu wanalazimisha kutuaminisha vizazi vya sasa tusiopenda kuchimba mambo kua wamisri wa kale walikua watu weupe/Wazungu kwa kutumia vitabu na filamu mbalimbali.
Ukweli usiopingika ni kwamba Misri ya kale ndio kitovu cha mambo mengi katika ustaarabu wa mwanadamu ila tu hawataki kukubali kua ni mtu mweusi ndio kafanya hayo sifa zote hua zinaenda kwa wagiriki, wakati mfamle temistokles wa Jiji la Athens (Ugirki) anahangaika kuhamasisha wafalme wa majiji mengine kama Queen Gogo, King Leonidas waungane wawe taifa moja wao wamisri walikua wanafanya vumbuzi kubwa kubwa zilizoacha ulimwengu kinywa wazi. Nitaorodhesha baadhi ya mambo machache ambayo yamegunduliwa na wamisri weusi kipindi hiko hata Amerika kunakaa nyani na sokwe ,Red Indian na Wamaya
Baadhi ya vitu vilivyogunduiwa na wamisri
- Mathematics
- Maandishi
- Dawa ya meno
- Wigi, Make-Up na Vipodozi
- Wino Mweusi, Karatasi na Meza
- Mashine za kuvuna na kusaga nafaka na kilimo cha umwagiliaji
- Majira na Kalenda
- Kufuli
- Polisi na Serikali
- Egyptian Hieroglyphics
Hii ni michoro adhimu kabisa iliyobuniwa na wazee wa kiafrika ili kuwasiliana, pia zilikua zinatumika kueleza matukio yaliyopita na yajayo..so ilitumika kuweka rekodi za jamii ya watu wa misri. Unaweza kuona mchorouiliochorwa miaka zaidi ya elfu tano iliyopita ukionyesha image ya aeroplane ni ile ie iliyochorwa na Davinci miaka ya 1600sBC. Michoro hii hakuna wengine walioweza utengeeneza kama wamisri walivyofanya japo na wamaya walijitahidi kiasi chao kwenye ustaarabu wao.. mpaka leo zimebaki kama alama ya kutambulisha falme ya misri
- Vifaa vya upasuaji
- Mummification
Hii ndio moja ya teknoljia kubwa sana kwa kipindi hicho ambayo imetengenezwa na wamisri, hii ilikua teknoljia ya kuhifadhi miili ya marehemu hasa wafalme. Kwa kutumia njia hii inawezesha kugundua ugonjwa uliomua hata baada ya miaka 1000. Hukojuu nimesema kua wamisri waliamini kuzika watu kwa heshima kunaweza kuwafanya wakaenda mbinguni, hivyo kwa upande wa wafalme au watu wenye heshima mjini enzi hizo walifanya hii mummification. Walikua wakizikwa wanazikwa na vyakula,nguo safi mabegi kadhaa, masanduku ya dhahabu na vitu vya thamani.waliamini kua siku wakifufuka watavitumia ila cha kufurahisha zaidi ni kwamba kuna watu walikua wanajitolea kuwasindikiza marehemu wwakiwa wazima kabisa tena walikua wanagombania hiyo nafasi kweli. Ndio maana unaweza kuta Farao kazikwa na watu zaidi ya mia wakiwa wazima.
Mazishi yao yalifanyika kwenye pyramids huko, moja ya vumbuzi kubwa na la ajabu kuwahi tokea duniani.
Moja ya watu muhimu kutoka misri kuwahi tokea duniani aliyefanya mambo makubwa sana hadi wagiriki walibidi wamuabudu kama Mungu wao anaweza kua binaadamu mwenye akili nyingi zaidi tutamzungumzia panapo majaliwa....
Wazungu hawatatu-Appreciate public ila kimoyo moyo wanajua sana kua bila sisi wao hawawezi kuishi humu duniani. Enzi zile kila mzungu ndoto yake kubwa ilikua kuja kusoma jijini Alexandria. Hili jiji ndio lilikua kitovu cha Elimu duniani, Topic nyingi za hisabati ulizowahi kusoma zimefanyiwa tafiti hapo.
Itaendelea....
~Da’Vinci