Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,899
- 155,954
MISRI ni nchi inayozunguka kona ya kaskazini mashariki ya bara la afrika hadi kwenye Rasi ya Sinai kusini magharibi mwa bara la Asia
Nchi ya Misri imepakana na nchi kama Israel, Palestine, Jordan, Sudan na Libya
Pia imepakana na bahari za Mediterranean na bahari nyekundu
Nchi ya Misri ina watu milion 100 ni nchi ya 14 kwa wingi wa idadi ya watu duniani huku kwa afrika ikiwa nafasi ya tatu ikitanguliwa na Nigeria na Ethiopia tu
Kabla ya mwaka 1953 nchi ya Misri ilikuwa ikiongozwa kifalme kabla ya utawala wa kifalme kupinduliwa ......tokea hapo hadi sasa ni maraisi SITA wameiongoza Misri huku raisi aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani ni Hosni Mubaraka aliyeiongoza Misri kuanzia 1981 hadi 2011
Raisi wa sasa was Misri ni Abdel Fattah el-Sisi
MISRI ni nchi yenye historia kubwa duniani huwezi kutajaa taaluma yoyote duniani bila kuitaja Misri kuanzia hesabu, sayansi, utawala, fasihi, usanifu wa Majengo, hata dini n.k
Ni miongon mwa nchi kongwe zaidi duniani zaidi ya karne na karne kabla ya kuzaliwa YESU KRISTO Nchi ya Misri ilikuwepo zaidi ya miaka elfu 5
Kwahiyo historia ya Misri ni kubwa saana kila utakavyoielezea bado hutoimaliza
YAFUATAYO NI MAMBO MACHACHE USIYOYAJUA KUHUSU NCHI YA MISRI
1) Wamisri wa kale ndio waanzilish wa dawa ya meno ambapo walichanganya chumvi, majani ya mnanaa ( mint) pilipili, na maji .....kisha walitumia miswaki ya miti au nguo kusugua meno yao
2) Tokea mwaka 972 CAIRO ulikuwa mji mkuu wa Nchi ya Misri kwahiyo ni zaidi ya miaka elfu 1 Cairo ni mji mkuu wa Misri ....unashikilia rekodi ya mji mkuu mkongwe zaidi duniani ijapo inasemekana kuna mji mkuu mpya unatengenezwa nchin Misri
3) Kihistoria wanawake wa kimisri walikuwa na haki sawa na wanaume kumiliki Mali, kuwa viongozi wa dini, kufanya biashara hata kuwa na haki za kumuacha MUME yaan kumpa talaka au kuomba talaka
4) Wamisri wa kale walikuwa wanapenda na kuwaabudu paka ....wakiamini kupata mema hata mtu anayezikwa na paka wanaamini huyo ni moja kwa moja pepon kumuua au kumdhuru paka kwa aina yoyote inaweza kupata adhabu ya kifo
5) Wamisri wa kale walikuwa na zaidi ya MIUNGU 2000 ambaye kila MUNGU walimuomba kwa jambo fulani...kulikuwa na Mungu wa vita, Mungu wa njaa, Mungu wa mapenz n.k
6) Mgomo wa kwanza wa wafanyakazi duniani umetokea MISRI katika miaka ya 1152 kabla ya kuzaliwa YESU KRISTO ...ambapo wafanyakazi waligoma kufanya kazi kwa sababu HAWAJALIPWA
7) Sanamu kongwe zaidi duniani lipo Misri ... Sanamu la sphinx ambalo Lina kichwa cha binadam na mwili wa simba inasemekana lilitengenezwa katika kipindi cha Khafre (c. 2558–2532 BC).
8) Wamisri wa kale walianzisha kalenda yao yenye siku 365...miezi 12 ya mwaka ambayo ina siku 30 kwa mwezi ....lakini utajiuliza 12*30 ni 360 je hizo siku 5 zimeenda wapi ...jibu ni kuwa hizo siku tano ni siku za kuzaliwa MIUNGU yao Mitano ambayo ni Osiris, Horus, Seth, Isis, na Nephtys Seth alikuwa ni Mungu wa maovu
Lakini kalenda zao ziliwasaidia kwenye masuala ya kuabudu na kilimo
9) Nguo kongwe zaidi duniani imetokea Misri..... Nguo hiyo waliipa jina la Tarkhan ilipatikana mwaka 1913 na inakadiriwa kuwa ina zaidi ya miaka elfu 5
10) Asilimia 90 ya raia wa MISRI ni waislam huku ni asilimia chini ya 10 ndio wakristo ....lakini.... hapo awali Misri ilikuwa ni mji muhimu wa kikristo kabla ya UISLAM kuingia mwaka 639 baada ya kuzaliwa YESU KRISTO.... ijapo kuwa Wamisri wa kale walianza kuabudu Mungu zaidi ya miaka elfu 3 kabla ya kuzaliwa YESU KRISTO
11) Mfereji wa Suez canal ndio njia rahis ya majini kwa waarabu kuingia ulaya...kabla ya hapo ilibidi waarabu wazunguke saana kufika bara la ulaya ... Mfereji wa Suez canal ulianza kujengwa mwaka 1859 hadi 1869 .......mfaransa Ferdinand De Lesseps alipewa ruhusu kujengwa Mfereji huu ..
12) Misri ndio wazalishaji wakubwa wa TENDE duniani....asilimia 17 ya tende zote hutokea MISRI
13) Afrika kuna nchi mbili tu zenye METRO ( underground railway system) ni jiji la Alger nchini Algeria na wewe Jiji la Cairo nchini Misri
14) Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Misri ndio iliyofanikiwa zaidi katika historia ya afrika huku Al Ahly ndio timu iliyofanikiwa zaidi kisoka baran afrika kwa ngazi ya vilabu
15) Mkataba wa Amani wa Kadesh ndio Mkataba wa kwanza wa amani ( peace treaty) duniani ulifanyika MISRI...ni kipindi cha Shaba (bronze age) katika kipindi hicho ndio teknolojia inaanza kukua... biashara baina ya nchi na nchi ...bara na bara ndio zinaanza kushamiri........ Mwaka 1274 kabla ya kuzaliwa YESU KRISTO kulitokea vita baina ya Mfalme Muvattalli II wa Hittite dhidi ya mfalme Ramesses II wa MISRI ya kale........ himaya hizi mbili zilizo na nguvu duniani kwa wakati huo kugombania eneo MUHIMU la kibiashara la Kadesh
Mwisho wa siku wakaona suluhu peke ya kutatua mgogoro huo ni Mkataba wa Amani baina yao ndio wakaweka Mkataba wa kwanza wa amani duniani .....mfano wa Mkataba huo upo katika jengo la umoja wa mataifa New York
16) Mto Nile ndio mto mrefu zaidi DUNIANI...watu wa kale wa MISRI waliuita kama mto wa maisha kutokana na umuhim wake kwenye shughul zao za kimaisha