Eleza changamoto unazokutananazo ukiwa kama 'Programmer' mpya unayejifunza mwenyewe

Patiee

JF-Expert Member
Sep 20, 2018
474
718
Binafsi najifunza programming just for fun and enjoyment ya kupata maarifa mapya.
Nimeanza na HTML pamoja na CSS kadri siku zinavyoenda tutapeana updates ya jinsi darasa linavyoenda.

Site nizitumiazo Kwa sasa ni
  • Freecode camp
  • Solo learn.

Pamoja na Youtube channels kama;
  • The net ninja.
  • Brad traversy

Nakaribisha wanafunzi wote kuleta changamoto zao ili wabobezi watoe ufafanuzi. Binafsi mimi nasumbuliwa kwenye suala zima la Ku comment na uncomment kwenye HTML (najua it sounds funny kwa wajuzi)

Nawasilisha.


UPDATE - APRIL 2024

I'M A PROFESSIONAL SOFTWARE DEVELOPER


Ni miaka 4 imepita sasa. Sikumbuki mara ya mwisho kusoma huu uzi ilikuwa ni lini lakini leo nimeupitia na nimejicheka sana.

Hapo juu niliandika kwamba nilikuwa nasumbuliwa na ku comment code😂😂. Hivi mtu unasumbuliwaje na kufanya kitu kama hicho 😂.( Kwa usiyefahamu ku add comments kwenye code , fikiria jambo lolote jepesi zaidi kwenye fani yako)

Kwa sasa nafanya kazi kwenye Moja ya kampuni za takwimu hapa nchini kama Software Developer.

Sikufichi, Kuna muda unaweza jiona kama you're not good enough for this, lakini that is just a day in the life of a software developer.

Katika miaka 4 ilopita, nimejifunza mengi na naendelea kujifunza kila siku.

Ewe unayeanza, usikate tamaa Wala usiishie njiani ... Kaza go damnit

Adios !
 
Freecode camp ni nzuri ila ningekushauri ujifunzie kwenye website ya w3schools utajifunza mengi zaidi na utapata exercises kila baada ya kujifunza kitu flani
 
HTML unaweza kujua hata siku moja ila kuja kuiremba kwa CSS sasa confusions kwa sisi Newbies
 
Huwezi kusema unajifunza programming kwa kusoma css na html coz hizi sio programming languages.
Acha USHAMBA wewe.

Kujifunza html na css ni moja ya step za kujifunza programming japo hizo sio programming lang's.

Unaweza kwenda kujifunza karatee ukashangaa unaambiwa zoezi la kwanza ni kuvaa na kuvua koti ndo utashangaa sasa.


Patiee Endelea kula tutorials next step iwe Javascript au python
 
Acha USHAMBA wewe.

Kujifunza html na css ni moja ya step za kujifunza programming japo hizo sio programming lang's.

Unaweza kwenda kujifunza karatee ukashangaa unaambiwa zoezi la kwanza ni kuvaa na kuvua koti ndo utashangaa sasa.


Patiee Endelea kula tutorials next step iwe Javascript au python
Hapana, siwezi kuacha ushamba kwa hilo jambo.
 
I agree with you, miaka km mitatu au minne hv nilianzisha harakati za kujifunza programming ila baada ya miezi sita tu niliacha sababu kuu pc yangu ilivunjika kioo basi darasa likaishia hapo hapo ila very soon narudi ulingoni tena this year na mimi naahidi kutoa feedback jinsi darasa likavyokua linaendelea!
Ni kweli siyo programming languages lakini html na css ni msingi mzuri wa kuanzia katika programming.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom