Dizasta vina

Dizasta Vina ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yake na ni mwanaume pekee akiwa na dada zake wawili, alizaliwa mnamo tarehe 17 Februari 1993. Ingawa kiasili ni Mnyakyusa kutoka Mbeya (mkoa uliopo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania) alizaliwa mkoa wa Iringa kabla ya wazazi wake kuhamia Dar es Salaam ambako alianza shule.

Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi ya "Kimanga" iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam aliandikishwa katika shule hiyo mnamo mwaka wa 2000. Mwaka wa 2007 alijiunga na elimu ya sekondari katika shule binafsi ya "White Lake High School" iliyopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es Salaam kisha kumaliza masomo ya sekondari katika shule ya "Southern Highlands Secondary School" iliyopo Soweto jijini Mbeya — mnamo mwaka wa 2O1O. Aliendelea na kidato cha tano katika shule ya "Kigoma High School" mkoani Kigoma ambapo alisoma kwa muda wa miezi minne tu kabla ya kumalizia masomo yake ya elimu ya sekondari katika shule ya "Mbeya High School". Dizasta alijiunga na masomo ya elimu ya juu mwaka wa 2013 katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kilichopo jijini Dar es Salaam na kusoma shahada ya kwanza ya uhasibu.


Source Wikipedia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom