tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 22,097
- 18,719
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"
"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"
"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili
MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.