tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,962
18,471
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"

1712736007088.jpeg

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.
 
Mchungaji na mwimbaji nguli wa nyimbo za injili, Christina Shusho anadai aliachana na mume wake kwa makusudi ili aanzishe kanisa apige pesa peke yake kwa kuwa aliona akiungana na mume wake wakawa wanagawana maokoto ya sadaka, asingefiika mbali.

Mchungaji huyo amenukuliwa na mitandao ya kijamii akisema maneno hayo bila kumumunya maneno, kupepesa macho wala kutikisa masikio, kama alivyonukuliwa ifuatavyo:

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili
Ninge shangaaa ata ivyo miaka Karne na Karne sikuwai sikia kama kulikua na mchungaji wa kike lakn Leo hii wamejaa wanatupeleka mbio mbio tubadirike kila mtu abaki na Imani yake thabiti Mungu tusaidi tuwe na mawazo mapana ya kukusujudu ww
 
"Kizazi cha nyoka" si Me wala Ke ukizubaa tu unafanywa ngazi ya mafanikio na kupigwa chini.
Ni mwendo wa kuviziana tu, timu kataa ndoa mpewe ulinzi tafadhali.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Ninge shangaaa ata ivyo miaka Karne na Karne sikuwai sikia kama kulikua na mchungaji wa kike lakn Leo hii wamejaa wanatupeleka mbio mbio tubadirike kila mtu abaki na Imani yake thabiti Mungu tusaidi tuwe na mawazo mapana ya kukusujudu ww
Siku hizi kila mtu anataka apige pesa kivyake mkuu. Ndio maana Shusho kachungulia mechi akaona kama akiendelea kuishi na yule mzee atamchelewesha sana kwenye maokoto..
 
haha! acheni kumlisha hayo maneno labda awe amepanda maruhani kusema hivyo!
Kaema kweli mkuu. Fuatlilia mitandao ya kijamii......kila mtu anamshangaa. Alishaasi ndoa tangu kitambo. Leo ameona bora afunguke kabisa kama mbwai iwe mbwai.
 
Yesu alipokubali tu kuoshwa miguu, kufutwa kwa nywele na kupakwa mafuta na yule kahaba ndipo alipokaribisha Malaya kama hawa kanisani. Nadiriki kusema Ukristo una viongozi na watumish wezi sana, wazinzi sana, walafi sana sana na wapotoshaji sana.
 
Apostles tunamuanagalia, tumafuatilia na tunamuombea zaidi hekima katika kunena na kuwanenea waliomfikisha hapo.....

ni swala la muda tu, Bwana hakawii kuitimiza ahadi zake....

hapana kisingizoa uchawi, ushirikina wala mapepo...
 
Yesu alipokubali tu kuoshwa miguu, kufutwa kwa nywele na kupakwa mafuta na yule kahaba ndipo alipokaribisha Malaya kama hawa kanisani. Nadiriki kusema Ukristo una viongozi na watumish wezi sana, wazinzi saba, walafi sana sana na wapotoshaji sana.
Umemaliza kila kitu mkuu. Subiri wenyewe waje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom