Babu Tale na Salam Sk wamekuwa Mameneja wa hovyo sana wanaombebesha Diamond mzigo wa migogoro na media

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,259
42,188
Wasalaam wana JF...

Ni ukweli ulio wazi vyombo vyetu vyote vya habari vinatabia zinazo fanana na vinatofautiana sana kwa kiasi kidogo sana vyombo vyote vinapenda kubembelezwa ,kuabudiwa,kusifiwa na kupewa kipaumbele...lakini pamoja na haya yote wasanii wetu walio wengi wameweza kutoboa akiweno Diamond Platinumz...
Tutakuwa waongo na wanafiki tukihindwa kujua kuwa ukubwa na alipofikia Diamond kwa sasa kumechangiwa sana tena sana na vyombo vya habari hivi ambazo muda mwingine tunaviona vya wanyonyaji au havitoi haki au vina watangazaji wenye chuki na Roho mbaya kwa wasanii wetu tuwapendao.

Lakini pamoja na mabaya mengi ya media hizi Diamond ameweza kufikia hapa na nina fikiri kabisa alikuwa na watu wanao jua zaidi kutatua migogoro na kuimaliza inapotokea na kizuri zaidi hawa Mameja wake wamekuwa nae siku nyingi japo si sana lakini hivi karibuni Diamond na WCB wamekuwa wakiandamwa na migogoro na media tena migogoro isiyopatiwa ufumbuzi kwa makusudi na wachochea migogoro wakuu wamekuwa ni Mameneja wake wakina Babu Tale na Salam Sk...
Diamond si mkorofi ni mmoja wa watu hummble sana,pamoja na matatizo yake yote lakini si mtu anayependa migogoro na watu bali ni maneneja wake ndio si watatuzi wa migogoro bali ni wachochezi wa migogoro na media.....

Diamond alikuwa na mgogoro na EATV/EARADIO jitihada zilifanywa hasa Fella kutatua huu mgogoro japo mgogoro huu ulikuwa ni wa watangazaji wa Planet bongo na Diamond kwa kuokoteza maneno ya vichochoroni....lakini pamoja na jitihada za Fella kutatua mgogoro huu Babu Tale na Salam hawakuwa tayari na wakaenda mbali zaidi kutopeleka nyimbo pale hata za wasanii wote wa WCB sasa mgogoro huu umegeuzwa wa WCB na EATV/EARADIO.

Sasa wameingia kwenye mgogoro na Clouds baada ya Mose iyobo kuwapiga wambea lakini hili limegeuzwa kama ugomvi wa Clouds na WCB na hii imechangiwa sana na Mameneja hawa wawili Salam na Tale maana kwakweli wana midomo mirefu sana na kibri kilichopitiliza na wameligeuza jambo lile kuwa anayetafutwa ni Diamond kushushwa baada ya Clouds fm kusema wamesikitishwa na wambea wao kutandikwa na Iyobo,najua Clouds wanacho hitaji ni kuombwa radhi na walitegemea ni Diamond,Tale au Salam ndio wajitokeze kuomba msamaha kwa Clouds saa hilo jambo halijafanyika.

Lakini pamoja na hayo yote nilitegemea Mamneja wa Diamond hasa Salam Sk wakimya na si wapiga kelele au kushutumu watu ooooh wanataka kumshusha Diamond,ooh wana chuki kitu ambacho pengine si cha uhakika bali ni hisia....kwakweli Maneneja wa Diamond wamekuwa watu wa kuendekeza migogoro na kumbebesha migogoro Diamond isiyo na tija......
Sioni sababu ya Salam kuanza kutamba na kutoa povu instagram kwa jambo pengine halipo kabisa maana hata dunia inajua kuwa ni vigumu sana kumshusha Diamond kwa sasa maana walishamuacha akapanda...

Kama ni swala la Iyobo kuwapiga wambea wa Clouds hayo ni maswala yanayo muhusu Iyobo na wale wambea waliotandikwa hivyo ni vyema na ni busara kwa mameneja kujiweka pembeni na jambo hilo kwanza ni jambo la wanawake hivyo si vyema kujihusisha nalo.

Pamoja na WCB kupanga kufungua vituo vyao vya radio bado kabisa vyombo vilivyopo vinahitajika sana tena sana kwa ustawi wa wa wasanii wa WCB hivyo ni vyema sana mameneja mkafanya jitihada za kutatua migogoro kuliko kuikuza.

Wasalaam
 
Sallam ndie aliemchonganisha diamond hata na bob juniour..

Hivi ukweli mtu aliyekurekodia nyimbo bure wakati huna hela ya studio... tena studio ya gheto kwake kishkaji mnakesha mnatengeneza hit song kama mbagala leo akuchukie kweli... vinanda vimepigwa kwenye mbagala vizuri kuliko hata nyimbo zake mwenyewe bob juniour na hapo ilikuwa kishkaji tu....

mimi diamond namkubali sana ila hawa mameneja waliofata kipindi cha mafanikio ni opportunist tu.... wanaokupenda kweli ni wale mliosota nao...

babu tale kawakimbia kina tunda na madee kabanana wcb....
 
Nakubaliana na wewe ni kweli mameneja awa wawili haswa salllam ana matatizo... ila pia ujue watu tumetofautiana kubeba mambo sio wote wanaweza kuwa wanyenyekevu mpaka dakika ya mwisho.

mimi nafikiri tujipe muda tutajua ukweli, sidhani kama ishu ya moze iyobo na shilawadu ndio imewagombanisha ni kipndi kirefu toka mwaka uanze siskii nyimbo za wcb hapo clouds media.

nna uhakika kuna ishu ya maslahi maana diamond wa sasa yupo very strict inapokuja ishu ya maslahi sidhani anaweza kuharibu mahusiano yake na media kama clouds akaaribu maslahi ya wcb yote sabab ya densa wake moze iyobo.

muhimu tuombe waelewane maaana kwa level ya diamond vita yao itaumiza pande zote sio wcb pekee.
 
Watakao kuwa wanaumia ni wale vijana wa WCB........
 
Komando jide ghafla aligeuzwa komando nyoso usicheze na nguvu ya media aache ushamba enzi zile hata smartphone hazikuepo tungemjulia wapi bila media usidharau ulikotoka, vita vya panzi furaha ya kunguru haya yangu tuone vita ya mafahali hawa nani ataumia.
 
Domo soon anaanzisha media zake TV na Radio.....
 
Wewe umenena kabisaaa,media zinapenda kuabudiwa sana
 
Hakuna kurud nyuma,hao Media ni wahindi wa Pili kwa unyonyaji TZ
HAIVUMILIKI
HAIKUBALIKI
WANATAKA KUOMBWA RADHI WAO KILA SIKU
WALIANZA KWA KINA MR2
KINA JIDE
KINA RUBY
NA WENGINE HAWAJAWAH KUSEMA KAMA KINA DUDU BAYA NA HATA TID

NA UKIANGALIA MIGOGORO MINGI INAENDA KUGOTEA KWENYE MGONGANO WA KIMASLAHI TU HAKUNA JIPYA,WALISHAAMBIWA NA MADJ WA CLUB,ULAYA WASANII WANAWASAMINI ZAID CLUB KULIKO MEDIA NA HATA NYIMBO HUPELEKWA HUKOO,SASA WAO WANATAKA WAPELEKEWA AFU UWACHEKEECHEKEE DAILY

RIGHT NOW WAMEGUSA PASIPOGUSIKA,TUTAGAWANA MBAO AISEE

HUU NI ULIMWENGU WA DOT COM,RADIO/TV NI ADDITION TU
 
Mimi binafsi sijaona huo unyonyaji wa hizo media kwa WCB kiasi kwamba hawa mameneja wawili wanashindwa kukaa kimya kuyaacha au kuyamaliza.
 
Komando jide ghafla aligeuzwa komando nyoso usicheze na nguvu ya media aache ushamba enzi zile hata smartphone hazikuepo tungemjulia wapi bila media usidharau ulikotoka, vita vya panzi furaha ya kunguru haya yangu tuone vita ya mafahali hawa nani ataumia.
Ndio maana nasema tatizo liko kwa hawa mameneja wake.....
 
Sallam ndie aliemchonganisha diamond hata na bob juniour..

Hivi ukweli mtu aliyekurekodia nyimbo bure wakati huna hela ya studio... tena studio ya gheto kwake kishkaji mnakesha mnatengeneza hit song kama mbagala leo akuchukie kweli... vinanda vimepigwa kwenye mbagala vizuri kuliko hata nyimbo zake mwenyewe bob juniour na hapo ilikuwa kishkaji tu....

mimi diamond namkubali sana ila hawa mameneja waliofata kipindi cha mafanikio ni opportunist tu.... wanaokupenda kweli ni wale mliosota nao...

babu tale kawakimbia kina tunda na madee kabanana wcb....
Halafu Salam ni mropokaji sana wala hatulii hata akisikia jambo uchochoroni analibeba na analipeleka instagram....kwakweli huyu jamaa na Tale wana shida ya kibri na ujuaji mwingi sana kwakweli wanapenda migogoro sana tena sana
 
Watakao kuwa wanaumia ni wale vijana wa WCB........

Najua wataumia sana wcb lakini ata clouds sidhani kama nao hayo maumivu hayatawafikia. Kwa sasa diamond ana nguvu sidhani kama haitawaathiri pia clouds.

ngoja tuone ila bado naamini ishu imeanzia kwenye maslahi sisi tumekuja kuona matokeo tu, so hatujui mambo ya maslahi yalepelekea vipi wakafika huku.

naunga mkono hoja wa kuyamaliza haya kwa amani asiumie mtu.
 
sallamu ni jeuri na jeuri ndio iliyomfikisha hapo alipo
lazima asimamie misingi yake ili kuendelea hapo alipo

Nafikiri sallam ajtahidi kufanya kazi kuendana na mazingira kwa ufanyaji wake kazi anafaa sana kufanya kazi kimataifa sabab kule vitu vimenyooka hpa kwetu uswahili upo mpk kwenye biashara mwanangu mwanangu nyingi kwenye bizness
 
Back
Top Bottom