MBUNGE WA MBOGWE, Mhe. Nicodemas Henry Maganga Amtaka Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Kufika Mbogwe Kutatua Migogoro ya Ardhi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,033
974

MBUNGE WA MBOGWE, Mhe. Nicodemas Henry Maganga Amtaka Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Kufika Mbogwe Kutatua Migogoro ya Ardhi

"Kupitia Kamati ya Mawaziri Nane (08) wanaoshughulikia utatuzi wa migogoro ya vijiji 975, hifadhi ya Msitu wa vilima vya Mkweni haiikuwa kwenye orodha ya Misitu yenye migogoro, hivyo hapakuwa na mapendekezo yoyote ya kumegwa kwa hifadhi hii. Ilibainika kuwa hakuna uhaba wa Ardhi Katika vijiji vya jirani na Msitu bali kulikuwa na uelewa mdogo wa masuala ya uhifadhi na hasa mipaka ya Msitu huo. Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) imeelekezwa kuimarisha mipaka na kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi katika maeneo hayo. Kwa kuzingatia mazingira hayo pamoja na umuhimu wa hifadhi hii kwa jamii inayozunguka Msitu husika tunashauri wananchi wa maeneo hayo wazingatie Mipango ya matumizi bora ya Ardhi iliyoandaliwa mwaka 2021, kwa kufanya hivyo watatumia Ardhi yao kwa manufaa zaidi bila kuwepo migogoro yoyote kwa kuzingatia mahitaji yao mbalimbali" - Mhe. Dunstan Kitandula, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

"Mawaziri Nane (08) hawakufika Mbogwe lakini mgogoro wa Ardhi upo Mbogwe na wananchi wanauhitaji, Je, uko tayari kuongozana na mimi twende tukaone uhalisia ili tuwasiadie wananchi? Wilaya ya Mbogwe imekaa katikati ya mapori, upande wa Geita kuna Kijiji cha Nyashinge wananchi wakiwa wanaingia Mbogwe wanakamatwa na kupigwa na Askari wa hifadhi. Huo ni utaratibu au ni kinyume na Sheria? Naomba ufafanuzi" - Mhe. Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-05-17 at 22.24.47.mp4
    25.1 MB
Back
Top Bottom