Waziri Slaa anaonekana kuwa mbunifu baada ya kuja na clinic za kutatua kero za migogoro ya ardhi.
Jana akiwa Mbeya alionekana akitoa maamuzi ya mgogoro wa mtu anayeonekana ni Mchina ambaye kwa mujibu wa Waziri watu waliuza nyumba yake kwa TZS 80,000,000.
1. Yaliyonishangaza ni kuona mgogoro huo unatatuliwa mbele ya camera papo kwa hapo. Niliona anamsikiliza mchina na mmoja wa wapangaji na mtu aliyenunua pamoja na mwenyekiti wa s/mtaa. Huenda keshafuatilia huko nyuma kuusu huo mgogoro. Sina uhakika.
2. Mchina huyo Slaa anamtambulisha kama Muwekezaji. Hivi kuna muwekezaji mgeni ambaye kawekeza kiasi hicho kidogo cha pesa? Sheria ya uwekezaji kwa wegeni hairuhusu.
3. Kama hajakidhi vigezo na si Mtanzania, anamilikije ardhi/nyumba? na si muwekezaji?
4. Je hii haikuwa staged? Sina uhakika na siwezi kutoa conclusion.
Nia ya Waziri ni njema sana. Nashauri asichanganye na siasa za kibongo. Achague tu either kuwa mtendaji au mwanasiasa.