Jerry Silaa, migogoro ardhi inatokana na watumishi wa idara ya ardhi. As long as hujawagusa, tatizo litabaki kuwa kubwa

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,822
74,993
Unafanya kazi nzuri, nimeona Tanga katika kesi mbili ulizozimaliza. Kesi ya Tahameed moja kwa moja kuna collusion ya watendaji wa idara ya ardhi.

Wanarekodi zote, haiwezekani Tahameed akajua kuwa kiwanja fulani hakina mtu. Ni kuwa wanacollude na idara ya ardhi na kufanya uhalifu huo.

1. Wanaingia eneo la mtu kwa kutumia vishoka wanapima, na kuchora ramani za mipango miji, (vishoka hawawezi kuchora ramani zikawa part ya mipango miji), it means wanashirikiana na idara ya ardhi.

Wanapima wanapata viwanja, wanauza kupitia vishoka. Ukienda unakuta eneo lako limepangiwa matumizi bila wewe kuhusika/kushirikishwa.

Leo upo Wizara ya ardhi, kesho ukiondoka inakuwaje? jenga misingi ya kudumu kumaliza migogoro hii.
 
Una fanya kazi nzuri, nimeona Tanga katika kesi mbili ulizozimaliza. Kesi ya Tahameed moja kwa moja kuna collusion ya watendaji wa idara ya ardhi. Wana rekodi zote , haiwezekani Tahameed akajua kuwa kiwanja fulani hakina mtu. Ni kuwa wanacollude na idara ya ardhi na kufanya uhalifu huo.
1. Wanaingia eneo la mtu kwa kutumia vishoka wanapima, na kuchora ramani za mipango miji, (vishoka hawawezi kuchora ramani zikawa part ya mipango miji), it means wanashirikiana na idara ya ardhi. Wanapima wanapata viwanja, wanauza kupitia vishoka. Ukienda unakuta eneo lako limepangiwa matumizi bila wewe kuhusika/kushirikishwa.
Hili ndilo linanishangaza. Inawezekanaje ubomoe nyumba yenye hati mbili halafu aliyetoa hati haguswi. Utapeli unafanya na mtoa pesa na mtu wa ndani wa wizara.
 
Hili ndilo linanishangaza. Inawezekanaje ubomoe nyumba yenye hati mbili halafu aliyetoa hati haguswi. Utapeli unafanya na mtoa pesa na mtu wa ndani wa wizara.
Kwanza inawezekaba vipi kiwanja kimoja kiwe na title deeds mbili tofauti ambazo zote ni halali? Hili linawezekanaje?
Je, inawezekaba kweli mtoto mmoja akawa na two different biological mothers? Is it possible?
 
Jerry Silaa amepata jukwaa la kujitangaza kama bidhaa ili mbele ya safari apate wepesi kwenye ajenda yake ya siri. Kutwa kucha anahangaika kutatua migogoro ya watu wachache anaowapanga na kutatua migogoro yao mubashara.

Migogoro yote inafuata mtindo wa ukiukwaji wa sheria na kwenye hili watumishi wa wizara na Idara zake ndio wahusika wakuu katika kila mgogoro aidha kwa kushiriki moja kwa moja au kufumba macho na midomo mwanzoni mwa utata.

Utatuzi wa migogoro na kuikomesha kabisa ni kuanza na watendaji wake kwanza, awashikishe adabu hao kwanza. Hatua ya pili apitie upya sera ya ardhi. Ardhi iliporwa na wakoloni lakini hata badaa ya kupata uhuru Serikali imeendeleza uporaji kwa mtindo ule ule wa wakoloni.

Ardhi ni mali ya wananchi, kwa kuwa haikuwezekana kuwa mali ya wakoloni, haiwezi kuwa mali ya Umma chini ya uangalizi wa Rais. Ardhi ipimwe na imilikishwe kwa kila mwananchi kulingana na umiliki wa asili, kila mtu awe na kipande cha ardhi na ile inayobaki ibakie kuwa ardhi ya hifadhi ya Taifa ambamo Serikali nayo itapata kumiliki ardhi yake.
Tunatakiwa kupata uhuru upya ili tujipange upya.... Katiba Mpya haiepukiki!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Kama mfumo usiposhughulikiwa atamaliza muda wake mambo yatabaki pale pale
Yaani hata 0.01% ya matatizo hatatatua. Akimaliza leo hapa akiondoka, kesho yanazuka mawili pale pale alipoondoka. Hivi huwa hawaoni hili au wanaamua kujitoa ufahamu ili mradi waonekane wanafanya kazi? Hili suala linahitaji kuanzia kwenye kufumua katiba na mfumo mzima wa uongozi halafu urudi kwenye kubadilisha sheria, ndiyo umalizie na watu.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Mfumo wa utendaji kazi wao yafaa ubadilike. Kwann wanakaa ofisini badala ya kuwa wakiamka wawe wanaenda site kupima ardhi?

Ili kumaliza migogoro hii lazima ardhi yote ipimwe ili mtu akitaka kiwanja awe anakabidhiwa tu. Linashindikanaje hili?

Kitu kingine, mamlaka zote ziongee lugha moja. Kama eneo lina shida, basi umeme, maji, huduma za afya , shule , kituo cha polisi, n.k visipelekwe.

Inashangaza watu wamepewa kila huduma halafu anatolea mtu anasema hii ni hifadhi, hili eneo la wazi, hili eneo la shule, hii ni hifadhi ya barabara, n.k
 
Back
Top Bottom