Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,540
- 13,214
Jerry Slaa ametoa agizo hilo wakati akikabidhi Hati za viwanja katika Mtaa wa Rungwa, Kata ya Kazima Mkoani Katavi ambapo ametoa agizo la kila Mtumishi wa Ardhi nchini kuwa msuluhishi wa migogoro ambayo inajitokeza hasa kwa kuanzisha Kliniki ya Ardhi ambayo inawezesha Wananchi kupata uwazi zaidi kwa kuwafikia walipo.
Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Katavi, Chediel Mrutu amesema jumla ya wakazi wanapaswa kupewa Hati za Viwanja ni 1997 huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi, Idd Kimanta akimpongeza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutatua mgogoro huo ambao ulikuwa kikwazo kwa Wananchi na Serikali kwa jumla.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Jamila Yusuf ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ameishukuru Serikali kwa kutatua mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 10 ambapo amewasisitiza Wananchi kutoanzisha mgogoro mwingine wa ardhi katika maeneo hayo.
Mwelelwa Nkokwa na Sesilia Baltazar wameishukuru Serikali kwa kutatua mgogoro huo na kukabidhiwa Hati Miliki ambazo zitawanufaisha katika shughuli mbalimbali za kiuchimi.
Aidha, Slaa amewapiga marufuku viongozi wa vijiji na mitaa kutojihusisha na migogoro ya ardhi na badala yake wawe wasuluhishi.