Vita ya Wasafi na kampuni ya usambazaji wa Muziki 'ZIIKI MEDIA' imefika pabaya, ZIIKI wazuia utoaji wa wimbo wa Lavalava, Diamond awachana

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,095
Ziiki Media kampuni kutoka Kenya inasimamia usambazaji wa muziki kidijitali, Ziiki inashirikiana na kampuni zaidi ya 200 za ku-stream muziki online, wao wanakusambazia muziki kwenye platforms online kisha hukusanya mapato ya kwenye hizo platforms kwa niaba ya msanii.

Pichani ni boss wa ziiki "Arun Nagar"

1713559290069.png


Kupitia insta story ya Diamond leo kayaandika haya

NI MASIKITIKO KUONA KAMPUNI YA ZIKI INAZUIA WIMBO WA LAVALAVA #KIBANGO KUTOKA SIKU YA LEO NA KULAZIMISHA KUTOKA TAREH WANAYOITAKA WAO, TENA MWEZI UJAO PASIPO SABABU ZA MSINGI

TOKA KUWAKATALIA ZIKI KUNUNUA HISA ZA UMILIKI KWENYE KAMPUNI YA WASAFI LEBO NA KUAMUA KUANZISHA LEBO YAO BINAFSI, MBALI YA KUSAMBAZA KAZI ZA MUZIKI ZA WATU MBALIMBALI TU KAMA ILIVYOKUWA AWALI YANI (DISTRUBUTER), ZIKI WAMEKUA WAKIJARIBU MARA NYINGI KUTUVURUGIA UTOAJI WA NYIMBO ZA LEBO Hil YA WASAFI, KUANZIA MIMI DIAMOND HADI LEBO NZIMA YA WASAFI, ZIKI IMEKUA PIA IKIJARIBU MBINU MBALIMBAKI ZA KUIUA LEBO NA WASANII WA WASAFI KISANAA, ILA KWASABABU YA MUNGU, UWEZO WA VIPAJINA NGUVU YA MASHABIKI WAMESHINDWA KUFANIKIWA!

ZIKI WAMEAHIDI PIA, KWAMBA ENDAPO SIKU YA LEO TUTAUPANDISHA WIMBO WA LAVALAVA #KIBANGO WATAUSHUSHA KILA PLATFORS NA KUHAKIKISHA WATU HAWAUPATI POPOTE....KWA KAULI HIYO IMEFANYA TUONE KUWA MSHIRIKA WETU HUYU KIBIASHARA CHUKI YAKE ZIDI YETU IMEKUA KUBWA SANA NA INAYOHATARISHA BIASHARA YETU, HIVYO NI VYEMA SASA KWA MASHABIKI KUJUA YANAYOENDELA LAKINI PIA IMETURADHIMU KUANZA KULISHUGHURIKIA RASMI SASA JAMBO HILI KISHERIA NA SI KIRAFIKI KAMA ILIVYOKUWA MWANZO

WASAFI INAWAKUMBUSHA ZIKI KUWA WASAFILEBO INA TAALUMA NA UZOEFU WA KUTOSHA KWENYE TASNIA HiIl, INAFAHAMU TARATIBU SAHIHI ZA UTOAJI WIMBO PAMOJA NA MARKETING... WASAFI NDIO MNUFAIKA AMA MUHANGA MKUBWA ENDAPO KAMA KAZI ZAKE HAZITIENDA INAVYOPASWA, HIVYO INAPOAMUA KUCHIA WIMBO TAREH FULANI INAFAHAMU NINI INACHOFANYA, NA NDIOMAANA SIKU ZOTE IMEKUA IKITOA NYIMBO ZENYE MAPOKEZINA MAKUBWA LICHA VIPINGAMIZI VINGI ILIYOKUA IKIWEKEWA NA ZIKI KWENYE UTOAJI WA NYIMBO ZAKE!!

MSIJALI MASHABIKI ZETU #KIBANGO LAVALAVA x DIAMOND PLATNUMZ TUNAITOA LEO NA WAKIITOA KWA PLATFORMS TUTAWASAMBAZIA ATA KWA WHATSAPP!! OMBI LANGU, SUPPORT KUBWA ILI WAJUE KUWA MASHABIKI WANATAKA NGOMA SIO PROPAGANDA!!! WAACHIE NGOMA ZITOKE!!!
 
Hii ni sawa na kukemea shetani kwa jina la Yesu huku umeshika panga na kumwambia utamkata kama haonyeshi kukusikiliza.

Ziki hawana hisa WCB,mamlaka ya kuzuia nyimbo wanatoa wapi?? Ni distributor.

Distributor anatoa wapi mamlaka ya kuzuia wimbo wakati ni mlanguzi tu wa kazi za music??mlio wa mbwa.

Kuna tetesi nilisikia hawa jamaa walimpa jamaa mapesa mengi,lakini kwa mabadilishano ya vingi ikiwamo haki zake za kazi mitandaoni yeye binafsi sio lebel nzima.sasa mbinu ni kufanya featuring,jamaa nao naona wamekuwa smart.
KUMEKUCHA.
 
Back
Top Bottom