Binti atoa penzi siku 3 bila ridhaa yake, na kesi kashindwa

Binti (Miaka 19) yupo kwa Basi, anatoka zake Dar kwenda Uyulo-Mbeya kumsalimu Shangazi yake, anawasiliana nae kwa Simu akiwa safari, lakini anafika Iringa Simu inakata Chaji.

Binti anamuomba Simu Jamaa aliyekaa pembeni yake aitwaye MAPINDUZI NGALLA, lakini anapiga Simu Shangazi hapatikani. Jamaa anamchombeza Binti kwani unaenda wapi?
Binti anajibu Uyole-Mbeya,
Jamaa anamwambia mmh! pale Uyole usiku kuna wauaji, twende ukalale kwangu Mbalali kisha kesho utamalizia safari yako, Binti anamuuliza kwako unakaa na Familia?
Jamaa anajibu ndio.
👆🏿
Basi Jamaa anamchukua Binti anaenda nae kwake kijiji cha URUNDA- Mbarali, , kumbe Jamaa anakaa peke yake, wanalala chumba tofauti, lakini usiku Jamaa anaenda chumbani kwa Binti, anadai penzi, Binti anakataa lakini Jamaa ana force kingi - anambaka Binti, kesho inafika Jamaa anamfungia Binti ndani, usiku anambaka tena, kesho yake Jamaa anasahau kufunga mlango Binti anafanikiwa kutoka ndani, baadae Jamaa anakamatwa kwa ubakaji.
👆🏿
Jamaa ameshinda kesi. Unajua kwanini? Kifungu -130(1)(2)(b)- ambacho alishtakiwa nacho kinaelezea ubakaji ambao Mwanamke anakubali kufanya mapenzi lakini kukubali kwake kunatokana na kutishiwa kuuliwa, kuumizwa... lakini hii kesi ushahidi wa Binti ulikuwa kwamba alilazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa (consent) yake, hii kitu inaangukia kifungu kingine tofauti -130(1)(2)(a) cha Kanuni ya Adhabu.
Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji MASHAKA imemuachia jamaa aliyekuwa amefungwa miaka 30 na mahakama kuu.
Jaji :- Mashaka
Wakili wa Serikali 1 .Edgar Luoga.
2. Devise Msanga.

Nani alaumiwe?
  1. shangazi aliyepotea hewani.
  2. Mapinduzi[mbakaji]?
  3. Binti[Tunda]?
  4. Mawakili wa Serikali waliokosea vifungu vya sheria?
  5. Mungu aliyeshindwa kumfanya jama adindishe?
  6. Serikali inayosajili mawakili chini ya viwango?
Hakika haki ya kweli ipo Mbinguni🤣
 
Binti anafahamiana na kijana

Hakufika kwa shangazi moja kwa moja alifika kwa kijana

Walikuwa na ugomvi au ulijitokeza kipindi binti akiwa kwa kijana

Binti akamsingizia

Hata kama walifahamiana kwenye basi, itakuwa binti alidanganywa kwa kuahidiwa malipo, asingekubali kwa namna yeyote nyingine.

Ugomvi wa malipo ukapelekea binti kushtaki
Huu ndio ukweli, binti anakuwaga ameridhia ila anasingizia kubakwa baada ya kutopata alichotarajia baada ya mapenzi, nini kifanyike?
 
Binti anafahamiana na kijana

Hakufika kwa shangazi moja kwa moja alifika kwa kijana

Walikuwa na ugomvi au ulijitokeza kipindi binti akiwa kwa kijana

Binti akamsingizia

Hata kama walifahamiana kwenye basi, itakuwa binti alidanganywa kwa kuahidiwa malipo, asingekubali kwa namna yeyote nyingine.

Ugomvi wa malipo ukapelekea binti kushtaki
ukikua utaqcha
 
Wakulaumiwa ni State Attorney kwa ku cite provision ambayo sio sahihi na haiendani na ushahidi,yani kesi imesikilizwa kuanzia mahakama ya wilaya hadi hukumu inatoka hawakugundua hilo na mtego huo huo Jaji wa mahakama kuu hakuona hayo makosa kwenye rufaa hadi wazee wa juu ndio wameona.
 
Binti akiwa kakosa msaada safarini aombe msaada kwa Konda wa basi au Dereva wa Basi. Kama keshashuka Basi aombe msaada kwa Mwanamke mwenziye kwanza.
Ili ampeleke Kituo cha Polisi au Serikali ya Mtaa au Kituo cha msaada kama Kanisani, Msikitini Nk.
 
Kuna ushahidi wowote? Tuanzie hapo

Mkuu ushahidi upo wa kutosha kabisa kwenye hiyo kesi,tatizo ni kwamba huo ushahidi uliokuwepo na ambao ulitolewa na muhanga mwenyewe wa hilo tukio haukuendana na kifungu cha sheria ambacho mtuhumiwa alishitakiwa nacho,ushahidi uliotolewa unaangukia kifungu cha 130 (1) (2) (a) lakini kwenye hakti ya mashtaka kifungu kinasomeka 130 (1) (2) (b) ya Kanuni za Adhabu,kwa hiyo maelezo yalipo kwenye hati ya mashtaka hayaendani na ushahidi uliotolewa. Kwa hiyo kulikuwa na makosa kwenye uandaaji wa hati ya Mashtaka.
 
Mara ya kwanza kufika Mbeya nilikuwa nina miaka 17, nilifika 7 usiku. Sikuwa na mwenyeji nililala Lodge.
Nilikuwa naenda kidato cha tano.

Bure ni gharama. Yeye hakuwa na pesa za Guest si angelala Stendi kama abiria wengine?
M
Akalale guest apoteze pesa wakati msamaria mwema ameshajitokeza ana nyumba hapo maeneo ya Mbarali na anaishi na familia yake so hakuna risk yoyote ya kupigwa tukio la kingono!!!
Cha msingi hela ya dharura ni muhimu sana aisee.... Au angelala tu stendi kama abiria wengine as you said.
 
Wakulaumiwa ni State Attorney kwa ku cite provision ambayo sio sahihi na haiendani na ushahidi,yani kesi imesikilizwa kuanzia mahakama ya wilaya hadi hukumu inatoka hawakugundua hilo na mtego huo huo Jaji wa mahakama kuu hakuona hayo makosa kwenye rufaa hadi wazee wa juu ndio wameona.
Kama kweli report ya Dr imethibisha kua kweli mbegu za mbakaji zimekutwa ndani ya Binti,basi Mahakama ya rufaa itakua imekosea sana kwa kupuuza report ya mtaalamu na kukimbilia kwenye mapungufu ya State Attorney ili kuitupa kesi na kumuachia Mbakaji!!
 
Nyumba za vijijini zipo mbali mbali.
Jamaa alikwenda chumbani kwake usiku saa saba akaanza kuomba mchezo, kunyimwa akamvua chupi maana dada alikuwa maevaa kanga moja pekee.
Jamaa kiona tunda akapenya.
Hivi unapajua uyole au unaandika tu?
 
Kama kweli report ya Dr imethibisha kua kweli mbegu za mbakaji zimekutwa ndani ya Binti,basi Mahakama ya rufaa itakua imekosea sana kwa kupuuza report ya mtaalamu na kukimbilia kwenye mapungufu ya State Attorney ili kuitupa kesi na kumuachia Mbakaji!!
Kwamba kukuta mbegu ndo kithibitisho kikubwa cha mwanamke kubakwa? Vipi nikielewana na binti baada ya muda akaenda mahakamani baada ya kuhitilafiana,napo ni ubakaji kisa wamekuta mbegu?
 
Mkuu ushahidi upo wa kutosha kabisa kwenye hiyo kesi,tatizo ni kwamba huo ushahidi uliokuwepo na ambao ulitolewa na muhanga mwenyewe wa hilo tukio haukuendana na kifungu cha sheria ambacho mtuhumiwa alishitakiwa nacho,ushahidi uliotolewa unaangukia kifungu cha 130 (1) (2) (a) lakini kwenye hakti ya mashtaka kifungu kinasomeka 130 (1) (2) (b) ya Kanuni za Adhabu,kwa hiyo maelezo yalipo kwenye hati ya mashtaka hayaendani na ushahidi uliotolewa. Kwa hiyo kulikuwa na makosa kwenye uandaaji wa hati ya Mashtaka.
Ushahidi upi, wa video?
 
Hili la kuombwa simu kwenye bus lishakuwa changamoto, mie nilikapa simu kushuka kakaniganda eti simu ya shangazi yake haipatikani, nikakapeleka kituo cha polisi kakatoka baru
 
Akalale guest apoteze pesa wakati msamaria mwema ameshajitokeza ana nyumba hapo maeneo ya Mbarali na anaishi na familia yake so hakuna risk yoyote ya kupigwa tukio la kingono!!!
Cha msingi hela ya dharura ni muhimu sana aisee.... Au angelala tu stendi kama abiria wengine as you said.

Kuna Watu wanacheza na maisha
 
Hana hela ya kulipia gesti.

Kwa hiyo anaona abiria wanaolala Stendi ni wajinga.
Binti ameonyesha tabia za kimalaya na asiyejali maisha yake.

Unamuamini vipi mtu uliyekutana naye kwenye Basi tena kwa ujinga unaamua kwenda kabisa kulala kwake. Akikutoa kafara au kuchukua viungo vyako?

Hiyo ya kubakwa ni kosa kisheria. Lakini haina uthibitisho.
Binti naye kafanya kosa la kiusalama
 
Back
Top Bottom