Nimesoma habari huko mtandaoni nimepata mtatiziko kidogo baada ya mwandishi kuandika watu wenye group B msile kuku, na wakati mimi kuku ndio moja ya kitoweo changu pendwa sana.
Msaada hapo wa kuhakiki taarifa hii iwapo ni kweli kuku si salama kwa wenye damu group B
Kuna chama kilishaanza kampeni isiyo rasmi ya uchaguzi Mkuu 2025, huhitaji kuwaza kujua kuwa hii ni kampeni ya kum-"brand" mgombea wao na kujibrand wao wenyewe ili majina yao yatajwe kila siku na watu lakini pia wakumbukwe kuwa wapo kama walisahaulika.
Kubwa zaidi ni kumuuza kwa lazima mgombea...
Umewahi kukutana na daladala imejaza abiria halafu upande mmoja unakuwa umeelewa utafikiri inataka kuanguka?
Sijui nini kinasababisha hali hiyo na sina hakika iwapo hiyo ni salama kwa abiria, maana huwa nawaza likiyumba kidogo tu huenda likabinuka na kusababisha ajali.
Kwanini magri haya...
Video hii inaonesha mtu akichapwa fimbo huku akiambiwa "Hapa si bara" sababu za kuchapwa eti ni kwa kuwa amekula mchana chakula wakati wa Ramadhani.
Hivi Zanzibar, mnawachukuliaje watu wa bara? Ni watu baki au ni watu wasio na haki ya kukaa Zanzibar? Maana hapo ni ubaguzi wa wazi, kupanda mbegu...
Ni kubwa sana kiumbo, ikiwa kwenye hadhira,
Ni Mamba kama wa Mombo, Sema ye hana madhara,
Yakichambuliwa mambo, yatakutia hasira,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?
Hukaa kimya majini, hutoka mwingine mwaka.
Huletwa vingi vitini, kusoma walo potoka,
Vinasomwa kwa makini, imara bila...
Umejengwa utamaduni wa ajabu kwa kutoa Sifa kwa viongozi wa kisiasa wanaposimamia utekelezwaji wa miradi ya kitaifa, na kusahaulika Mwananchi ambaye ndiye aliyemwaga jasho kutafuta pesa na kuipa kodi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Sifa hizo kwa sasa zimeenda mbali zaidi kusifia hata pale...
Ni mchezo mchafu wa wanaotoza hela kwa wanaotaka kuingia Magufuli stendi, ni mara kadhaa kila nikifika pale ukiwa na sh. 500 au 1000 nk watakwambia hawana shilini 100 au 200.
Mara nyingi wanafaya mchezo huo wakati kukiwa na msongamano wa foleni wanakwambia uchukue chenji nusu au wakurudishie...
Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza...
Leo nilifika kituo cha afya Kimara baada ya ndugu yangu kuniita nikalipie gharama ili mtoto wake apatiwe matibabu baada ya kuanguka na kuumia mguu.
Picha linaanza kuingia kwa daktari, mama wa mtoto anaeleza mwanaye kaumia baada ya kuaguka wakati anacheza, dk bila hata kumgusa wala kumwangalia...
Majuto ni mjukuu
Jitajidi kufanya maamuzi sahihi katika wakati sahihi ili kuepuka kujuta baadaye.
Kumbuka siku zote ningejua huja mwisho wa safari.
Je, umewahi kufanya jambo gani lililokufanya ujutie maamuzi yako?
Wakuu habari,
Hii habari ya Asec Mimosas kuomba kutumia uwanja wa Mkapa kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya Simba kwenye ligi ya mabingwa Afrika ina ukweli wowote?
Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya.
Mjadala umechagizwa na kauli ya...
Habari, nawasalimi kwa jina la muungano......
Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kumkataa mtoto kumpokea ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na mtoto ni mbali sana...
Hili sakata la dola linanivuruga sana, ukifuatia kulikuwa na taarifa mtandaoni kuwa Tanzania kuna uhaba wa dola Za kimarekani.
Sasa naona tena kuna taarifa inazagaa mtandaoni kuwa BoT akiba hiyo imekauka kabisa, na si dola pekee sasa hadi shilingi ya Tanzania nayo imekauka.
Kuna ukweli hapa...
Habari.
Mimi ni Safari Guide, nina Kero kubwa sana kuhusu Traffic Police wa Arusha.
Wamekuwa wakisimamisha magari ya watalii kila mahali hawajali kama umebeba wageni au la, waanza kuomba leseni na kukagua gari wanachukua hadi dakika 10 wamekusimamisha bila kujali umetoka wapi na unaratiba gani...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.