UZUSHI Watu wenye Damu kundi B hawatakiwi kula kuku

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimesoma habari huko mtandaoni nimepata mtatiziko kidogo baada ya mwandishi kuandika watu wenye group B msile kuku, na wakati mimi kuku ndio moja ya kitoweo changu pendwa sana.

Msaada hapo wa kuhakiki taarifa hii iwapo ni kweli kuku si salama kwa wenye damu group B

IMG_20240404_151617_723.jpg
 
Tunachokijua
Makundi ya damu ni uainishaji wa damu kwa kuzingatia kuwepo au kutokuwepo kwa dutu za antijeni za kurithiwa kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu (RBCs).

Antijeni hizo zinaweza kuwa protini, kabohaidreti, glikoprotini au glikolipidi, kutegemeana na mfumo wa aina ya damu.

Kuna makundi makuu manne ya damu ambayo ni A, B, AB, O na kila kundi lina aina yake ya razazi ambazo ni (+) na (-).
1712219889216-jpeg.2953585
Je, ni kweli watu wenye kundi "B" hawatakiwi kula kuku?

Kumekuwepo na madai kuwa watu wenye damu kundi B wasile baadhi ya vyakula ikiwemo Kuku huku wakielezwa kuwa chakula hicho si salama kwa afya zao.

Ukweli ni kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaothibitisha kuwa kuku si salama kwa watu wenye kundi B la damu, watu wenye kundi hilo la damu wanaruhusiwa kula vyakula yote kama yalivyo makundi mengine.

Madai hayo yanakanushwa zaidi na Wizara ya afya, kupitia mtandao wa X imekanusha kuwa watu wenye kundi B la damu hawana sababu yoyote ya kuepuka kula kuku, kanusho hilo limefafanua kuwa si kweli kuwa watu wenye kundi B la damu hawaruhusiwi kula kuku kwani hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaothibitisha madai hayo.

GKTdK6CXQAAuZG_
Kufuatia kanusho la Wizara ya Afya, Jamiicheck imethibisha kuwa taarifa zinazodai watu wenye kundi B la damu wasile kuku ni taarifa za Uzushi.
Taaluma ya afya ni pana sana na wadau wanafanya tafiti mbalimbali juu ya mwili wa binadamu ngoja tusubiri wataalam wa afya wanamajibu gani.
 
Sasa nafuga kuku wa nini..... nishaandaa pilau langu la miguu ya kuku na vichwa (don't mind ndio vilivyobaki after pasaka) halafu unaniambie nisile pilau la kuku kweli? Mzaha si mzaha
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom