Sasa ni dhahiri kuna chama kilishaanza kampeni isiyo rasmi ya uchaguzi Mkuu 2025

Mawele

Member
Jul 25, 2023
30
117
Kuna chama kilishaanza kampeni isiyo rasmi ya uchaguzi Mkuu 2025, huhitaji kuwaza kujua kuwa hii ni kampeni ya kum-"brand" mgombea wao na kujibrand wao wenyewe ili majina yao yatajwe kila siku na watu lakini pia wakumbukwe kuwa wapo kama walisahaulika.

Kubwa zaidi ni kumuuza kwa lazima mgombea wao namba moja kwani hulazimisha kumtaja na kumuhusisha na kila kitu kinachoendelea nchini ili mradi tu asikke na watu wajenge imani kuwa yeye bora.

Wakati huu chama hicho utawaona watu wake wamegawana makanisa wakihubiri, kupiga masimu makanisani, kutoa sadaka kubwa na michango na misaada kedekede, bila kusahahu utawaona wakifuturisha na kutoa michango kwenye misikiti au ya ujenzi wa misikiti.

Si ajabu ushaanza kuwaona au kusikia wametembelea majimbo yao, wengine wakipanda dalddala na kufuturu kwa mama Ntilie huku wengine ati wakipanda bodaboda, ni hiko chama kiko kwenye kampeni huku kikiaminisha Umma kuwa kampeni za uchaguzi bado hazijaanza na kwamba kuna sheria inazuia kuanza mapema.

Chama hicho sasa kila tukio wataweka picha ya mgombea wao, hata misibani watamsifia mgombea wao wanaweza kukushangaza kwani hawashindwi kumsifu mgombea wao kwa kufanikisha marehemu kulala pema peponi ilimradi atajwe hata pasipohusika.

Kama kampeni zimefunguliwa kwa nini vyama vingine bado wamesinzia wanasubiri kuamka kuvuta shuka asubuhi kumekucha, wagombea wao hata hawajulikani, wala hawajihusishi na uchaguzi kwa wakati huu. Ni sahihi kwao kwani wanafata kanuni ya uchaguzi inavotaka.

Sina hakika iwapo kampeni bado kufunguliwa maana sina hakika kwani sijaona popote chama kile kikimewa kwa kampeni za mapema ndio maana nadiriki kusema sina hakika.
 
Na,usisahau,hudanganya wajinga kwamba kina wanachama zaidi ya milioni nyingi mnooo!Subiri uchaguzi ufike sasa!Ni wezi wa kura balaa kwa kuwatumia watumishi wa umma wa kada za chini ambao mishahara yao tu ni huzuni.
 
Mimi nimemiss zile kampeni za Nape na Kinana ambazo fisi walitumika kama vivutio, wakajumuika kwenye ujenzi na wananchi huku wakila nao wali maharage.

Hakika ilikuwa burudani ya kukata na shoka!
 
Mimi nimemiss zile kampeni za Nape na Kinana ambazo fisi walitumika kama vivutio, wakajumuika kwenye ujenzi na wananchi huku wakila nao wali maharage.

Hakika ilikuwa burudani ya kukata na shoka!
Mimi nime miss matrekra,mikokoteni & Punda wa Bashite
 
Mimi nimemiss zile kampeni za Nape na Kinana ambazo fisi walitumika kama vivutio, wakajumuika kwenye ujenzi na wananchi huku wakila nao wali maharage.

Hakika ilikuwa burudani ya kukata na shoka!
Kama hizi hapa
JamiiForums2012770947.jpg
 
Kuna chama kilishaanza kampeni isiyo rasmi ya uchaguzi Mkuu 2025, huhitaji kuwaza kujua kuwa hii ni kampeni ya kum-"brand" mgombea wao na kujibrand wao wenyewe ili majina yao yatajwe kila siku na watu lakini pia wakumbukwe kuwa wapo kama walisahaulika.

Kubwa zaidi ni kumuuza kwa lazima mgombea wao namba moja kwani hulazimisha kumtaja na kumuhusisha na kila kitu kinachoendelea nchini ili mradi tu asikke na watu wajenge imani kuwa yeye bora.
Ukata wa fedha umefanya vyama kua dahifu na vinyonge sana. Njaa na utegemezi wa misaada ya nje na ndani ya wadau sio kitu kizuri aisee dah....
 
Back
Top Bottom