YAJUE YA TANGA MJINI NA MAAJABU YAKE

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,966
15,502
1 - Saa 3 usiku hakuna daladala barabarani.
2-Saa 4 usiku huoni watu nje na usiulize kwanini. Jiongeze bro!
3-Ugali wa 1500 unapata mboga 7, usisahau uono (dagaa mchele) buree.
4- Ndio jiji lenye baiskeli za kukodi kama bodaboda na kiti chenye sponji.
5- Disco wanapiga taarabu.
6- Hakuna kelele wala vurugu ni kimyaaa hadi raha.
7 - Kijana akishakuwa na uhakika wa kula na kulala anaoa hata wake watatu kwa mpigo.
8- Binti wa Kitanga mwambie apande pikipiki utalipa. Akifika mnunulie chips yai na soda. Kwisha!
9 - Ndio jiji lenye soda zake. 'Healtho' au 'Anjari'. Huko Bakhresa na Mo hawasikiki.
10 - Ukiishi na watu vizuri kuoa na kuolewa hupati shida wao ndo wanamaliza kazi.
11-Raskazone, Donge,Tanga Beach ndio ushuani kwa mafogo.
12- Maji ya kunywa siyo ya kununua dukani, ya bomba tu yanakata kiu, safi hadi raha.
13- Kwa mabinti uwe na pumzi, ukijiroga bro utatolewa jasho ujute.
14 - Kuna traffic light mbili tu pale Toyota na Mombo Hospitali.
15- Machimbo yetu yaleee ni nenda Sabasaba na Kwa Chichi. Hii ni code kwa wakware.
16 - Daladala ipo radhi kumsubiri mtu hata ikibidi kupiga rivasi kumfuata alipo.
17- Ni jiji lililopangika vizuri uswahilini, mjini mpaka ushuani.
18 - Kule madem wanaenda bar au club na madera na ushungi kichwani.
19 - Tanga kila binti anajua mapenzi na wanaheshimu wanaume.
20 - Mabinti wa Tanga wanapenda ndoa na wanajua kulea waume.

Ongeza nyingine ✍️
 
 
Sio mbaya nimeitoa telegram huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom