Waziri Ummy ataadharisha unywaji wa pombe uliokithiri unavyochangia ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza nchini

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
124
203
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa unywaji wa pombe nchini unazidi kukithiri licha wastani wa wanaokunywa kupungua kutoka 26% mpaka 20%, hali ambayo amedai kuwa imekuwa ikichangia angezoko la magonjwa yasiyoambukiza.

Akizungumza leo April 23, 2024 alipokuwa akifungua mkutano wa kujadili magonjwa yasiyoambukiza barani Afrika PEN-Plus ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani WHO kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, amesema kuwa utumiaji wa pombe unapokithiri muhisika anakuwa katika mazingira ya kupata magonjwa yasiyoambukiza.

"Tanzania tuna ongezeko la kiwango kikubwa cha unywaji wa Pombe wakati tumepunguza watu wanaokunywa pombe. Kitakwimu kwa tulikuwa na watu wanaokunywa pombe kwa wastani wa 26% tumepungunza mpaka 20%.

Ameongeza "Lakini kiwango cha pombe kimeongezeka kutoka wa wastani wa lita 9.1 mwaka 2016 mpaka wastani wa lita 10.4 kwa mwaka kwahiyo kiwango cha watu kimepungua lakini wanakunywa sana"

Pia kufuatia madai kwamba ana taarifa kuhusu uwepo wa pombe zisizo kidhi ubora, amesema atashirikiana na TBS kuona namna ya kufuatilia madai ya uwepo wa pombe hizo ambazo zinaingizwa zinadaiwa kuingizwa sokoni, hali ambayo anadai kuwa inaweza kuchochea magonjwa yasiyo ya kuambukiza

"Juzi kuna kiwanda cha pombe waliniletea malalamiko kwamba sisi tunazalisha pombe yenye ubora tena wameniomba kwamba watanipa ushahidi wa kiasi gani cha ambazo hazina ubora kinadhalishwa na kinaingizwa sokoni hili kuwaweka watanzania katika hatari ya magonjwa haya (magonjwa yasiyo ya kuambukiza)."

"Ni eneo ambalo nalichukua tutaenda kulifanyia kazi na watu wa TBS (Shirika la viwango nchini) na sheria yetu haiko vizuri sana kwamba nani anatakiwa kuthibiti masuala ya pombe" amesema Waziri Ummy

Lakini amesema kuwa Tanzania kama Nchi nyingine za Afrika inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.

"Tunaona ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa yasiyoambukiza hususani shinikizo la juu la damu, kisukari, Saratani lakini pia Selimundu kama nchi tutaendela kuwekeza katika mikakati ya kinga na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata elimu na huduma dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza" amesema Waziri Ummy.

Aidha Mkurugenzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Afrika wa WHO, Dr.Benido Impouma akizungumzia mkutano huo unaofanyika kwa siku tatu nchini Tanzania, amesema kuwa unawakutanisha wadau mbalimbali hususani kutokea bara la Afrika ambao wanapata fursa ya kubadilishana ujuzi na udhoefu kuhusu mkakati wa kukabiliana na changamoto hiyo.

Itakumbukwa Ripoti ya WHO inaonyesha kwamba magonjwa hayo yasioambukiza, (NCD), yanasabisha asilimia 74 ya vifo kote ulimwenguni na nyingi ya vifo vinatokea katika nchi zinazoendelea, kutokana na wagonjwa kutofikia huduma za kinga na za kudhibiti magonjwa hayo.

Ripoti hiyo iliyotolewa wazi 2022 na kupewa jina la "Nambari zisizojulikana" inasema Magonjwa ya Moyo, saratani, kisukari na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa kupumua yanasababisha vifo vingi duniani kuliko magonjwa yasioambukiza.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofadhiliwa na taasisi ya Bloomberg' unataja maeneo muhimu ya kupatiwa msisitizo ikiwemo kudhibiti matumizi ya tumbaku, uchafuzi wa hewa, milo isiyo na lishe, kufanya mazoezi na kuboresha usalama barabarani, huku pia unywaji wa pombe uliokithiri ikitajwa kati ya vyanzo vinavyopelekea magonjwa hayo.

Inaelezwa kuwa baada ya kuona changamoto hiyo WHO ilianzisha mradi wa PEN-Plus kwa Afrika ambao unalenga kusaidia jamii za kiafrika kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kuhusu magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ili kuongeza uelewa kwa jamii ili iweze kuchukua hatua.

FB_IMG_1713903766009.jpg
FB_IMG_1713903760807.jpg
FB_IMG_1713903754074.jpg
 
Back
Top Bottom