Takwimu: Mtu mmoja anakunywa pombe lita 10.4

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
216
478
WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema takwimu zinaonesha kuwa wanywaji wa pombe wameongezeka nchini hali inayofanya kuanza uhamasishaji wa kupunguza unywaji wa pombe.

Takwimu alizotoa zinaonesha kuwa mtu mmoja anakunywa lita 10.4 kwa mwaka ambapo awali mtu mmoja alikuwa anakunywa lita 9.1.

Akizungumza katika Mkutano wa Kwanza wa Mipango Mikakati wa Kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza Afrika (ICPPA) Ummy amesema takwimu za mwaka 2016 watu waliokuwa wanakunywa pombe walikuwa asilimia 26 na walipunguza hadi asilimia 20 lakini kiwango cha unywaji pombe kimeongezeka kwa sasa.

“Tunahamasisha kupunguza unywaji wa pombe ulipitiliza tumeongeza kiwango mtu mmoja anakunywa lita 10.4 kwa mwaka hii ni hatari kwa afya,”amesisitiza ummy

Ummy amesema kuwa Tanzania kama nchi zingine inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti na wanaona ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa yasiyoambukiza husani shinizo la juu la damu, kisukari, masuala ya afya ya akili, selimundu na mengine ikiwemo ajali.

“Tutaendelea kuwekeza katika mikakati ya kinga na kuhakikisha wananchi wanapata huduma na kwenye kinga tutajikita katika kutoa elimu ya afya kwa wananchi kujikinga na tumekuwa na wataalamu kama Prof Janabi wamekuwa wakihamasisha kuzingatia ulaji unaofaa.

Aidha amewasisitiza vijana kufanya mazeozi na wasisubiri wapate magonjwa hayo ndio waanze kufanya mazoezi.

Chanzo: Habari Leo
 
Mbona chache sana maana kwa mnywaji wa kawaida kwa siku anakunywa tano hadi kumi ambazo ni lita karibis mbili hadi tatu sasa kwa wiki tu huyu anapiga zaidi ya kumi
 
Aliyezuia viroba na kuleta huu utitiri wa mapombe ya plastic sijui aliwaza Nini, aisee Hawa jamaa sijui wanatoa leseni kwa kuzingatia Nini, hivi vipombe vya plastic vishawamaliza vijana
Vijana, wanakwambia Sungura hapinwgwi, vinauzwa buku mbili, ukitaka nusu wanawapimia cha buku,

Serikali ifanye jambo, vijana wanaangamia,
 
Aliyezuia viroba na kuleta huu utitiri wa mapombe ya plastic sijui aliwaza Nini, aisee Hawa jamaa sijui wanatoa leseni kwa kuzingatia Nini, hivi vipombe vya plastic vishawamaliza vijana
Bora viroba TBL na kiroba original walikua wanazingatia viwango, hata mapombe ya vikopo vinatengenezwa vichochoroni bila kuzingatia viwango, vilianzia Uganda vijana wakawa wanafakamia ili wazeeke nataka waanze kulipwa pension na serikali now vimehamia tz.
 
WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema takwimu zinaonesha kuwa wanywaji wa pombe wameongezeka nchini hali inayofanya kuanza uhamasishaji wa kupunguza unywaji wa pombe...
Lt. 10 kwa mwaka ni hatari!

Wakati dr. Janabi anashauri mtu mmoja kupata bia mbili kwa siku ambayo ni lt. 1 (Balimi na Safari .. 0.5 lt)

ie: 1x365 /10(crete) =lt 365.5 ama crete 36 na nusu kwa mwaka.

Tena huo ni unywaji kwa afya.

Sasa hizo crete 2 kwa mwaka halafu ni hatari kwa afya kwa nini wasiifute pombe?

Jamani au hizi ni takwimu za kupika Waziri kabambikwa?

Mi hainiingii akilini ati!
 
Back
Top Bottom