Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,678
- 698,787
Isichukuliwe kama dhihaka! Isichukuliwe kama maskhara na furahisha genge! Bali ikupe fikra fikirishi ya huko tunakoelekea na dhana nzima ya kubana matumizi.
Akiripoti kutoka Dodoma mwandishi wa kituo cha WAPO RADIO, amesema wananchi wa Dodoma leo wamesifu kitendo cha Waziri Mkuu cha kutembea kwa miguu UMBALI WA MITA 200 kutoka makazi yake-Ikulu ndogo ya Dodoma hadi ofisini kwake (zingatia mita 200)akiwa na walinzi wachache.
Kitendo hicho kimetajwa kama kitendo cha aina yake chenye UADILIFU kilichookoa MAMILIONI YA PESA ambayo yangetumika kwenye msafara wa magari yasiyopungua sita.
Tuupinge kwa nguvu zote huu upuuzi, mwendo wa mita 200 katika uhalisia wake mtu anaweza kupanda gari na msafara?
Je, kama Leo imeonekana ni ajabu ina maana siku zote ndivyo ilivyo?
Je, kutembea mita 200 ni kubana matumizi?
Ni habari za namna gani hizi jamii inapewa?
Ina maana Dodoma leo kuanzia asubuhi hakukuwa na habari nyingine zaidi ya hii?
Hii breaking news imeniacha na maswali mengi.