Hayati William Kusila, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa zamani aliyekimbia furushi la fedha ofisini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,433
8,251
Mbunge wa Bahi (CCM), Keneth Nollo ametoboa siri ya uzalendo wa Hayati William Kusila kwamba aliwahi kukimbia furushi la fedha zilizopelekwa ofisini kwake ili apokee hongo na kutoa upendeleo.

Nollo ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 25, 2022 wakati akitoa salamu za rambirambi mbele ya mwili wa Kusila wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Kuu la Anglikana Dodoma.

Mbunge huyo amewaambia waombolezaji uzalendo aliokuwa nao mtangulizi wake katika jimbo hilo ulikuwa umepitiliza ambao hata yeye angetamani kuufikia lakini anaona viatu vyake ni vikubwa.

Kusila alifariki dunia Agost 21, 2022 jijini Dar es Salaam alikokimbizwa kwa matibabu na mwili wake utazikwa shambani kwake kijiji cha Mtitaa kesho Ijumaa Ijumaa Agost 26, 2022.

Wakati wa uhai wake, Kusila aliwahi kuwa Mbunge wa Bahi kwa miaka 20, waziri kwa nyakati tofauti katika wizara za uchukuzi na kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na alimaliza kwa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo.

“Huyu mimi ni kaka yangu kwa ukoo, hata kabla sijawa mbunge aliwahi kuniambia kuna wakati alipelekewa furushi la mamilioni ya fedha ili kusudi afanye maamuzi ambayo hayakuwa na maslahi kwa nchi yake lakini aliamua kuikimbia ofisini na kuwaacha waliopeleka fedha hizo wasiwe na majibu huu ni uzalendo wa hali ya juu sana,” amesema Nollo.

Mwanasiasa huyo amesema kazi alizozifanya Kusila akiwa mbunge bado zinaendelea kumtesa jimboni kwani kila akifanya jambo zuri wananchi wanamlinganisha na kusema amekaribia kwa Mzee Kusila ingawa hajafikia,” amesema.

Hata hivyo, amewaomba wananchi kuwa watulivu hasa wapiga kura kwa kuwa viatu alivyoviacha mzee huyo ni vikubwa kwa hiyo kuvichukua moja kwa moja inahitaji ujasiri wa kutosha lakini atajitahidi kutembea navyo.

MWANANCHI
 
Binafsi namfahamu W. Kusila, maana ni jirani na rafiki.

Itoshe kuandika kuwa huyu mtu hakuwa kama wana magamba tuwajuavyo.

R.I.P W. Kusila.
 
Back
Top Bottom