Waziri Mkuu aokoa mamilioni, atembea kwa miguu kwenda ofisini

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,641
698,017
Isichukuliwe kama dhihaka! Isichukuliwe kama maskhara na furahisha genge! Bali ikupe fikra fikirishi ya huko tunakoelekea na dhana nzima ya kubana matumizi.

Akiripoti kutoka Dodoma mwandishi wa kituo cha WAPO RADIO, amesema wananchi wa Dodoma leo wamesifu kitendo cha Waziri Mkuu cha kutembea kwa miguu UMBALI WA MITA 200 kutoka makazi yake-Ikulu ndogo ya Dodoma hadi ofisini kwake (zingatia mita 200)akiwa na walinzi wachache.

Kitendo hicho kimetajwa kama kitendo cha aina yake chenye UADILIFU kilichookoa MAMILIONI YA PESA ambayo yangetumika kwenye msafara wa magari yasiyopungua sita.

Tuupinge kwa nguvu zote huu upuuzi, mwendo wa mita 200 katika uhalisia wake mtu anaweza kupanda gari na msafara?

Je, kama Leo imeonekana ni ajabu ina maana siku zote ndivyo ilivyo?
Je, kutembea mita 200 ni kubana matumizi?
Ni habari za namna gani hizi jamii inapewa?
Ina maana Dodoma leo kuanzia asubuhi hakukuwa na habari nyingine zaidi ya hii?

Hii breaking news imeniacha na maswali mengi.
 
Mwisho wa ku quote ni wapi na maoni yako yameanzia wapi??? Punguza jazba Mkuu.

Hehehe watu wengine bwana!!
Sasa tupinge nini!!
Naona kama ninyi wenyewe ndio mnakuza vitu
Mkiishiwa hoja
Mnatafuta sababu za hovyohovyo

Nina hakika tangu umeamka hadi sasa hivi haujatembea huo mbali wa mita 200. Tuache kulalamika lalamika kama wanawake.
Mahaba niuwe....ukipenda chongo huona kengeza! Ukipenda pengo huona mwanya
 
Hayo ni maoni ya wanainchi kulingana na mada yako na wala si taarifa rasmi toka ofisini ya Waziri Mkuu.

Isikupe shida kabisa,nadhani alitoka kufanya zoezi la kutembea na kusalimia wanainchi may be hiyo asb kama mila za kiafrika tu.
Ni kweli imagine sasa haya ndio maoni na mwandishi kaona aripoti...sijasema ni taarifa ya serikali tafadhali
 
Back
Top Bottom