Wako wapi mapedeshee walioimbwa na kugawa pesa kwa wasanii wa bendi?

Habari za week end wadau,

Kwa wale mashabiki wa mziki wa dance nchini,hasa bend za Fm Acadamia,Twanga pepeta,Malaika Bend,Acudo impact,Mashujaa band,Msondo Ngoma,Sikinde n.k mtakua mashahidi katika hili,

Miaka michache iliyopita nyuma kulikua na wimbi kubwa la vibopa,matajiri au kwa jina lingine mapedeshee wa jiji hili la Dsm waliokua wakiimbwa sana na kutajwa tajwa kwenye nyimbo za bendi hizi kila mara au kwenye matamasha ya bendi hizi,hii ilipelekea wao kutawanya au kugawa pesa nyingi kwa wanamuziki husika (hasa wenye asili ya Congo) na kwa mashabiki pia hasa dada zetu wa bongo movie na wasanii.

Wakati mwingine walikua hata wakigawa dola ya mmarekani na euros.

Jambo la kushangaza siku hizi siwasikii wala kuwaona wakifanya kufuru hizo,
Napatwa na mashaka pengine nini kimewakuta?au wameamua kwenda kutapanya nchi za jirani kama Malawi na Msubiji?

Wadau unaweza mtaja pedeshee uliyekua unamwamini sana kwa kutapanya au moja ya tukio uliloshuhudia akitapanta.

Binafsi nakumbuka kufuru ya Pedeshee Ndama mutoto ya ngombe na Pedeshee Bitus dhahabu...wadau wakubwa wa Fm Academia wazee wa Ngwasuma popote pale ndani ya jiji hili hasa Mango Gardern na maeneo mengine.
Nakumbuka kufuru aliyofanya Ndama mtoto wa ng'ombe kwa Fary Ipupa hadi Ipupa akapagawa kidogo amsahau jidada bonge Yasmine ,kumbe ni hela ya sembe,sijui kesi yake ya kutakatisha pesa ya sembe imeishia wapi.
 
Ridhiwani Kikwete bado yupo ila haendi tena China baada ya ndege yake iliyokuwa na makontena ya powder kuwa seized na yeye kupewa STOP ya kukanyaga China mpaka anakufa. Tunasikia yeye zake siku hizi ni Mzoga na Chalinze tu kupelekea wazee baiskeli mbovu na kugawa magodoro ya kunguni kwa wasiojiweza.
Hahaaaaaaaaa
 
Kwa mara ya mwisho alionekana akipanda daladala ya Gongo la Mboto kwenda Posta baada ya matumaini kuishia Sheikh Amri Abeid,ila akina Musukuma,Lugola,Tibaijuka ni watu wabaya sana wamemuacha mwenzao solemba mchana kweupe pee
jamaniiii!!
 
Ridhiwani Kikwete bado yupo ila haendi tena China baada ya ndege yake iliyokuwa na makontena ya powder kuwa seized na yeye kupewa STOP ya kukanyaga China mpaka anakufa. Tunasikia yeye zake siku hizi ni Mzoga na Chalinze tu kupelekea wazee baiskeli mbovu na kugawa magodoro ya kunguni kwa wasiojiweza.
 
Ndama Mutoto ya ng'ombe
Chicago Matelefoni
Papaa Musofe
Chief Kiumbe
Na wengine wako Wapi?
Tumewamiss sana, hata muziki wa bendi umedorora kwa ukimya wenu
Hivi huyo chief Kiumbe ndo yule mtaalam wa karate na judo au?
 
Naelekea lusaka kwenye onyesho la Koffie Olomide , hii nchi yenu yenye majonzi siku zote nawaachieni kwa muda .

Bendi zote zimekufa kwa ukata uliotokana na dhiki kubwa iliyolikumba Taifa , imebaki police jazz band tu wana vangavanga
 
Unaenda kuangalia onyesha la mpiga mateke wanawake halafu kesho ndio uje upande majukwaani eti ni muokozi wa wanawake,buure kabisa .
 
Back
Top Bottom