Usiku huu umekuwa mgumu sana

Mar 21, 2024
23
118
Ni semester ya mwisho sasa (6 semester), performance yangu hapa Duce ipo nzuri sana by the way hadi sasa Kwa semester tano za nyuma na average GPA ya 4.3.

Lakini, Sina furaha kabisa kwani ndoto zangu za kusoma Master naona zinayeyuka, my family economic status is too bad. Nashidwa hata ku afford chakula sometimes.

Tamaa na shauku yangu ni endele na masters ni ndoto yangu kuwa university tutor, lakini naona hii ndoto inakwenda kufa.

Wakuu, mtu anae jua process za kupata sponsorship anielekeze.

Maskini Mimi!!

Bachelor of science with education biology and chemistry.
 
Jitahidi ukaze semester ya mwisho umalize na Gpa ya jumla hiyo hiyo 4.3

Hapo lazima utapata udsm merit scholarship ya kusoma masters bure.

Sababu kuu ni unasoma masomo ya sayansi.. hayo masomo yana scholarships sana
 
Elewa ndoto Mkuu. Hiyo ni kazi ya ndoto yake ambayo anaona inaenda kukwama kwa ugumu wa maisha katika familia yao.

Hayo ni mambo mawili tofauti.

Issue ni kuwa kama anataka kuwa lecturer, huwa kuna posts za tutorial assistant ambao huitaji bachelor degree na akipata, hapo anapata sponsorship hata akitaka kusoma hadi PHD

Na kama ni ugumu wa maisha kwa sasa, kama yupo chuo na hana boom. Kwa semester zote alizokaa ni nadra kukosa alternative ya hapo hapo chuoni, unless ni Mambo ya ada na matumizi mengine compulsory,

Yote kwa yote naamini sponsors watamuona
 
Usikate tamaa, mapito ni magumu lakini amini ipo njia katikati ya unayopitia ambayo huwezi kuiona endapo ukikata tamaa.

Ndoto yako ingali hai, endelea kuongeza bidii huku ukitafuta ufadhili.
Usisahau kumuomba Mungu.
But ana degree tayari anaweza omba TA, kikubwa GPA.
 
Mshukuru Mungu kwa yote na hilo ni kubwa pia la kuwa na GPA kubwa hivyo kwa hapo DuCE .
Ila jitahidi kaangalie mechi ya Simba na Yanga maana hapo ni karibu alafu jumatatu nenda ofisi za DC hapo DUCE omba kuonana na MR .Sheu Mutabazi , lecturer wa DC mwaka wa kwanza mpe salamu mueleze shida yako.
Ila ukimkosa mtafute mmama mmoja akiwa Dean of student miaka ya zamani nisijue yupo au hayupo tena akiitwa Madam Pendo nenda msimulie haya unayoyaota hakika ipo siku utanitafuta kunipa walau hela ya bia moja .
Zaidi wambie umewiwa kuwashirikisha ndoto zako na unahitaji wakusaidie , mimi hata ukinitaja
 
Hapo hapo shikilia maliza kwanza ,halafu scholarship ni bwerere hata vyuoni wanatangaza hapo hapo.

Usiwe na wasi umefika mbali sana haswa kweny performance...
 
Ni semester ya mwisho sasa (6 semester), performance yangu hapa Duce ipo nzuri sana by the way hadi sasa Kwa semester tano za nyuma na average GPA ya 4.3.

Lakini, Sina furaha kabisa kwani ndoto zangu za kusoma Master naona zinayeyuka, my family economic status is too bad. Nashidwa hata ku afford chakula sometimes.

Tamaa na shauku yangu ni endele na masters ni ndoto yangu kuwa university tutor, lakini naona hii ndoto inakwenda kufa.

Wakuu, mtu anae jua process za kupata sponsorship anielekeze.

Maskini Mimi!!

Bachelor of science with education biology and chemistry.
Wewe bwege kweli ,watu waache kusaidia masikini wenye mahitaji ya muhimu waje kukusaidia wewe upate masters kisha urudi kuwatambia.
 
Scholarships zipo nyingi sana Mkuu, utachagua unahitaji kusoma nchi gani na kozi gani, we komaa semester hii uue vizuri pia. Wengine tulishindwa kupata hata Gentlemen GPA.
 
punguza wenge kijana. mpe hi doctor senguro msellemu, Dr Naives Kinunda, Dr Ayo, Dr Mhajida, Dr Vakolavene hao wote ni History department Duce. Mungu abariki kazi za mikono yao kwa kunifanya niwe mwl wa history.
 
Back
Top Bottom