Ushauri: Ununuaji wa magari

VVTI ni new technology ni bora kuliko previous Engine Technology.
Chukua Vitz ya cc chini ya 1000.

Starlet zimeshapitwa na wakati, meaning hakuna production from Year 2000.
 
Wadau nahitaji Mark X ya kuanzia mwaka 2000 na kuendelea, je naweza pata kwa Shs ngapi?
 
Naomba msaada wa ushauri nataka kununua gari aina ya pick up ambayo nafikiri itanisaidia sana katika shughuli zangu za kila siku lakini huku nilipo pickup zinazopatikana ni Mitsubishi L200 na Ford Rangers. Wenye uzoefu mnisaidie ipi kati ya hizi mbili inafaa kufuatana na hali yetu ya Bongo!
Asanteni
 
Ni vema ukatafuta TOYOTA, hii itakupa unafuu kwenye gharama za uendeshaji kwani vipuri vinapatikana kwa wingi, unaweza ukaagiza moja kwa moja Japa jaribu Trust Car Company au Autorec

Kila la kheri.
 
Ni kweli kabisa Toyota itakufaa sana maana zinadumu sana na vipuri bei chee na ziko kwa wingi.
 
Toyota itakufaa - ni ngumu, roho ya paka, spare parts zipo, ukitaka kuiuza itatoka.
 
Asante sana wakuu lakini huku niliko Toyota Hilux hazipatikani na ikipatikana bei yake kubwa sana
 
Wewe uko wapi na unataka kuipeleka wapi hiyo pick up? Kula Ford Ranger kaka, jembe la ukweli: siku hizi hukosi spea kaka, dunia imekuwa kijiji, unaweza kuagiza spea yoyote popote!
 
mpangwa1, Hayo magari mawili uliyoyataja ni 'bomu' tu. Kama una pesa si unaweza nunua Toyota popote? Au hiyo hela yako imefungamanishwa na mahali ulipo?
 
Mitsubishi L200, pickup single cabin. Fuel consumption ipo poa, four wheel drive yake ipo bomba. Vipuli vyake vyapatikana. Inadumu fresh tu.
 
Habari zenu wana JF.

Nipo katika maandalizi ya kurudi Tanzania ili kuja kulitumikia taifa. Nahitaji kununua gari, ila kabla sijanunua nilikuwa napenda kufahamu upatikanaji wa spea parts na bei kwa ujumla (juu, au wastani kama magari mengine eg.Toyota) kwa huko Tanzania. Gari ambayo nataraji/ningependa kununua ni either Volkswagen (Golf,Polo au Passat), Peugeot(307).

Naomba ushauri wenu kwa wenye na ufahamu wa hayo magari.

Natanguliza shukrani zangu.
 
sirgeorge, Polo au VW sioni kama ni gari nzuri kwa nchi kama Tanzania,naona nyingi zinaungua ukisafiri long distance,
nimewahi kuwa na Suzuki Escudo nafikiri ni nzuri, Toyota the best, Subaru Forester not sure lakini ni gari nzuri vilevile,
ila kama unataka ukaishi Dar usinunue gari mzee, sidhani kama Dar ni mahali pazuri pa kuendesha gari yako kwa sababu ya traffic.
 
Polo au VW sioni kama ni gari nzuri kwa nchi kama Tanzania,naona nyingi zinaungua ukisafiri long distance, nimewahi kuwa na Suzuki Escudo nafikiri ni nzuri, Toyota the best, Subaru Forester not sure lakini ni gari nzuri vilevile, ila kama unataka ukaishi Dar usinunue gari mzee, sidhani kama Dar ni mahali pazuri pa kuendesha gari yako kwa sababu ya traffic.
Asante kwa ushauri wako Mr.Mbeki nitaufanyia kazi. Na vipi kuhusu Ford (focus) na hiyo Peugeot (307)? spea?
Ngoja nisubiri na maoni ya wadau wengine. Huwa ninaishi Dar, ila kwa jinsi mizunguko yangu ilivyo mingi kutokana na kazi zangu kwa kweli suala la gari halikwepeki.
 
Karibu, ufikirie gari ambalo litahimili mambo yafuatayo:
1. Traffic jam
2. Barabara mbovu za Dar kama ile ya Mwananyamala na zinazojaa maji wakati wa mvua
3. Ubabe wa madereva wa daladala. So hilo nalo la kuliwazia unapotaka kununua gari, muhimu angalia liwe na ubavu kutanua na subira kwenye foleni
Asante kwa ushauri wako Mr.Mbeki nitaufanyia kazi. Na vipi kuhusu Ford (focus) na hiyo Peugeot (307)? spea?
Ngoja nisubiri na maoni ya wadau wengine. Huwa ninaishi Dar, ila kwa jinsi mizunguko yangu ilivyo mingi kutokana na kazi zangu kwa kweli suala la gari halikwepeki.
 
Polo au VW sioni kama ni gari nzuri kwa nchi kama Tanzania,naona nyingi zinaungua ukisafiri long distance, nimewahi kuwa na Suzuki Escudo nafikiri ni nzuri, Toyota the best, Subaru Forester not sure lakini ni gari nzuri vilevile, ila kama unataka ukaishi Dar usinunue gari mzee, sidhani kama Dar ni mahali pazuri pa kuendesha gari yako kwa sababu ya traffic.
Mkuu hiyo gari USIPIME, ni moto.

Ninayo Subaru Forester SF5-2000cc, gari hizi ukizitazama kwa umbo ni rahisi kukosea na kuzifananisha na corolla!
Hii gari ni 4WD na engine ni 2000cc. sawa na Chaser.

Kwa kuridhika nayo nimechukua tayari model ya mbele SG5-2000cc,Cross sports,4WD, Manual/Automatic gear box.
Ni moto sana tu vile vile.

Kizuri hakikosi kasoro
1. Bei yake si chini ya $6,000-7000 (mwaka 2002 kuendelea)
2. Spare zake ghali
3. Watu wengi wanaiogopa

Strong points
1. Engine ya sports, revs up to 8000rev/min
2. Si rahisi kuiharibu, ni gari madhubuti(ukiliganisha na Chaser,corolla etc)

The choice is yours. Ni moto vile
 
Mwenzenu ninataka kuagiza gari, but nataka the most fuel economical car kwa kuzingatia hali ya foleni nchini Tanzania. Sasa nina option hizi mbili. Mitsubishi Pajero Jr (cc 1100) ya 1995 CIF yake ni around 2000, Na nyingine ni Suzuki Kei (cc 660) ya mwaka 2000 CIF yake ni 2000.

Ninajua kwamba kutakuwa na ile dumping cost, but kwangu ni nafuu, kwa kuzingatia kwamba magari aina hii ya mwaka 2002 bei zake zipo juu sana. Sasa ninaomba mnishauri ipi kati ya hizi ni better? Pili kwa magari kama haya inaweza ikanigharimu bei gani kuyatoa pale bandarini? Maana ile calculator ya TRA imenishinda kuitumia.

Nitashukuru sana kwa ushauri wenu.
 
Mkubwa sina uzoefu sana na hili ila nitajibu kutokana na nilivyosikia kwa wadau mbalimbali, kuwa gharama za kulitoa pale bandarini andaa mahela yanayokaribia hela ulonunulia au nusu ya bei ulonunulia, hope wengine watakuja kuongezea hapo wenye ujuzi zaidi

Lukolo
 
Mkubwa sina uzoefu sana na hili ila nitajibu kutokana na nilivyosikia kwa wadau mbalimbali, kuwa gharama za kulitoa pale bandarini andaa mahela yanayokaribia hela ulonunulia au nusu ya bei ulonunulia, hope wengine watakuja kuongezea hapo wenye ujuzi zaidi
Thanks mkuu. Ila kuna watu wamenitisha kwamba eti jamaa wanacalculate kwa kuangalia bei ya hiyo gari mpya kwa sasa, wanatafuta deprecion, halafu ndo wanafanyia mahesabu hapo. Inasemekana gharama uliyonunulia hawahesabii. Hapo ndo pananitia uoga kidogo.
 
Mwenzenu ninataka kuagiza gari, but nataka the most fuel economical car kwa kuzingatia hali ya foleni nchini Tanzania. Sasa nina option hizi mbili. Mitsubishi Pajero Jr (cc 1100) ya 1995 CIF yake ni around 2000, Na nyingine ni Suzuki Kei (cc 660) ya mwaka 2050 CIF yake ni 2000.

Ninajua kwamba kutakuwa na ile dumping cost, but kwangu ni nafuu, kwa kuzingatia kwamba magari aina hii ya mwaka 2002 bei zake zipo juu sana. Sasa ninaomba mnishauri ipi kati ya hizi ni better? Pili kwa magari kama haya inaweza ikanigharimu bei gani kuyatoa pale bandarini? maana ile calculator ya TRA imenishinda kuitumia.

Nitashukuru sana kwa ushauri wenu.

Gari za mwaka huo zimeshotoka mkuu
 
Back
Top Bottom