Kabla ya kununua gari, hakikisha unajua bei za spea za gari unalotaka kununua

Grand Canyon

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
457
927
Majuzi gari langu lilipata shida. Nilianza kupita maduka ya spea kutafuta spea za gari. Nilishangaa kuona taa tu ya baadhi ya magari zianauzwa hadi milioni 1.5. Tena si magari ya bei mbaya kwamba ikiwa alinunua gari milioni 100 hashindwi taa ya 1.5 m. Baadhi ya magari ni ya bei ya kawaida 15-30 m.

Sasa ikitokea taa za mbele zimepata shida na bima ni 3rd part huu ni mtihani .

Gereji nilikuta magari mengi sana. Fundi alinitajia baadhi ya changamoto ya magari hayo. Moja ni Peugeot bado mpya ila ina shida ya sensor, na sensor imetafutwa bila mafanikio. Gari imeanza kupata kutu.

Nilichojifunza:
Unapotaka kununua gari ni vizuri kwanza kujua upatikanaji wa spea na gharama zake la sivyo ikipata shida itatelekezwa gereji.
 
Kunaa mwamba hapaa ana BMW...imeuwa pump...chuma ipo juu ya mawe mwez umekata amekosa spare bongo....akiagza through sea itafka june.... Soo now n mwendo wa boda boda gooo..
Hiyo ni shida kubwa. Unakuta gari nzuri inauzwa milioni 7-15 unakimbilia kununua kumbe spea hazipatikani au ni bei ghali.
 
Mkuu kama unatumia carina, niambie mafuta yanaendaje
Nilikuwa nafikiria kubadilisha gari.Nimefanya ka utafiti kaangu kadogo,gari ambayo mafuta ni wastani,vipuri vinapatikana kwa urahisi.Ina mwendo na stability.Naona hiyo.Najichanga changa,si unajua sisi makabwela.
 
Mifumo inazidi kuimarika, tutaweza kuoata spea toka nchi yoyote ndani ya siku 14 toka inapoagizwa.

Lina suluhisho
 
Mifumo inazidi kuimarika, tutaweza kuoata spea toka nchi yoyote ndani ya siku 14 toka inapoagizwa.

Lina suluhisho
Kweli. Changamoto inaweza kuwa gharama zake. Mfano umejichanga ukanunua gari milioni 7. Kisha inapata shida unaambiwa spea ipo dukani ila ni Tsh 1.5 m.
Unatoboa kweli?
 
Watu mna mawazo ya ajabu sana, had leo bado hamjui link za kununua spare kutoka kokote duniani? Mnataka nchi nzima tuendesge Carina?
 
Kweli. Changamoto inaweza kuwa gharama zake. Mfano umejichanga ukanunua gari milioni 7. Kisha inapata shida unaambiwa spea ipo dukani ila ni Tsh 1.5 m.
Unatoboa kweli?
Pagumu hapo.

Ndo maana tunanunua gari tunaziweza kuzimiliki na kuziendesha..... sio uwezo wa kuinunua tu.
 
Back
Top Bottom