Ushauri kwa Serikali: Baada ya kuwashughulikia machinga sasa ni zamu ya wauza simu feki wa Kariakoo na Makumbusho

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,341
8,266
Serikali baada ya kuwashughulikia machinga naomba tuwashughulikie wauza simu feki wa Kariakoo, Makumbusho na maeneo mengine.

Saivi kuna sumsung, iphones na nyingine nyingi, zote hizo ni feki.
Serikali iangazie jicho pale Makumbusho, Kariakoo na maeneo mengine mwaga vijana wa TCRA na TBS.

Simu nyingi ni za magendo. hazilipiwi kodi wala nini ndio maana zinaingia zikiwa feki.

Serikali inapoteza kodi nyingi kupitia simu feki. Serikali ikiweza kudhibiti ipasavyo biashara ya simu itaingiza mapato mengi sana.

Ni vyema yale maduka yote ya simu kariakoo, makumbusho na kwingineko wapewe watu maalumu wanaoweza kuuza bidhaa zenye ubora unaotakiwa na taifa hili. Wezi wote na matapeli waondolewe kabisa.

Tukiiheshimu electronic business na kuifanya kuwa quality tutaingiza mapato mengi serikalini.

Kitu cha kwanza tudhibiti importation ya hizo electronics tuhakikishe simu zote zinazoingia ziwe Bora.
Baada ya hapo tudhibiti wauzaji wa simu, tutafute wauzaji maalumu wenye mitaji ndio wauze simu maeneo yote yanayofanya biashara za simu.

Tufanye biashara tuchukue kodi, tuendeshe nchi.

Ukiangalia wauza simu wa maeneo mengi ya Dar es Salaam ni mafundi simu wanauza simu zilezile mbovu na feki. Wanahujumu uchumi wa taifa hili.

Kwanini hayo maeneo serikali isiwape watu maalumu wenye mitaji ndio wafanye biashara kuliko kuwapa wababaishaji.
 
Kwani simu feki zikiingizwa nchini hakuna mamlaka ya kuzikagua kabla ya kumfikia mtumiaji?

Simply ukitaka original usipende cha bei rahisi.
 
Simu feki zilishafungiwa na TCRA. Uzembe wa kutaka kununua vitu vya bei poa barabarani ndio unaokuponza. Kanunue kwenye maduka ya simu.
Saivi kuna sumsung, iphones na nyingine nyingi. Serikali iangazie jicho pale Makumbusho, Kariakoo na maeneo mengine mwaga vijana wa TCRA, alafu simu nyingi ni za magendo. Hazilipiwi kodi wala nini. Ndio maana zinaingia zikiwa feki.
 
Mkuu,kwanini msiagize simu mtandaoni au kununua maduka yenye sifa ? Tatizo ni kupenda zile iPhone 11 za laki nane,hao vijana wameona fursa
 
Mkuu,kwanini msiagize simu mtandaoni au kununua maduka yenye sifa ? Tatizo ni kupenda zile iPhone 11 za laki nane,hao vijana wameona fursa
Mkuu hii ni nchi yetu tuna TCRA, tuna TBS lazima tuhakikishe raia wetu wanauziwa bidhaa huku serikali ikiingiza mapato.
 
Serikali baada ya kuwashughulikia machinga naomba tuwashughulikie wauza simu feki wa Kariakoo, Makumbusho na maeneo mengine.

Saivi kuna sumsung, iphones na nyingine nyingi, zote hizo ni feki.
Serikali iangazie jicho pale Makumbusho, Kariakoo na maeneo mengine mwaga vijana wa TCRA na TBS.

Simu nyingi ni za magendo. hazilipiwi kodi wala nini ndio maana zinaingia zikiwa feki.

Serikali inapoteza kodi nyingi kupitia simu feki. Serikali ikiweza kudhibiti ipasavyo biashara ya simu itaingiza mapato mengi sana.
Tumefungua nchi mangi

USSR
 
I phone yangu nashindwa kupata Google translate offline. Na ile simu ya swali ilikuwa inawezekana.
Inaonyesha ukosefu wa nidhami
Ole Sabaya alikuwa anapita kwenye maduka kutazama wanafanya nini.
Halafu Rais anasema anawaonya panya road, wakati hawa watu wanatuibia.
 
Tatizo la wabongo wengi wanataka kufeki maisha aonekane ana 13 Pro wakati ana feki/kopo alilonunua kwa laki 3 na nusu.

Kama huna huna tu nunua tekno yako au itel maisha yaendelee.
Nasema wacha wapigwe hao jingajinga,hakuna namna wala huruma.
 
Ukiona mmachinga anauza simu eti iPhone ujue jina limeandikwa tu kama Sanlg iandikwe Kawasaki

Utanunuaje iPhone kwa bei ya kitochi
 
Back
Top Bottom