Machinga Kariakoo walalamika kutoshirikishwa katika mchakato wa kupata EFD

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,037
9,926
Mkuu wa Machinga eneo la Kariakoo, Steven Lusinde amesema zoezi la kuwapatia mashine za EFD wamachinga walioko maeneo ya Kariakoo linatekelezwa bila kuwashirikisha bali wamepewa taarifa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa wanatakiwa kupewa mashine hizo za kikodi.

"Niseme ukweli kwamba jambo hili hatukushirikishwa kwa asilimia 100 bali tulikuja tu kupewa taarifa kuwa serikali kupitia Kamishna wa TRA imeamua kwamba wamachinga wa Kariakoo wanatakiwa wapewe EFD mashine," amesema Steven Lusinde, Mkuu wa Machinga eneo la Kariakoo akizungumza na East Africa Radio.

Ikumbukwe kauli hiyo inakuja baada ya kuripotiwa kwa taarifa kuwa Mamlaka ya Mapato (TRA) imeanza kuwasajili Wafanyabiashara wadogo (Machinga) wote waliopo Kariakoo ili waanze kulipa Kodi.

Ikielezwa kuwa ni baada ya kubaini baadhi ya Wafanyabiashara wanakwepa Kodi kwa kusambaza bidhaa kwa Machinga.

Akizungumza na wanahabari jana Jumatatu Desemba 12, 2022 Meneja wa Mkoa wa Kikodi, Alex Katundu amesema tayari machinga 5273 wameshasajiliwa ili kuingizwa kwenye mfumo wa malipo ya kodi wa makadirio.

“Usajili huu unafanyika kwa kila machinga aliyepo Kariakoo kwa sababu tulibaini baadhi ya wafanyabiashara wengine sio waaminifu, haonekani akifanya biashara ila mizigo yake anaisambaza kwa machinga ili akwepe kodi.

“Lakini tunawasajili baada ya kujiridhisha kwamba wote wanaingiza mapato zaidi ya Sh4milioni kwa mwaka, kuna mapato mengi yanapotea hivyo wataanza kulipa kodi” amesema Katundu.

Ikumbukwe mwaka 2017 - 2018 Hayati Rais Magufuli aliagiza Machinga wote nchini kulipa kodi kwa kununua vitambulisho maalumu ambavyo vinatolewa kwa Tsh. 20,000 ikiwa ni malipo ya mwaka mmoja.

Hata hivyo Serikali badae ilitangaza kuondolewa kwa wamachinga kwenye maeneo ambayo sio rasmi hususani kwenye maeneo ya majiji, kwa upande wa Kariakoo zoezi la kuwaondoa wamachinga limekuwa endelevu ambapo hivi karibuni baadhi ya vyombo vya viliripoti taarifa ya baadhi ya Machinga kudaiwa kuondolewa kwa nguvu na kubomelewa mabanda yao.
 
Mtu ana mtaji wa ml 20 halafu hataki kulipa kodi.
muhudumu wa Afya analipwa kima cha chini anakatwa kodi mpaka kwenye nanilioo
Aliyewaita Watanzania wanyonge ALAANIWE KABISA
 
Back
Top Bottom