KERO Upotevu wa maji kata za Kichanga na Tungi Manispaaa ya Morogoro imekuwa ni kero na uharibufu wa miundombinu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Rumanyika Donatus

New Member
Aug 3, 2021
3
1
Kumewekuwepo na upotevu mkubwa wa maji hasa katika sehemu tajwa hapo juu. Hii ni kutokana na miundombinu mibovu hasa ya maji.

Ukitembea hatua chache uanakuta barabara zimejaa maji na maji hayo yanatokana na ubovu wa miundombinu ya maji.

Kila baada ya hatua kumi unakuta maji yanabubujika na hii inapelekea barabara za mitaa kuharibika na kuwa na mashimo na hivyo kusababisha uharibifu wa barabara na kuleta kero kwa watumiaji wake.

Nipende kuwashauri Mamlaka ya Maji MOROWASA kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa maji na kupunguza hasara za kugharamia utengenezaji wa barabara zinazoharibiwa na maji.

Vilevile Mamlaka ijitathimini ni kwa namna gani itaweza kufanya maboresho miundombinu ya maji inayoleta kero kwa wananchi wana maeneo husika.
 
Back
Top Bottom