KERO Morogoro: Wakazi wa Maeneo ya Manyuki mwisho tunateseka kwa Shida ya Maji, yanatoka mara 1 tu kwa Wiki.

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
88
105
Wana morogoro maeneo ya manyuki mwisho tuna teseka na Maji ya Serikari Maana kuna mambomba lakin maji yana toka jumanne tu kila Week

Licha ya kutoka mara 1 bado yanakuwa hayana nguvu kiasi kwamba yanashindwa kupanda kwenye Matenki na kutulazimisha kubebelea Ndoo na Madumu

Sasa hii imekuwa kero kwa mji Kama morogoro. Maji mengi kuna mito ya kutosha kwanini wananchi wa morogoro tusifaidike na mkoa wetu

Maji yanatoka kwetu lakini yanahudumia vizuri mikoa mingine kushinda morogoro hii ni aibu kwa Serikali

MOWASA, Mamlaka ya Maji haisemi shida ni nini na ni lini Changamoto hii itatatuliwa kwani tumeshachoka kuteseka.

Tumekuwa tukilazimika kununua Ndoo au dumu la maji kwa Shilingi 500.
 
Na ukimwambia mtu anunie gari walau atakuwa anaweka ndoo 5 nyuma akitoka kazini anarudi na maji home bado haelewi... Mjinga mmoja yeye hela ya gari kanunua bodaboda then anasema vyote vinalingana maana bei ni moja, sijui akili zinauzwa wapi nimnunulie
 
Hayo Maji Mwanzoni Niliyategemea Sana Toka MORUWASA Ila Ikifika Mwezi Wa Saba Hakuna Hata Hayo Kidogo Kwenye Mabomba Nikaona Bora Nichimbe Kisima Haijalishi Maji Yatakayotoka Ya Kijani/Mekundu Muhimu Yafae Kwa Matumizi

Nikachukua Gari Hapo PUMA VIWANDA Nikachimba Nikapata Maji
Wakaja Home Hao Kudai Eti Kodi Maana Maji Ni Yao Nikawakimbiza Mbali Sana
 
Back
Top Bottom