A
Anonymous
Guest
Huduma ya Majisafi Manispaa ya Morogoro ni kitendawili kilichoshindikana kuteguliwa, mara nyingi maji yanatoka yakiwa machafu
Huduma ya Majisafi katika Manispaa ya Morogoro chini ya Mamlaka ya Moruwasa ni changamoto, mara kwa mara maji yamekuwa yakitoka yakiwa machafu jambo ambalo linatupa mashaka na hofu wakati tukiwa tunayatumia.
Jambo hili limekuwa kero ya muda sasa maana watumiaji tupo kwenye hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuepukika, suala hili limekuwa likisemwa kwa muda mrefu lakini mabadiliko ni kiduchi bado kero hiyo inaendelea kujitokeza mara kwa mara.
Kuna mdau amewahi kuleta hii kero hapa jukwaani lakini hatuoni mabadiliko yenye tija - MORUWASA hivi haya ndio maji safi mnayosambaza manispaa ya Morogoro?
Tunaomba Moruwasa watoke hadharani watueleze changamoto hii inasababishwa nanini na wawajibike kwa uharaka kuchukua hatua maana maji yamebeba usalama wetu kwa asilimia kubwa.
Hatuna taarifa zenye uthibitisho wa moja kwa moja lakini kuna watu wamekuwa wakiumwa matumbo ghafla jambo ambalo upelekea kuhusishwa na changamoto ya maji machafu yanayotoka baadhi ya nyakati kwenye mabomba ya Moruwasa.