KERO Chemba za Baa ya Lavipark - Tegeta zinatiririsha maji machafu barabarani, ni hatari kwa afya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Baa ya Lavipark – iliyopo Tegeta Jijiji Dar es Salaam chemba zake zinatiririsha maji machafu barabarani zaidi ya miezi mitano sasa lakini hatuoni hatua zikichukuliwa.

Tunaomba mamlaka zitusaidie zitusaidie kumuwajibisha mwekezaji wa baa hiyo ambayo ipo Tegeta kwa Ndevu kwenye njia inayoelekea kwenye Chuo cha Mzumbe
photo_2024-04-29_09-39-28 (2).jpg

photo_2024-04-29_09-39-28.jpg
Ni zaidi ya miezi mitano baa hiyo ambayo pia kuna lodge chemba zake zimekuwa zikimwagwa maji machafu kwenye barabara ambayo Watu wamekuwa wakipita hususani wanafunzi wa shule za primary, pia ni maeneo ambayo ni kando ya makazi.

Mamlaka za Mtaa zimeshindwa kabisa kumuwajibisha mhusika kwa sababu jambo hili limekuwa kero ya muda mrefu lakini hakuna jitihada zozote za kuthibiti chemba hizo maana siku zinaenda hali hiko vilevile utafikiri kapewa kibali cha kufungulia chemba.

Cha kushangaza zaidi hata Jeshi la Polisi Kituo cha Tegeta ambao ofisi zao zipo karibu na eneo hilo ambao wana dhamana ya kuhakikisha usalama wa Wananchi unastawi wamezibwa mdomo na kushikwa mikono bila kumchukulia hatua yoyote ya kisheria mhusika licha ya maji taka yanayotoka kwenye chemba hizo kupita kwenye njia ambayo wanaipitia hata wao kila wakati kando na ofisi zao.
photo_2024-04-29_09-40-07.jpg

photo_2024-04-29_09-39-29.jpg
Wahusika wa karibu wanakerwa na hali hiyo kwa kuwa pia maji taka hayo yanatoa harufu mbaya lakini wanashindwa kuchukua hatua zozote za kisheria kwenye ngazi ya Mtaa kwa kuwa mwenye baa hiyo anadaiwa kutumia pesa kujiwekea kinga ya kuwajibishwa kwa watendaji wenye mamlaka hizo kwenye ngazi za Mtaa hata kwa baadhi maafisa wa Polisi wa Kituo cha Tegeta ambao wanafahamu kero hiyo.

Mazingira hayo ni hatari kwa wananchi wanaopita kwenye njia hiyo hususani Watoto ambao wakati mwingine upita kwa kutembea peku kutokana na michezo ya watoto wapokuwa wanatoka shule.

Pia maeneo hayo kuna watu wanafanya biashara mbalimbali ikiwemo biashara za matunda na vyakula kuna muda magari yanapita na kutumua maji hayo jambo ambalo linaweza kupelekea urahisi wa Watu kupata magonjwa yanayotokana na maji taka.

Kwa niaba ya wengine nimejitoa kuwa sauti yao tunaomba mamlaka kumchukulia hatua bila kumfumbia macho ili aweze kukarabati chemba hizo hali ambayo itasaidia kuondoa kero na kuweka mazingira rafiki ya ustawi wa maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom